Ukitaka kujua Wasira kazi yake ni nini, ujiulize kazi ya Kingunge Ngombare Mwiru alipokuwa katika nafasi hiyo kazi yake ilikuwa ni nini? Kimsingi hana kazi lakini anastahili kuwa na hadhi ya waziri. Kwa sababu katika ofisi hiyo hiyo ya Rais kuna waziri wa utawala bora, naye kazi yake ni nini? Kwa kuwa hawa wote hawana kazi maalum wala inayoonekana wazi kwa wananchi, haikuwezekana kuzifanya kuwa ni idara tu katika Ofisi ya Rais? Huyu ni Rais wa Matumizi, Rais mlipa fadhila kuliko yeyote aliyewahi kupita ndiyo maana kunakuwa na wizara kama hizo siyo kwa sababu zinahitajika bali kwa vile kuna watu wanalazimika kuwa mawaziri hata kama hakuna wizara zinazowahitaji!