TANZIA Waziri wa zamani, Basil Pesambili Mramba afariki dunia kwa ugonjwa wa COVID-19

Waziri wa Zamani, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo agosti 17 akiwa anapatiwa matibabu regency hospital. Mramba alilazwa wiki mbili zilizopita kwa maradhi ya COVID-19.

Kifo chake kimesababishwa na Mshituko wa Moyo(Cardiac arrest)

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa fedha, pia Waziri wa viwanda, biashara na masoko

View attachment 1895289
Basil Pesambili Mramba

Born: 15th May, 1940. Departed: 17th August, 2021. With great sadness, the Mramba’s Family hereby announce the passage of our beloved father, Basil Pesambili Mramba; A life so beautifully lived deserves to be beautifully remembered.

Mzee succumbed to illness at the Regency Medical Center earlier this morning, 17th August; 2021. Given the pandemic situation, the family accepts your sympathies and prayers and asks for privacy.

We will receive visits from Family Members ONLY at his residence on Mawenzi Road, Oysterbay. Further information and program will be shared at a later stage.

The Lord has given, and the Lord has taken away; May God rest his soul in eternal peace. Amen.

Godfrey B. Mramba

======
Huyu ndiye Basil Pesambili Mramba

Waziri wa zamani, Basil Mramba amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 kwa ugonjwa wa UVIKO-19.

Akiwa ni mmoja wa mawaziri waliowahi kufungwa kwa makosa waliyoyafanya wakati wakiwa kwenye nafasi zao za uongozi.

Mramba ambaye amewahi kufungwa miaka mitatu kwa matumizi mabaya ya madaraka alizaliwa mwaka 1940 alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo Uganda na kupata shahada ya kwanza na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha City London kilichopo Uingereza na kupata Shahada ya Uzamili katika Biashara.

Amefanya kazi Serikalini katika nyadhifa mbalimbali. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Rombo kabla ya kuteuliwa kuwa waziri.

Mwaka 2006, Mramba aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2008 ambapo alibaki kuwa mbunge wa kawaida.

Julai 7, 2015, Mramba na Yona walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh5 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.5 bilioni.

Kesi yao ilitokana na makosa waliyofanya wakati Mramba akiwa Waziri wa Fedha na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hata hivyo, Februari 6, 2016, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwabadilishia adhabu viongozi hao wastaafu na kuwa kifungo cha nje wakiwa tayari wametumikia miezi saba gerezani.

Katika kutekeleza adhabu hiyo, viongozi hao walitakiwa kuripoti na kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza – Palestina kila siku siku asubuhi kwa miezi tisa. Walitekeleza adhabu hiyo mpaka walipokamilisha Novemba 5, 2016.

Tangu walipomaliza adhabu hiyo, Mramba hakuonekana hadharani kama ilivyo kwa wastaafu wengine maarufu. Amekuwa kimya kwa kipindi kirefu mpaka alipofariki leo Agosti 17 katika hospitali ya Regency kutokana na maradhi ya UVIKO-19.
R. I. P. Brother Mramba

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Ukiwa mzima na umebalikiwa fanya moja jema la kumkumbusha Mungu duniani akupunguzie adhabu kwa faida ya ulichokiacha duniani.
Jenga nyumba ya ibada,chimba kisima,jenga darasa moja,jenga daraja,nk ambacho walio hai watakitumia hata usipokuwepo.
 
..Ndiye aliyeanzisha SIDO.

..aliongoza mchakato wa kuanzisha TRA.

..akiwa Waziri wa Fedha alihitimisha mchakato wa Tanzania kuingia ktk mpango wa World Bank na IMF kusamehewa madeni.

..baada ya kusamehewa madeni ndipo serikali ilipopata uwezo wa kugharimia miradi mingi ya maendeleo ktk awamu za 4 na 5.

..alipatikana na HATIA ktk kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kusamehe kodi ya shillingi BILLIONI 11.

CC Mlachake

Hapo kwenye hatia (MABAYA) mkuu wapo wengi sana sema tu inategemea ntu na ntu.

Unakumbuka furniture za Bashite?
Unakumbuka maskendo ya kodi yalioihusu home shopping centre na nani alikua nyuma yake
wale waliochukua pesa za escrow na sandarusi waliwahi kutajwa kweli.
Meremeta na kagoda je?

All in all nimekusoma vizuri mkuu
 
Yes he was right and correct many Tanzanians are not productive the solution fir them is to continue eating grass for the nation to prosper and develop.

He was one of the best finance our country hs ever had.

Rest in peace Mwamba
He was best where, in Tanzania?

He studied economics but he was useless and corrupt like other corrupt leaders.

Yes, he did some good stuff like SIDO but he was craftsman.

Nyerere (RIP) gave him THB, it was his biggest corporation in the country by then, you know what he did with it?

Everywhere he went, he messed up and at last he ended up in jail for graft charges.

We should not be making people heroes when they must be held accountable and face consequences for their actions.

RIP Mr Basil Pesambili Mramba.
 
Huyu ndie aliyeua shirika la ndege,akaua reli ya tanga,ilipokufa reli ya tanga baada ya kuhamisha karakana ya reli mji wa tanga ukarudi nyuma.
Ktk watu yafaa makaburi yao yafungwe minyororo na huyu yumo.
Aliona bora ajenge lami hadi kijijini kwake kuliko kuunganisha lami dodoma mwanza.
Wivuu
 
Bogus kabisa huyu sio kisiasa Wala kiuchumi, alikua anabebwa tu na che Nkapa. Warombo wenyewe walishamkataaga kwa matusi yake. Kule Mbeya alikokua mkuu wa mkoa alifanya Nini? Kwanza hakusoma uchumi na alikua haujui.
Acha chuki zako za kijinga ni mchumi mahiri na alipata masters yake miaka ya 80 huko UK
Alijitahid mno alipokuwa wazir wa fedha ndio maana alikaa kipind kirefu
 
Ni Bora wanakufa Mana Kuna watu wameandaa mifumo ya ajira mpaka kwa vizazi ambavyo avijazaliwa,
 
"Hata ikibidi wananchi wale nyasi ila ndege ya Rais itanunuliwa."
Namkumbuka kwa kauli hii ya kijeuri na kiburi.Muumbaji amuweke anapostahili.
 
Waziri wa Zamani, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo agosti 17 akiwa anapatiwa matibabu regency hospital. Mramba alilazwa wiki mbili zilizopita kwa maradhi ya COVID-19.

Kifo chake kimesababishwa na Mshituko wa Moyo(Cardiac arrest)

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa fedha, pia Waziri wa viwanda, biashara na masoko

View attachment 1895289
Basil Pesambili Mramba

Born: 15th May, 1940. Departed: 17th August, 2021. With great sadness, the Mramba’s Family hereby announce the passage of our beloved father, Basil Pesambili Mramba; A life so beautifully lived deserves to be beautifully remembered.

Mzee succumbed to illness at the Regency Medical Center earlier this morning, 17th August; 2021. Given the pandemic situation, the family accepts your sympathies and prayers and asks for privacy.

We will receive visits from Family Members ONLY at his residence on Mawenzi Road, Oysterbay. Further information and program will be shared at a later stage.

The Lord has given, and the Lord has taken away; May God rest his soul in eternal peace. Amen.

Godfrey B. Mramba

======
Huyu ndiye Basil Pesambili Mramba

Waziri wa zamani, Basil Mramba amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 kwa ugonjwa wa UVIKO-19.

Akiwa ni mmoja wa mawaziri waliowahi kufungwa kwa makosa waliyoyafanya wakati wakiwa kwenye nafasi zao za uongozi.

Mramba ambaye amewahi kufungwa miaka mitatu kwa matumizi mabaya ya madaraka alizaliwa mwaka 1940 alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo Uganda na kupata shahada ya kwanza na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha City London kilichopo Uingereza na kupata Shahada ya Uzamili katika Biashara.

Amefanya kazi Serikalini katika nyadhifa mbalimbali. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Rombo kabla ya kuteuliwa kuwa waziri.

Mwaka 2006, Mramba aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2008 ambapo alibaki kuwa mbunge wa kawaida.

Julai 7, 2015, Mramba na Yona walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh5 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.5 bilioni.

Kesi yao ilitokana na makosa waliyofanya wakati Mramba akiwa Waziri wa Fedha na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hata hivyo, Februari 6, 2016, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwabadilishia adhabu viongozi hao wastaafu na kuwa kifungo cha nje wakiwa tayari wametumikia miezi saba gerezani.

Katika kutekeleza adhabu hiyo, viongozi hao walitakiwa kuripoti na kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza – Palestina kila siku siku asubuhi kwa miezi tisa. Walitekeleza adhabu hiyo mpaka walipokamilisha Novemba 5, 2016.

Tangu walipomaliza adhabu hiyo, Mramba hakuonekana hadharani kama ilivyo kwa wastaafu wengine maarufu. Amekuwa kimya kwa kipindi kirefu mpaka alipofariki leo Agosti 17 katika hospitali ya Regency kutokana na maradhi ya UVIKO-19.
"A life so beautiful lived"?seriously !!?
Huyu alikuwa mmoja wa majizi na mafisadi wa Awamu ya tatu,ya Mkapa!!
Huyu aliwahi kusema Bora wananchi wale nyasi ila Ndege ya Raisi itanunuliwa,kumbe ilikuwa deal Ili yeye na mume mwenzie Mkapa,wapige pesa ndefu poleni he was ur father,great man,provider in ur family eyes!
Ila kwetu wananchi,this man deserve to rot in hell and may Almighty grant our wish
 
Ukiwa mzima na umebalikiwa fanya moja jema la kumkumbusha Mungu duniani akupunguzie adhabu kwa faida ya ulichokiacha duniani.
Jenga nyumba ya ibada,chimba kisima,jenga darasa moja,jenga daraja,nk ambacho walio hai watakitumia hata usipokuwepo.
Unaweza kuishi maisha ya kuwajali wengine (kuwapenda kama unavyojipenda mwenyewe) na ukawa umefanya jambo kubwa kuliko hata kujenga nyumba za ibada mia moja. Siyo kwamba napingana na wewe ila nataka tu kuonyesha kuwa siku hizi watu wamekuwa kama wanyama na hawathamini binadamu wengine na ndipi hasa tatizo linapoanzia. Ukiwapenda wenzako hutawafunga jela bila sababu, wala hutaiba fedha zilizotengwa kununua dawa za hospital, wala hutajenga hutatembea na mke wa mtu.....mambo ni mengi.
 
..hivi suala la ununuzi wa ndege ya raisi kwanini analaumiwa mramba peke yake?

..kwanini rais mkapa, na waziri wa uchukuzi[ anayehusika na ndege] wa wakati huo, hawalaumiwi?
 
Kutokana na maneno ya kipumbavu aliyoongea.
Kukaa kimya nako Ni busara lkn ma CCM hawakujui Hilo.
Bilioni 11 zilimfanya ajisahau kabisa (sio Mimi, mahakama ilidhibitisha)
 
Back
Top Bottom