msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Mawaziri wote kwenye viapo vyao huwa wanaapa kuhifadhi, kuitetea na kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kiapo hicho ni sheria na hupaswa kufuatwa kwa mtu yeyote anayepewa dhamana ya uwaziri kwani anakuwa anafanya kazi kwa niaba ya Rais wa nchi.
Jambo la kushangaza badala ya kuilinda katiba, waziri wa Tamisemi mhe. Ummy mwalimu amekuwa kinara wa kuvunja katiba na sheria za nchi kwa matamko yake ambayo amekuwa akiyatoa.
Tamko la kwanza ni kuhusu kupiga marufuku uhamisho kwa walimu
kama tunavyofahamu 'uhamisho' ni haki ya msingi ya kila mtumishi na hakuna anayeweza kuzuia haki hii kwakuwa ipo kwa mujibu wa sheria.
Lakini katika hali isiyotarajiwa, waziri ummy amepiga marufuku walimu wa vijijini kuhamia mjini kwa madai kwamba bado kuna upungufu mkubwa wa walimu katika shule za vijijini.
Ofcourse anaweza kuwa sahihi na dhamira njema lakini suluhisho ni kuajiri walimu wapya na kuwapeleka vijijini kuondoa huo uhaba lakini sio kuzuia uhamisho kwa walimu kwa sababu ni haki yao ya msingi ambayo ipo kwa mujibu wa sheria.
Au kama kuajiri haiwezekani, waziri apeleke muswada bungeni ili itungwe sheria inayoweka zuio kwa walimu wa vijijini kuhamia mjini lakini kwa sasa sheria haimpi mamlaka ya kuzuia 'uhamisho' kwahivyo tunamwomba waziri azingatie sheria za nchi.
Kuhusu walimu kuajiriwa na tume ya walimu 'TSC' badala ya wizara
Waziri ummy ametamka kwamba sasa walimu wataajiriwa na tume ya utumishi wa walimu badala ya wizara
Kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma, tamko hili lina kinzana na sheria kwa sababu tume ya utumishi wa walimu ilianzishwa chini ya kifungu cha 15 cha sheria ya utumishi wa umma. Sheria namba 8 ya mwaka 2002 ambapo kinataja majukumu ya tume kuwa ni kusimamia masuala ya kinidhamu kwa walimu, kusimamia maadili ya walimu, kusajili walimu, kuwapandisha vyeo walimu nakadhalika lakini sio kuajiri walimu
Na kwenye kifungu hicho sheria imeweka wazi kwamba tume ya utumishi wa walimu sio mwajiri wa walimu bali ni mamlaka ya ajira ikiwa na maana kwamba tume ni idara inayotakiwa kusimamia ajira rasmi katika utumishi wa umma na sio kuajiri kwa sababu hilo ni jukumu la wizara.
Vifungu vyote vinavyo eleza haya na msingi wa kuundwa kwa tume ya walimu vyote vipo kwenye sheria za utumishi wa umma kwahiyo ni vyema waziri akavifanyia marejeo ili asiendelee kutoa matamko yanayo kinzana na sheria.