WAZO LA LEO na Kutekwa kwa Dk. Ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WAZO LA LEO na Kutekwa kwa Dk. Ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Jun 28, 2012.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Watanzania ni wepesi kudanganyika.

  Kipigo cha Ulimboka kimelenga kuwagawa Watanzania ili wasiweze kuona ukweli wa madai ya madaktari na udhaifi wa serikali katika kutekeleza ahadi zao.

  Aidha kwa kipigo hiki watanzania badala ya kujadili mstakabali wa nchi inayoamua kupiga wanaoomba haki inawaadhibu kwa kichapo, wanaanza kutukanana wenyewe kwa wenyewe.

  Utambue kuwa madaktari wakigoma wasigome wao hawataathirika sana kwa sababu ya huduma mbovu ya afya. Ni sisi, hata kama wewe unawapendelea watawala.

  Badala ya kuwauliza hao wanaotumia fedha zetu kwenda India imekuwaje sisi tunakula mbovu mahospitalini na wao ndio waliopewa dhamana ya kuboresha huduma, sisi tunaanza kugombana.

  Ulimboka akifa kwa kwa kupigwa, wewe utakufa kwa kupewa huduma mbovu hospitalini.


  Kalagabhao!
   
 2. j

  jigoku JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Umenena vyema Katulanda,lakini nini kifanyike?na ni kwa vipi,tufanyeje tuondokane na maneno zaidi na iwe ni kwa vitendo zaidi
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Watanzania wengi sana wanakufa kwa kukosa dawa. Madaktari wamegeuzwa kuwa kama eye witness wa wagonjwa wanaokata roho badala ya kuokoa uhai wa wagonjwa hao.

  Inakuwaje serikali itumue nguvu nyingi kuzima madai ya watu wanataka huduma bora kwa watanzania lakini ikae kimya licha wizi wa kutisha (grand theft) unaofanywa na watu wachache?

  Inakuwaje wabunge wa CCM kama Martha Mlata analaumu madaktari wanao dai haki zao badala ya kukemea serikali inafuga wezi?
   
 4. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ndugu Fred Katulanda, Kwanza nakupongeza kwa kuwa na moyo wa uzalendo, Mungu atakubariki !
  Pili, nikujulishe kuwa kuna watu wa aina mbili ambao wao kila kitu hukifanya kama propaganda. Wao upeo wao wa kutafakari ni mdogo sana.
  Kwanza kuna watu wanaitwa wana CCM, pili kuna watu wanaitwa Usalama wa Taifa.
  Unapoona watu wanatetea ufedhuli, upu.mbav u, uhu ni, nk basi ujue ni watu wa CCM au wa Usalama.
  Wao kipaumbele chao ni matumbo yao, na hivyo wanafikiri kwa kutumia matumbo.
  Hawajui kuwa madaktari wanatetea huduma ya afya kwa manufaa yao na watz wenzao. Wala hawakumbuki kuwa hao vigogo wanatibiwa nje na kwenye hosp za kimataifa ambazo zipo tz kwa sasa.
  Kwa hiyo wasituvunje moyo!

  Its just a matter of time !
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sikubaliani na hoja yako kuwa WaTanzania wa siku hizi ni wepesi kudanganyika ,naamini kabsaa hili kwa siku hizi halipo ,siku hizi hadanganywi mtu ,isipokuwa hao wanaodanganya huwa wanajidanganya wenyewe.

  Uwezo waliokuwa nao WaTanzania kuukataa udanganyo bado ni mdogo ,haujafikia kiwango cha kuwatisha wanaodanganya ,WaTanzania wanajua wanapodanganywa sehemu ya kwenda kuukataa uongo huo kwa WaTanzania hao haipo.

  Utaona tunapodanganywa tukikubali tusikubali uwongo utaprevail kwa kuwa hatuna la kufanya.

  Na ikiwa limefanywa hili ili kuwapindisha WaTz naona itakuwa hao wamejidanganya wao ,WaTz kwa muda huu cylinder 12 zote zinafanya kazi. Tanganyika tunaisubiri ,Katiba tunaisubiri uchaguzi tunausubiri. Na yote tutadili nayo kwa uangalifu mkubwa.
   
 6. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  true !!!
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Ila wangapi wanajua hilo kwamba times change? Kuna mzee mmoja nilipata kuongea naye, nikagundua ndio maana mambo hayaendi...wale walio kwenye institution nyeti wanaamini wanajua chochote kitakachoipata Tanzania na dnio maana haya wasiyoyapangilia wanataka kuyazima kwa nguvu zote.
  Ukweli ni kuwa tulipofika sasa watanzania wanataka watawala watimize wajibu wao. Sio porojo tu na longolongo zisizo kwisha
   
 8. mbalu

  mbalu JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katulanda umenena ni kweli kabisa lengo la serikali ni kutugawa watz ili wale wenye maono mafupi yasiyoweza kupenya ukuta waweze kutupa lawama na laana zao kwa madakt, na kuwaacha watawala wakiendelea kupeta na kukimbilia Apollo kwa kodi yangu na yako ambayo wao wachache wamejitengea 6b nasisi wengi wametugawia 5b kwenye upande wa matibabu ya ndani bila aibu kwa seriakali inayojiita ni yakidemokrasi kama si domokrasi. Maisha bora kwa kila mtanzania.
   
 9. m

  mtendakazi Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mm sielewe mbona watanzania tunapenda kuzungumza sana? hoja zenye mashiko mnazo ila tukitangaza maandamano kupinga serikari ya kifedhuri hamjitokezi. hivi wokovu wa nchi hii utaletwa na wamisri waliolala kwenye uwanja wa taharir squire? chondechonde kesho tujitokeze uwanja wa jangwani kudai uhuru dhidi yaserikari dhaifu. kwani macho wanayo lakini hawaoni, masikio wanayo lakini hawasikii, pua wanazo lakini hawanusi. REAL BILA KUBADIRI MFUMO TUTABAKIKULALAMIKA. EEEEEEEEEEEEE BWANA TUKUMBUKE NCHI HII.
   
Loading...