Waziri wa Nishati, Dkt. Merdard Kalemani ateua wajumbe wa Bodi TANESCO

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1573651482472.png

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ameteua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) yenye wajumbe nane.

Dk. Kalemani amefanya uteuzi leo Jumatano Novemba 13, unatokana na Rais John Magufuli kumteua Dk. Alexander Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi kingine cha pili.

Rais Magufuli alimteua Dk. Kyaruzi Novemba 9, mwaka huu baada ya kuwa ameshika wadhifa huo kuanzia Mei 2016 hadi Mei 2019.

Dk. Kalemani amesema wajumbe hao wapya watakaa madarakani kuanzia Novemba 13, mwaka huu hadi Novemba 12, 2022.

Amewataja wajumbe hao kuwa ni Balozi Dk. James Nzagi (alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco iliyomaliza muda wake) na Dk. John Kihamba (Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Saam – DUCE).

Wengine ni Dk. Lugano Wilson (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uhandisi na Mkuu wa Teknolojia za Nishati – Tirdo), John Kulwa (Mkuu wa Idara ya Ukaguzi Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi – MUHAS) na Denis Munumbu (Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – Takukuru).

Wengine ni Dk. Gemma Modu (Mkurugenzi Nacte), Mathew Kirama (Mkurugenzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma) na Gilay Shamika (Mjumbe katika bodi iliyopita).

Dk. Kalemani alimpongeza Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua tena Dk. Alexander Kyaruzi kuisimamia Bodi hiyo.

Alimtaka Mwenyekiti huyo kulitumikia Shirika kwa Kasi, weledi na nidhamu ili kuwahudumia watanzania kwa kuondoa kero ndogo na kuifanya heshima ya Watanzania kwa Tanesco iendelee.

“Ni matumaini yetu mtakuja na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya katika kutekeleza azma ya Hapa Kazi Tu ili kulipa nguvu Shirika letu,” amesema Dk. Kalemani.

Kwa wajumbe wote, aliwataka wachape kazi ili kuhakikisha wadau wa Tanesco wanafaidi huduma nzuri na kuhakikisha Umeme unawafikia watanzania wote.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Dk. Kyaruzi amemshukuru Rais Magufuli kwa heshima kubwa kwake kwa kumteua tena kulisimamia shirika hilo.

Amesema Tanesco miradi mingi ya kimkakati ukiwamo Mradi wa Kufua Umeme wa Maporomoko ya Maji wa Julius Nyerere wa megawati 2,115 na wa Rusumo mkoani Kagera.

Amesema miradi hiyo na mingine wataisimamia kikamilifu kwa kuweka mikono yao humo kwa kufuata miongozo mbalimbali wanayopewa na viongozi wao.

Chanzo: Mtanzania
 
Naona uteuzi unaenda na trends zile zile alizozisema spika za kuangalia 'misonge' kama kwa CAG.
Ila tukumbushane tu kama vetting mechanisms zimeshindwa na kugeukia kwenye hizo A's, msisahau kwamba watu wengi katika awamu hii hii wamegundulika kuwa na vyeti fake na hapo bado 'elimu fake'. Watu wengi waliofanikiwa katika shughuli zao (business/ujasiliamali) wana elimu za chini na kati na wala si hiyo misonge!
 
WAchagga miaka hii wanasoma namba na vile JIWE hatoki mpaka 2035 aisee waendelee kuuza mbege huko kiraracha
 
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ameteua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) yenye wajumbe nane.

Dk. Kalemani amefanya uteuzi leo Jumatano Novemba 13, unatokana na Rais John Magufuli kumteua Dk. Alexander Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi kingine cha pili.

Rais Magufuli alimteua Dk. Kyaruzi Novemba 9, mwaka huu baada ya kuwa ameshika wadhifa huo kuanzia Mei 2016 hadi Mei 2019.

Dk. Kalemani amesema wajumbe hao wapya watakaa madarakani kuanzia Novemba 13, mwaka huu hadi Novemba 12, 2022.

Amewataja wajumbe hao kuwa ni Balozi Dk. James Nzagi (alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco iliyomaliza muda wake) na Dk. John Kihamba (Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Saam – DUCE).

Wengine ni Dk. Lugano Wilson (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uhandisi na Mkuu wa Teknolojia za Nishati – Tirdo), John Kulwa (Mkuu wa Idara ya Ukaguzi Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi – MUHAS) na Denis Munumbu (Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – Takukuru).

Wengine ni Dk. Gemma Modu (Mkurugenzi Nacte), Mathew Kirama (Mkurugenzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma) na Gilay Shamika (Mjumbe katika bodi iliyopita).

Dk. Kalemani alimpongeza Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua tena Dk. Alexander Kyaruzi kuisimamia Bodi hiyo.

Alimtaka Mwenyekiti huyo kulitumikia Shirika kwa Kasi, weledi na nidhamu ili kuwahudumia watanzania kwa kuondoa kero ndogo na kuifanya heshima ya Watanzania kwa Tanesco iendelee.

“Ni matumaini yetu mtakuja na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya katika kutekeleza azma ya Hapa Kazi Tu ili kulipa nguvu Shirika letu,” amesema Dk. Kalemani.

Kwa wajumbe wote, aliwataka wachape kazi ili kuhakikisha wadau wa Tanesco wanafaidi huduma nzuri na kuhakikisha Umeme unawafikia watanzania wote.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Dk. Kyaruzi amemshukuru Rais Magufuli kwa heshima kubwa kwake kwa kumteua tena kulisimamia shirika hilo.

Amesema Tanesco miradi mingi ya kimkakati ukiwamo Mradi wa Kufua Umeme wa Maporomoko ya Maji wa Julius Nyerere wa megawati 2,115 na wa Rusumo mkoani Kagera.

Amesema miradi hiyo na mingine wataisimamia kikamilifu kwa kuweka mikono yao humo kwa kufuata miongozo mbalimbali wanayopewa na viongozi wao.

Chanzo: Mtanzania
Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco na waziri wa nishati ninaomba kukujulisha kuwa mkurugenzi waTanesco Tanzania ana matatizo kwenye utendaji wake especially kupitishwa miradi ya umeme mikoani.unakuta mameneja wa Tanesco mikoani wametuma bajeti za miradi mipya ya kusambaa umeme mikoani kwa wateja, mkurugenzi mkuu wa tanesco anakalia miradi hiyo kwa zaidi ya mwaka mzima bila utekelezaji kuipitisha ifanyike au kutuma fedha ili miradi ufanyike.Hili tatizo limeendelea kuwa kubwa sana haswa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa ambsjo maeneo mengi hayajawahi kupata nishati ya umeme tangu nchi ipate uhuru.ombi tunamuomba mkurugenzi mkuu wa tanesco apitishe miradi iliyotumwa kwake na meneja wa Tanesco mikoa na ipo mezani kwake ili utekelezaji wa miradi hiyo uweze kufanyika kwa wakati .Tunatarajia atasikia kilio hiki ili siku ya kupiga Kura October 28,wananchi wasipigie kura gizani kwani Mh Rais Alisha toa ahadi ya kila mtanzania kupata nishati ya umeme.
 
Tanesco Wana matatizo Sana,

Wanaita watu kwenye interview halafu wanafuta mchakato wa ajira, nahisi labda waliopita sio watu wao ndio maana. Tendeni haki.
 
Back
Top Bottom