BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Ni matumaini yangu sauti kama hizi za kumtosa Kikwete ili asigombee tena 2010 zinaongezeka zaidi ndani ya CCM na pia nchini kote. Hakuna hata moja ambalo Kikwete alilolifanya tangu aingie madarakani linalostahili kumpa tena awamu nyingine.
Ni Rais muoga sana labda kutokana na yeye mwenyewe kuwa na madhambi yake au kuwa karibu mno na mafisadi ambao walimchangia mabilioni ya kampeni zake 2005 ili aibuke kama mgombea wa CCM.
Bado kuna muda wa kutosha tu wa kuongeza hizi kampeni dhidi ya Kikwete. Tanzania inahitaji Kiongozi shujaa asiyemuogopa yoyote yule, hajawekwa mifukoni mwa mafisadi na atakayekuwa tayari kufanya maamuzi mazito hasa katika kipindi hiki kigumu ambapo nchi imegubikwa na ufisadi na utendaji mbovu vya kutisha.
Kumrudisha tena Kikwete madarakani ni kuangalia zaidi maslahi ya Kikwete na mafisadi badala yale ya nchi na sidhani kabisa kumrudisha Kikwete itakuwa ni maslahi kwa CCM pia.