Wazo binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo binafsi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 17, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kikwete ninamfahamu katika sehemu ya ujana wake.Nikiwa Form II yeye alikuwa Form IV.Nilimpenda kwa utendaji wake mzuri aliokuwa nao wakati ule,na hata katika kinyang'anyiro cha urais nikawa ninampigia debe kwa rafiki zangu,nikijua kwamba Kikwete niliyekuwa namfahamu wakati ule ndiye huyo huyo leo,na kwamba anaweza kutusaidia.Sikujua kwamba mazingira yameshambadilisha kiasi cha kutisha!Wenzangu wakawa wananikebehi kwa kuniambia niwape mambo ya msingi ambayo yeye binafsi ameshawahi kuifanyia jamii.Nilishindwa kabisa,hata hivyo nikawa namshabikia kama mtu niliyepewa usembe.Baadae nilitambua kwamba hoja waliyotoa rafiki zangu wale ilikuwa sahihi kabisa,kwamba hapakuwa na jambo lolote la msingi ambalo alishaifanyia jamii mpaka wakati anaingia katika kinyang'anyiro cha urais,kwahiyo hapakuwa na haja ya kumshabikia kwa kuwa hatatufaa kma kiongozi.Nikitafakari utendaji wa Kikwete leo,najikuta nikiyakumbuka maneno ya rafiki zangu wale.Kumbe kile kilikuwa kipimo tosha kweli, kwamba Kikwete asingemudu mikiki mikiki ya majukumu haya mazito.Uchambuzi wangu wa kina kwa ujumla wa utendaji wake unanionyesha kwamba hakuna lolote la maana ambalo Kikwete anaweza kujivunia kwamba kawafanyia wananchi wa Tanzania.Mimi binafsi silioni,kama yapo ni ya kutunga tunga tu na wala sio halisi.Kwa kweli watanzania tutamkumbuka kwa kuturudisha nyuma katika mambo mengi ya msingi,wala sina haja ya kuyataja kwa vile wengi wetu tunayajua.Nadiriki kusema kwamba kama Kikwete atashinda uchaguzi 2010,watanzania tutakuwa tumeibiwa kura.Mungu atusaidie tuvuke 2010 salama.
   
Loading...