Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ni Waziri anayeongoza kwa kusifia vitu visivyo na maana

astranaut

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,276
1,021
Huyu ndie Waziri pekee alitumia dakika nyingi kusifia vitu visivyo na maana katika ziara ya Rais Magufuli mjini Mpanda mkoa wa Katavi pale alipopewa mic asalimie wananchi kwa dakika 1.

Yeye alisifia tu namna Rais alivyoweza kuruhusu mapori tengefu na vijiji vilivyokuwa kwenye hifadhi kubakia pale bila kueleza namna gani sasa hatua hiyo itawanufaisha wafugaji na uchumi kuimarika kutokana na mazao ya mifugo.

Aidha alishindwa kueleza mikakati ya kumunufaisha mfugaji pengine kutokana na uwekezaji utakao fanywa na Serikali aidha kwa kuanzisha minada ya mifugo,machinjio ya kisasa,sehemu za kunyweshea mifugo yao,kuhimiza wawekezaji katika viwanda vya nyama,viwanda vya maziwa,n.k

Dakika zote alizopewa alizitumia kusifia mapori tengefu,vijiji kubakia kwenye hifadhi ya misitu na bla bla nyingi sana hivyo kwa mantiki hiyo huyu waziri inabidi amulikwe kwa jicho la tatu je anatosha kubakia kwenye wizara hiyo?
 
yaani kwakweli ukitazama ziara za ngosha hadi utaona aibu...sio huyo w/mifugo & uvuvi tu ni woote hadi wakuu wa mikoa wakipewa kipaza sauti ni kama wanafanya MASHINDANO kwamba nani atasifia zaidi, duh!!
 
Back
Top Bottom