Niweke bayana kabisa, kitaaluma mimi ni mhandisi, ntayoyaandika hapa ni kutokana na uzoefu wangu kwenye kada hii.
Naamini Mheshimiwa Biteko utapita hapa na utapata chochote kitu. Inawezekana kabisa umwfanya makubwa wizara ya madini, ila wizara hiyo inawagusa watanzania wachache sana, hivyo leo hii ukimuuliza mtanzania wa kawaida ni nini umefanya wizara ya madini, hawezi kujua, maana hayamuhusu kwa namna yoyote ile kwenye maisha yake ya kila siku.
Sasa upo kwenye wizara yenye mahusiano ya kila siku ya mwananchi, hususani kwenye bidhaa za umeme na mafuta. Hapa ni rahisi sana kujenga au kubomoa image yako kwa jamii. Inawezekana si kwa kupenda ila baada ya Samia kuona makelele yamekuwa mengi wewe ndio mtu pekee uliyeonekana unawezaa okoa jahazi.
Niende moja kwa moja kwenye hoja
1. Wawekezaji wengi wamekuwa wakipigwa danadana pale wanapotaka wekeza kwenye uzalishaji wa umeme, Tanesco imekuwa ikiona wawekezaji kama competitors na sio collaborators, ni vyema sasa Tanesco ikagawanywa kuzaa makampuni mawili, kampuni moja imiliki production ya umeme, nyingine ikomae na transmission & distribution. Hii itaondoa ukiritimba mkubwa sana kwenye uzalishaji wa umeme.
2. Kwasasa mradi wa JK Nyerere ndio imekuwa kama ndoto, ikionekana kama hamna haja ya kuweka nguvu zaidi kwenye vyanzo vipya vya uzalishaji umeme. Nakuhakikishia Waziri, hizo Megawatt 2000 tutazozalisha zitaisha kama upepo na mahitaji yataendelea kuwepo. Kumbuka viwanda vingi vinaongezeka sasa, plus Reli nayo inasubili umeme huo huo.
3. Waziri Biteko, kila mkoa wa Tanzania utenge eneo kwa ajili ya uzalishaji wa umeme jua, atleast shamba litaloweza zalisha kuanzia Megawatt 100. Ukilaunch hii tenda, nakuhakikishia ndani ya masaa 3 mikoa yote itakuwa imepata wawekezaji. Kila mwekezaji apewe miaka 2 kutekeleza mradi huu. Mgao wa Umeme Tanzania utakuwa historia.
4. Waziri Biteko, huko mbugani hawataki badilika kabisa, bado wamekomaa na majenereta sababu wanapata bakshishi kwenye procurement ya mafuta. Malori ya mafuta mbugani si tu yanachangia kuharibu barabara za mbugani, bali pia uchafuzi waa mazingira. Hawa waamuriwe kutumia uzalishaji wa umeme jua na generator situmike tu as standby, teknologia imekuwa, watu hawataki badilika.
5. Waziri Biteko, Pamoja na kwamba inasemwa gas inazalisha umeme kwa asilimia 60 Tanzania, naamini ukiruhusu wawekezaji zaidi, Uzalishaji wa gas unaweza kuongezeka hata kufikia Megawatt 3000 ndani ya miaka 3. Wote tunajua gharama za umeme gas ni ndogo kuliko umeme maji.
Ningeandika mengi zaidi, ila haya yanatosha kukufanya wewe ukumbukwe na vizazi kwa vizazi. Naamini kabisa unaweza tumia muda mdogo sana kufikisha nchi kwenye uzalishaji wa umeme kutoka Megawatt 1500 hadi Megawatt 10,000 ndani ya miaka 4 ukiyafata haya.