BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Nakumbuka mwaka jana niliona kuna memba mmoja wa JF aliandika kuhusu huduma mbovu zinazotolewa na Hospitali ya K’s iliyopo Mbeya, sikuwa nimeweka umakini sana lakini kilichotokea wiki hii ndio nimeona kweli hiyo hospitali ni ya kidwanzi.
Wiki moja iliyopita nilifika hospitalini hapo si kwa lengo la kutibiwa bali kumsalimia ndugu yangu ambaye ni mtumishi wa Hospitali ya K’s kwa miaka kadhaa sasa.
Baada ya stori zetu za hapa na pale nikabaini kuwa mshkaji hana furaha na sura yake ni kama imekosa nusu, nikamdadidi tatizo nini hakuweza kuniambia, akasema tutazungumza baadaye, kwa kuwa nilikuwa ni mwenyeji wake kwa wiki nzima haikuwa tabu.
aadaye jamaa alinisimulia mambo mengi hasa jinsi watumishi wa hospitali hiyo wanavyopata tabu hasa kiuchumi na kunyanyasika.
Nadhani litakuwa jambo zuri nikimnukuu yeye mwenyewe japokuwa naweza kutoandika moja kwa moja kwa maana ya neno kwa neno alilosema lakini ukimaliza kusima ujumbe utakuwa umeeleweka na kama ni hatua basi Serikali au taasisi husika ziingilie kati kuwasaidia ndugu zetu hao.
“Hospitali ya K’s ina jina kubwa hapa Mbeya lakini ukweli ni kuwa kinachoendelea ndani ni aibu sana, kwanza hapa ninavyokwambia tunadai mishahara ya miezi 9 na huu Juni unaenda kuwa wa 10.
“Mara ya mwisho tulilipwa Februari 2023 lakini nyuma ya haoo kuna mishahara mingine ambayo tunadai, tukiuliza wanatuambia watalipa, mara NHIF hawajalipa, kwa ufupi blabla zinakuwa nyingi.
“Kuna kipindi madaktari waligoma kwa kutolipwa stahiki zao, lakini wakapewa majibu ya shombo kutoka kwa viongozi wa juu wakiwemo wamiliki wenyewe.
“Ilifika hatua jamaa wakaanza kujibu kwa nyodo kuwa hata tukiondoka wao wanaweza kubaki na watoto wao ambao ni madaktari tuko nao hapa, watafanya kazi kama kawaida.
“Kuna muda inafikia watu wanafukuzwa kazi kwa makosa ya ajabuajabu ilimradi tu wasiweze kudai maslahi yao, pia kuna washkaji wengi tu wameacha kazi hapa kutokana na mambo kutoeleweka.
“Kwa ufupi Wafanyakazi tuna hali mbaya na sisi ndio tunaodili na afya za watu, unadhani hapo kuna umakini kweli?”
Hiyo ni sehemu ya maelezo ya ndugu yangu, naomba Serikali iingiilie kati kuwasaidia wana hali mbaya ndugu zetu ambao wanadili na afya za watu, unadhani hapo tutegemee nini?
==================
Updates...
Walipotafutwa kujibu madai hayo kwa nyakati tofauti, Afisa Uhusiano wa Hospitali ya K’s, Suma Kabuje na Meneja wa K’s wote walisikiliza hoja kisha wakaomba muda kabla ya kujibu lakini bado hawajapatikana kutoa ufafanuzi.
Pia soma : Hospitali ya K’s Mbeya mna huduma mbovu