Wazo Fyatu: Tulizoea kushangilia "Mtu Kaula"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Mawazo mengine yanaudhi kabisa; yanaumiza, yanachekesha, yanasikitisha na wakati mwingine yanatia huruma - vyote kwa wakati mmoja. Tulizoea sana mtu akipata uteuzi tunasema "kaula". Ukisikia mtu kateuliwa wako watu nyuma wanaanza kushangilia kuwa angalau "mtu wao" kaula kwamba, hivi vyeo vilikuwa na labda vimeendelea kuwa sehemu ya ulaji, siyo utumishi tena.

Niliwahi kuandika huko nyuma kuwa ukishaondoa wazo la "utumishi wa umma" utakuta watu wanaanza "ulaji bila umma". Tukio la jana na labda mengine mengi (kuna jamaa yule wa Morogoro nishamsahau) linatukumbusha tu kuwa kwanza "vyeo ni dhamana" na ukiitwa kwenye nafasi ya serikali (kwa ajira au uteuzi) unaitwa kulitumikia taifa lako.

Huitaji kumuogopa Rais, wala kutetemeka, huitaji kuwa na hofu - kama una uhakika wa weledi wako na uwezo wako. Na uende utumike vizuri, wakati wako ukifika mwisho unaondoka anakuja mwingine. Hakuna mwenye "kiti" chake pale.

Tukilikubali wazo hili, tukaliheshimu basi mtu akiteuliwa au akipata nafasi ni lazima apongezwe lakini pia akumbushwe kuwa ameitwa kutumikia, nchi na wananchi wake. Usifanye sherehe kabla hujaapa, usianze kuaga hadi kuku (kama yule bwana balozi fulani). Tuheshimu hivi vyeo na watu watatuheshimu.

Tusifanye kazi kwa vile tunamwogopa Rais; tufanye kazi kwa sababu tumeanimiwa na Rais, vinginevyo imani ya Rais inaulizwa maana hadi akuteue ujue amekuamini sasa kama wewe mwenyewe hujiamini akikutumbua ndio ameondoa hiyo imani.

Lakini sote tunajua Magufuli huwa anawainua tena hata aliowaangusha, Mwigulu? kama ni Mbunge fanya ubunge wako vizuri na jioneshe kuwa ilikuwa ni siku mbaya tu, huwezi jua.

Nje ya hapo.. tumikieni Watanzania, mjiamini, na kama hamjiamini kateeni hizi teuzi au toeni udhuru, si kuna jamaa mmoja huko nyuma alikataa uteuzi wa Rais ukatenguliwa hata kabla ya kuapishwa? Si lazima uvae hilo joho hata kama halikutoshi au wewe hulitoshiiiii.

Acheni kula, mtaliwa!

MMM
 
Mashabiki wengi wa Magufuli wana "common trait" moja.

Ni watu wenye vijiroho vya kwanini, na wanaopenda kuona watu fulani wanapata shidaaaaaa na fedheha.

Mara nyingi stori zao utawasikia, " aisee enzi za Kikwete kuna jamaa Sinza alikuwa anakula bata, ila sasa hivi katumbuliwa ana hali tete. Magu kiboko!

Sasa hata kama mtu katumbuliwa, mshahara wake utapewa wewe?!!

Pili Magufuli anatumbua watu asiowapenda tu vitu vingine anatafuta visingizio tu, watu wake wote WANAULA na wataendelea KUULA.

Mfano: Prof Muhongo aliwahi kuchaguliwa Nishati na Madini kama kivuli ( angemchagua mtu wake, Kalemani directly wengi wangechonga). So Kalemani aka homeboy is there to stay.

Dotto is there to stay regardless afanye ubovu gani, case study Makonda.

Watu kibao kawatumbua kwa uonevu
 
Nimetoa msimamo wangu tangu jana, Rais hakufikiria kisawasawa juu ya hili.

Unataka kuniaminisha ndulane anamwogopa mh jiwe kiwango kile? Hapana, kuna tatzo pahala sio bure🤔🤔
 
Huyu jamaa bhana..

Kwani nini kimebadilika....
Juz mbunge wa Sumve anawaambia wanachi he is making 11.07M a month
Ukiwa waziri unajumlisha perdiems, VX , Meetings, Power and Extra allowances
Sasa sio kuula,
Acha kiroho cha kichawi we mzee
 
Mawazo mengine yanaudhi kabisa; yanaumiza, yanachekesha, yanasikitisha na wakati mwingine yanatia huruma - vyote kwa wakati mmoja. Tulizoea sana mtu akipata uteuzi tunasema "kaula". Ukisikia mtu kateuliwa wako watu nyuma wanaanza kushangilia kuwa angalau "mtu wao" kaula kwamba, hivi vyeo vilikuwa na labda vimeendelea kuwa sehemu ya ulaji, siyo utumishi tena...
Mnafiki katika ubora wako
 
Mawazo mengine yanaudhi kabisa; yanaumiza, yanachekesha, yanasikitisha na wakati mwingine yanatia huruma - vyote kwa wakati mmoja. Tulizoea sana mtu akipata uteuzi tunasema "kaula". Ukisikia mtu kateuliwa wako watu nyuma wanaanza kushangilia kuwa angalau "mtu wao" kaula kwamba, hivi vyeo vilikuwa na labda vimeendelea kuwa sehemu ya ulaji, siyo utumishi tena..
Huyu aliyetumbuliwa alishawahi kuwa Ded moro akafukuzwa kazi na majaliwa hilo hukulisema. Unekalia unafiki wakusifia watumbuaji wenye matatizo ya akili? Yaani mtu afanye vetting kisha asiguse elimu ya muhusika? Ndivyo mnavyofanya huki usa
 
Ukiwa waziri au naibu waziri kwa Tz ni kwamba 'umeula', huo ndio ukweli hata ubishe.

Huko kuwatumikia wananchi bado hakuzuii wewe 'kuula'.
 
Hivi ukinunua ndege kwa wazungu, kwa 'cash', halafu wazungu waka'kutulija', ... hizo spea za ndege utazitoa wapi?

1607581786671.png
 
Back
Top Bottom