Wazo la biashara au eneo la biashara kwanza.

Wazo la biashara au eneo la biashara kwanza.

SAMWEL98

New Member
Joined
Aug 26, 2020
Posts
1
Reaction score
0
Wadau nauliza wenye uzoefu watusaidie,

Jambo gani ni mhimu kuanza nalo ukiwa unafungua biashara(business)

Unawaza kwanza biashara ya kufanya ndio utafute location(eneo) Au unatafuta kwanza eneo ndio uwaze biashara(business ) ya kufanya.

MMH!?
 
Tafuta wazo la biashara kwanza,

Fanya research ya biashara kiujumla ( Jua Washindani wako )
Fanya research ya bidhaa ambayo umetarget, kuanzia bei ya kununua jumla, bei ya kuuza na faida utakayopata

Ukimaliza hayo rudi uunde mikakati jinsi utakavyowanyakua au kuwapata wateja

Mambo ya ziada, Jifunze na uunde kitu ambacho kitakutofautisha wewe na wafanya biashara wengine, yani uwe umebobea kwenye hicho kipengele ( Mfano kama ni bidhaa nzuri sana, Huduma nzuri sana, Au ucheshi wa aina yake kwa wateja wako, Ama ukarimu usioelekeza kwa wateja wako )
kiufupi uwe na jambo special ambalo litafanya uwin akili na mioyo ya watu ambalo ni special linapatikana kwako tu

Ukimaliza hayo, tafuta location sasa ili uingie field

Note; Biashara yoyote ile mwanzo huwa ni mgumu, Unajua ni kwanini ? Ni kwasababu hakuna anayekujua wala kufahamu bidhaa yako au huduma yako, hivyo mwanzoni ni lazima uwe mvumilivu haswa

Wateja wa mwanzo sio lazima wanunue bidhaa yako, hivyo wakija kuuliza bidhaa na kuondoka bila kununua furahi tuu! Jua unaonekana.

Yangu ni hayo.
 
Back
Top Bottom