Waziri Wassira kizimbani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAZIRI wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Steven Wassira, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam kujibu kesi ya madai, anadaiwa fidia ya sh milioni 90.

Waziri huyo ameiomba Mahakama hiyo iifute hiyo kesi, hukumu itasomwa Aprili 12 mwaka huu.

Ametoa ombi hilo leo wakati anajitetea mahakamani hapo, ameiomba mahakama isizingatie madai hayo kwa sababu hayana msingi wowote.

Mfanyabiashara, Andrew Ngai, amefungua kesi hiyo kuiomba mahakama imuamuru Wassira amlipe fidia hiyo kwa madai kuwa alimsumbua, alimpotezea muda, na pia alimdhalilisha.

Wasira amedia kuwa hana nia yoyote mbaya dhidi ya Ngai na kwamba, anachofahamu yeye ni kwamba walikuwa na uhusiano mzuri hadi alipoanza(Wassira) kudai vigae vyake alivyowekesha kwa mdai.

Kwa mujibu wa Wassira, alifungua kesi dhidi ya Ngai ili kupata haki yake na si kwa sababu ya chuki.

Wassira ameieleza mahakama kuwa, aliwekesha vigae 2,000 kwa Ngai na alikuwa anavichukua kwa awamu kwa maandishi.

Amesema,vilivyobaki 600 alipokwenda kuchukua aliambiwa havipo, baada ya kufatilia akabaini kwamba viliuzwa na kampuni ya Ngai na hivyo akaamua kufungua kesi ya madai na pia ya jinai.

Madai ya Ngai ambaye anamiliki Kampuni ya Siza Cold Storage yanatokana na Waziri Wassira kufungua kesi ya madai namba 211 ya 1999 katika Mahakama ya Kinondoni akitaka mmiliki wa Kampuni ya vifaa vya ujenzi ‘Cargo Building' kulipwa sh milioni sita kutokana na madai kuwa aliibiwa vigae vyake kupitia Kampuni hiyo.

Mahakama ya Kinondoni ilitupa shauri hilo kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya mdaiwa wake, Ngai.

Baada ya kesi hiyo kufutwa, Ngai alifungua kesi ya kupitia kwa wakili wake, Chabruma, anataka kulipwa fidia ya sh milioni 90.
 
Siku zote nilikuwa nikidhani Wassira ndiye mmiliki wa Siza Cold Storage kumbe sivyo au?
 
Back
Top Bottom