TANZIA Waziri wa zamani, Basil Pesambili Mramba afariki dunia kwa ugonjwa wa COVID-19

Wasomba

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
323
475
Waziri wa Zamani, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo agosti 17 akiwa anapatiwa matibabu regency hospital. Mramba alilazwa wiki mbili zilizopita kwa maradhi ya COVID-19.

Kifo chake kimesababishwa na Mshituko wa Moyo(Cardiac arrest)

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa fedha, pia Waziri wa viwanda, biashara na masoko

1629185914482.png

Basil Pesambili Mramba

Born: 15th May, 1940. Departed: 17th August, 2021. With great sadness, the Mramba’s Family hereby announce the passage of our beloved father, Basil Pesambili Mramba; A life so beautifully lived deserves to be beautifully remembered.

Mzee succumbed to illness at the Regency Medical Center earlier this morning, 17th August; 2021. Given the pandemic situation, the family accepts your sympathies and prayers and asks for privacy.

We will receive visits from Family Members ONLY at his residence on Mawenzi Road, Oysterbay. Further information and program will be shared at a later stage.

The Lord has given, and the Lord has taken away; May God rest his soul in eternal peace. Amen.

Godfrey B. Mramba


======
Huyu ndiye Basil Pesambili Mramba

Waziri wa zamani, Basil Mramba amefariki dunia leo Jumanne Agosti 17, 2021 kwa ugonjwa wa UVIKO-19.

Akiwa ni mmoja wa mawaziri waliowahi kufungwa kwa makosa waliyoyafanya wakati wakiwa kwenye nafasi zao za uongozi.

Mramba ambaye amewahi kufungwa miaka mitatu kwa matumizi mabaya ya madaraka alizaliwa mwaka 1940 alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo Uganda na kupata shahada ya kwanza na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha City London kilichopo Uingereza na kupata Shahada ya Uzamili katika Biashara.

Amefanya kazi Serikalini katika nyadhifa mbalimbali. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Rombo kabla ya kuteuliwa kuwa waziri.

Mwaka 2006, Mramba aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2008 ambapo alibaki kuwa mbunge wa kawaida.

Julai 7, 2015, Mramba na Yona walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh5 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.5 bilioni.

Kesi yao ilitokana na makosa waliyofanya wakati Mramba akiwa Waziri wa Fedha na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hata hivyo, Februari 6, 2016, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwabadilishia adhabu viongozi hao wastaafu na kuwa kifungo cha nje wakiwa tayari wametumikia miezi saba gerezani.

Katika kutekeleza adhabu hiyo, viongozi hao walitakiwa kuripoti na kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza – Palestina kila siku siku asubuhi kwa miezi tisa. Walitekeleza adhabu hiyo mpaka walipokamilisha Novemba 5, 2016.

Tangu walipomaliza adhabu hiyo, Mramba hakuonekana hadharani kama ilivyo kwa wastaafu wengine maarufu. Amekuwa kimya kwa kipindi kirefu mpaka alipofariki leo Agosti 17 katika hospitali ya Regency kutokana na maradhi ya UVIKO-19.
 
Back
Top Bottom