Waziri wa Sanaa na Michezo Palamagamba Kabudi kukutana na viongozi wa Simba, Yanga, TFF na Bodi ya Ligi Alhamisi

Waziri wa Sanaa na Michezo Palamagamba Kabudi kukutana na viongozi wa Simba, Yanga, TFF na Bodi ya Ligi Alhamisi

Rungu la kipepe,na ipo siku fifa watashusha rungu kweli.TUENDELEE KUENDEKEZA SIASA.
 
I have never seen such kind of rubbish in my life.
 
Wazee wa kanuni nao wamekubali kwenda? Wamekubali kwa kanuni ipi sasa harma ya derby kwenda kuamuliwa na wizara?
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.

"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Ofisa mmoja kutoka bodi ya ligi pia alithibitisha kupokea kutoka sekalini kuhusu kikao hicho; "Tumefahamishwa kuhusu kikao hicho na tutahudhuria. Ajenda kuu ni mjadala unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba," alisema ofisa huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi.

Source: Mwananchi
Kwanini 51mba hawajaitwa?
 
Haya ndio mambo yanayofanya Simba na Yanga wawe na vizuri. Kanuni si zipo? Kwa nini usichukue hatua
 
Back
Top Bottom