Waziri wa Nishati ieleze nchi kwanini tuko gizani? Huku Arusha tulilala gizani

Waziri wa Nishati ieleze nchi kwanini tuko gizani? Huku Arusha tulilala gizani

nicholasmari

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2024
Posts
1,940
Reaction score
1,248
Bosi mtajwa hapo juu utueleze umeme una shida gani, jana kuanzia saa 11 jioni huku Arusha umeme ulikatika na haukurudi mpaka tunaenda kulala. Asubuhi tuliukuta bila kujua ulirudi saa ngapi. Leo tena umekatika kuanzia mida ya saa 5 asubuhi mpaka sahizi haujarudi.

Kuna tatizo gani tuelezwe maana maisha yetu yanategemea umeme, bila umeme mkono hauendi kinywani. Au ni kwamba watumishi wa TANESCO wanaihujumu nchi kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu? We Dr. Biteko kazi yako imekuwa kufungua warsha, mikutano, vikao kazi na vitu vinavyofanana na hivyo.

Kama vipi hivyo vyeo vitenganishwe apatikana waziri wa nishati atakayeshughulikia nishati tu si kuchanganya na mambo mengine. Vinginevyo msije mkajiaminisha ushindi wa mserereko na labda kwa kuwa chadema hawashiriki uchaguzi.

Jaribu kuthamini maisha ya wananchi tayari tuna kero nyingi msituongezee zingine kwa uzembe wa watendaji
 
Jitahidi kuwa na uandishi mzuri ili hata Boss wako mtajwa hapo juu akipita kusoma aweze kukuelewa kirahisi.
 
Back
Top Bottom