Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Palamagamba Kabudi, azozana na Mwandishi wa habari

Halafu huyu prof. Kabudi ni muongo sana.

Anatumia elimu ndogo ya Watanzania kudanganya.

Eti Waingereza hawamkosoi Trump na Trump hawakosoi Waingereza. Labda tumwekee Twitter za Trump.
 
Mzee Mkapa aliwahi kuwaita waandishi wa Tanzania mabogus,tokea hapo alikataa kuhojiwa na chombo.chochote Tanzania lakini hamkumuelewa
 
My Take:
Kabudi badala ya kushambulia akili za wanaokuuliza maswali kwa nini usitoe majibu?

Mimi amenihuzunisha jinsi anavyotoa majibu ya kejeli kwa muuliza swali!

Mtu anauliza swali, yeye anasema muuliza swali hajui ngoja amfundishe!. Siyo kila muuliza swali hajui mzee, mwingine anataka majibu rasmi ya serikali ili akauhabarishe umma.

Mwandishi mwingine anauliza swali juu ya haki za Binadamu , Kabudi anasema huyo mwandishi aende ofisini kwake ampe nauli aende Zimbabwe, sasa aende Zimbabwe kufanya nini mzee?. Wewe jibu swali tu mzee!

Kabudi huyu ni mwanadiplomasia wetu namba mbili kama siyo namba moja, badala ya kujibu maswali kwa itulivu na unyenyekevu. Yeye anachukulia hiyo hadhara kama sehemu ya kutamba na kuonyesha "anavuojua", kujua ajue lakini atoe majibu ya kutosha na ya staha badala ya kutimia Tekniki za Kudunisha watu ili wasihoji maswali ya msingi!

Hayo majibu anayatolea kwa waandishi wetu ipo siku atatutia aibu akiongea na waandishi wa nje
Diplomasia umejifunza wapi !?
 
I my opinion, I think he does not deserve to be foreigner minister.....!
 
Swali linaongelea (current situation in Zimbabwe )

Huyu kabudi analeta historia..... sasa hivi Zimbabwe hajatulia/hapako Shwari....

Maelezo mengi hajajibu swali zaidi ya makelele yasiyo na tija.

Ngoja aende huko akaulizwe na beberu labda ataelewa.
Very true...mambo ya historia ya akina mwalimu yanasaidia nini kwa sasa? Wamarekani kwa mfano wanasema hawawezi ondoa vikwazo mpaka waone meaningful changes happening in Zimbabwe...sasa kuingia the new president ambaye more or less anatenda yaleyale ya predecessor wake kwenye kukanyaga haki za raia hakuwezi kuwa sababu ya sanctions kuwa lifted !!
 
Kwa upande mwingine mimi nadhani hata waandishi wengi wa habari Tanzania wana matatizo....

Uandishi wa habari si tu usomee Journalism. Ni vyema wakawa na specialization kwa maana ya uandishi wa habari wa kitaaluma....

Mfano;

Invegitigative Journalism (awe na mbobevu kwenye mambo ya ulinzi)....

Educational Journalism (awe mbobezi kwenye maswala ya kielimu na taaluma ya ualimu kwa ujumla).....

International Journalism (mtu awe mbobezi kwenye international relation, politics & diplomacy).....

Vivyo hivyo kwenye fani za afya, siasa, dini, ujenzi, history nk nk....

Na siyo mbaya mwandishi wa habari ukawa mbobezi ktk fani hats zaidi ya mbili, tatu na hata zote zilizopo duniani na wakati huohuo kujisomea na kujifunza kila siku ili kuwa aware na mambo yanayoendelea ktk jamii, nchini mwake na duniani.....

Hii ingewasaidia sana kujiamini na kuzitumia fani zao ipasavyo kwa kuzioanisha na fani mama ya uandishi wa habari kuhoji na kudadisi wanapokutana na viongozi mbalimbali kuzungumza nao na hata namna ya kuwauliza maswali.....

Mimi si mwandishi wa habari, lakini kwa uzoefu wangu wengi wa waandishi hata ktk mkutano huu na waziri huyu, uulizaji maswali wao umejengwa ktk msingi wa hearsays zaidi na wa kitoto sana si kwa sababu wanajua au wamefanya utafiti ama uchunguzi wa kutosha juu kile wanachokiuliza....

Wanauliza maswali hata ambayo mlevi aliyetoka bar na hajaenda shule ya uandishi wa habari anaweza kuuliza.....!!!

Hata ukifuatilia kwenye blogs nyingi ambazo kimsingi zaidi ya 90% ama zaidi zinamilikiwa na wanaojiita "waandishi wa habari"...

Fuatilia wanachokiposti kwenye blogs zao utashangaa. Ni umbea na habari za kijinga jinga tu.....

Na kuna baadhi ya YouTubes Channels mwandishi anayejiita "mwandishi wa habari" anaposti video anasoma habari fulani yeye ameiita " nyeti zilizotufikia" unashangaa hata kusoma na kutamka vizuri na kwa ufasaha maneno aliyoyaandika yeye mwenyewe anashindwa...!!

Sasa mwandishi wa namna anakuwa anatoa picha ya kuwa kichwani hana maarifa ya kutosha zaidi ya kutafuta vijihabari vya udaku na umbea tu wa mitaani naye anaiita "habari nyeti".....

Hawa ndio wanaajiriwa wa chombo fulani cha habari na ndiyo wanatumwa kwenye mkutano (Press Conference) ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania, unategemea nini?

Watasikiliza na ikifika wakati wa maswali ndipo unaposhangazwa na aina ya maswali waanayouliza na......

Kwa hiyo mimi sijashangaa hata kupewa jibu la "uje wizarani nikupe nauli/tiketi ya ndege uende Zimbabwe ukajifunze" kwa sababu ni kweli kiasi fulani wanahitaji kujifunza kama nilivyosema halo juu......!!

Kuonesha kuwa jibu hilo lilikuwa sahihi kwao na wengi wao walilifurahia, walipiga mpaka makofi
ikiwa ni ishara kuwa wamekubaliana na waziei...!!

Hawa ndiyo waandishi wetu na hats sijui mnalalamika na kushangaa kitu gani wakati ni kweli nyie ni weupe kabisa kichwani??
 
Alimjibu vizuri. Kuna baadhi ya waandishi hajui kitu Ila wanjifanya wajuaji. Wacha apewe shule.
Watanzania hasa wenye elimu ya chini wanajifanya wajuaji sana, na muda wote wanataka wasifiwe - 'una akili wewe!'. Kumbe hamna lolote! Na utawasikia wakiponda maprofesor na PhD za watu! Hawataki waelezwe kitu. Wengine utakuta wamepata vicertificate vya uandishi wa habari kwenye vyuo vya mitaani ambavyo siyo accredited. Lakini wanataka watambuliwe na kusifiwa na wabobezi wa taaluma hiyo ya uandishi kama Prof. Kabudi! Wasiambiwe kitu! Na huu umekuwa ugonjwa wa watanzania wengi, kukataa kujifunza zaidi na kuwaponda wenye kuwazidi kielimu. Haishii hapa tu, hii tabia utaikuta kwa watanzania wengi hasa mafundi ambao hawajaenda darasani kusomea haswa ufundi huo. Utamsikia akiponda mainjinia eti hawajui kufanya hiki eti wana degree! Ni mengi sana. Ndiowale wanaomponda mheshimiwa Kabudi. Ndio maana taaluma nyingi zinachukuliwa na waganda na waKenya - wao wanaamini kusomea taaluma fulani ni bora kuliko kubangaiza na kujisifia ujinga na kuwaponda waliokuzidi.
 
My Take:
Kabudi badala ya kushambulia akili za wanaokuuliza maswali kwa nini usitoe majibu?

Mimi amenihuzunisha jinsi anavyotoa majibu ya kejeli kwa muuliza swali!

Mtu anauliza swali, yeye anasema muuliza swali hajui ngoja amfundishe!. Siyo kila muuliza swali hajui mzee, mwingine anataka majibu rasmi ya serikali ili akauhabarishe umma.

Mwandishi mwingine anauliza swali juu ya haki za Binadamu , Kabudi anasema huyo mwandishi aende ofisini kwake ampe nauli aende Zimbabwe, sasa aende Zimbabwe kufanya nini mzee?. Wewe jibu swali tu mzee!

Kabudi huyu ni mwanadiplomasia wetu namba mbili kama siyo namba moja, badala ya kujibu maswali kwa itulivu na unyenyekevu. Yeye anachukulia hiyo hadhara kama sehemu ya kutamba na kuonyesha "anavuojua", kujua ajue lakini atoe majibu ya kutosha na ya staha badala ya kutimia Tekniki za Kudunisha watu ili wasihoji maswali ya msingi!

Hayo majibu anayatolea kwa waandishi wetu ipo siku atatutia aibu akiongea na waandishi wa nje

Prof ananisikitisha Sana namna anavyojibu maswali

Anatunga hoja za kumfanya aonekana anajua

Questions were very simple kwa any diplomatic learned brother
 
Watanzania hasa wenye elimu ya chini wanajifanya wajuaji sana, na muda wote wanataka wasifiwe - 'una akili wewe!'. Kumbe hamna lolote! Na utawasikia wakiponda maprofesor na PhD za watu! Hawataki waelezwe kitu. Wengine utakuta wamepata vicertificate vya uandishi wa habari kwenye vyuo vya mitaani ambavyo siyo accredited. Lakini wanataka watambuliwe na kusifiwa na wabobezi wa taaluma hiyo ya uandishi kama Prof. Kabudi! Wasiambiwe kitu! Na huu umekuwa ugonjwa wa watanzania wengi, kukataa kujifunza zaidi na kuwaponda wenye kuwazidi kielimu. Haishii hapa tu, hii tabia utaikuta kwa watanzania wengi hasa mafundi ambao hawajaenda darasani kusomea haswa ufundi huo. Utamsikia akiponda mainjinia eti hawajui kufanya hiki eti wana degree! Ni mengi sana. Ndiowale wanaomponda mheshimiwa Kabudi. Ndio maana taaluma nyingi zinachukuliwa na waganda na waKenya - wao wanaamini kusomea taaluma fulani ni bora kuliko kubangaiza na kujisifia ujinga na kuwaponda waliokuzidi.

Hivi namna ulivyoandika utakuwa ni hao makada wa vijiwe vya Lumumba. Hata huo u proffessor hujui ni kitu gani ??

Unaona ni sawa mtu akiitwa professor atembee na taulo pamoja na misuaki kwenye briefcase na kulala kwenye vigodoro ofisini huku akitumiwa na CCM

Na unaona wengine ni sawa hata akiwa ni mwizi wa kura maadamu ni professor haya tu
 
Kwa upande mwingine mimi nadhani hata waandishi wengi wa habari Tanzania wana matatizo....

Uandishi wa habari si tu usomee Journalism. Ni vyema wakawa na specialization kwa maana ya uandishi wa habari wa kitaaluma....

Mfano;

Invegitigative Journalism (awe na mbobevu kwenye mambo ya ulinzi)....

Educational Journalism (awe mbobezi kwenye maswala ya kielimu na taaluma ya ualimu kwa ujumla).....

International Journalism (mtu awe mbobezi kwenye international relation, politics & diplomacy).....

Vivyo hivyo kwenye fani za afya, siasa, dini, ujenzi, history nk nk....

Na siyo mbaya mwandishi wa habari ukawa mbobezi ktk fani hats zaidi ya mbili, tatu na hata zote zilizopo duniani na wakati huohuo kujisomea na kujifunza kila siku ili kuwa aware na mambo yanayoendelea ktk jamii, nchini mwake na duniani.....

Hii ingewasaidia sana kujiamini na kuzitumia fani zao ipasavyo kwa kuzioanisha na fani mama ya uandishi wa habari kuhoji na kudadisi wanapokutana na viongozi mbalimbali kuzungumza nao na hata namna ya kuwauliza maswali.....

Mimi si mwandishi wa habari, lakini kwa uzoefu wangu wengi wa waandishi hata ktk mkutano huu na waziri huyu, uulizaji maswali wao umejengwa ktk msingi wa hearsays zaidi na wa kitoto sana si kwa sababu wanajua au wamefanya utafiti ama uchunguzi wa kutosha juu kile wanachokiuliza....

Wanauliza maswali hata ambayo mlevi aliyetoka bar na hajaenda shule ya uandishi wa habari anaweza kuuliza.....!!!

Hata ukifuatilia kwenye blogs nyingi ambazo kimsingi zaidi ya 90% ama zaidi zinamilikiwa na wanaojiita "waandishi wa habari"...

Fuatilia wanachokiposti kwenye blogs zao utashangaa. Ni umbea na habari za kijinga jinga tu.....

Na kuna baadhi ya YouTubes Channels mwandishi anayejiita "mwandishi wa habari" anaposti video anasoma habari fulani yeye ameiita " nyeti zilizotufikia" unashangaa hata kusoma na kutamka vizuri na kwa ufasaha maneno aliyoyaandika yeye mwenyewe anashindwa...!!

Sasa mwandishi wa namna anakuwa anatoa picha ya kuwa kichwani hana maarifa ya kutosha zaidi ya kutafuta vijihabari vya udaku na umbea tu wa mitaani naye anaiita "habari nyeti".....

Hawa ndio wanaajiriwa wa chombo fulani cha habari na ndiyo wanatumwa kwenye mkutano (Press Conference) ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania, unategemea nini?

Watasikiliza na ikifika wakati wa maswali ndipo unaposhangazwa na aina ya maswali waanayouliza na......

Kwa hiyo mimi sijashangaa hata kupewa jibu la "uje wizarani nikupe nauli/tiketi ya ndege uende Zimbabwe ukajifunze" kwa sababu ni kweli kiasi fulani wanahitaji kujifunza kama nilivyosema halo juu......!!

Kuonesha kuwa jibu hilo lilikuwa sahihi kwao na wengi wao walilifurahia, walipiga mpaka makofi
ikiwa ni ishara kuwa wamekubaliana na waziei...!!

Hawa ndiyo waandishi wetu na hats sijui mnalalamika na kushangaa kitu gani wakati ni kweli nyie ni weupe kabisa kichwani??

Ndugu yangu , nchi zilizoendelea utakuta hata waziri mkuu anaulizwa maswali na mwanafunzi wa Chekechea na hujibu kistaarabu.

Niliona clip moja Rais Putin wa Urusi ametembelea hospitali na alikutana na mtoto wa chekechea na akaulizwa maswali na hakumpuuza alimjibu , hata kuna clip nyingi nimeziona za Waziri wakuu wa Sweden , Norway wakiulizwa maswali na watoto wadogo wa primary na chekechea na wakijibu maswali kistaarabu

Viongozi wa CCM kwa kujiona ni wababe wameshalemaa katika kutumia nguvu na kejeli hata hawa wanaojiita Ma professor ndio wamelemaa baada kuingia kwenye genge la wachawi
 
Watanzania hasa wenye elimu ya chini wanajifanya wajuaji sana, na muda wote wanataka wasifiwe - 'una akili wewe!'. Kumbe hamna lolote! Na utawasikia wakiponda maprofesor na PhD za watu! Hawataki waelezwe kitu. Wengine utakuta wamepata vicertificate vya uandishi wa habari kwenye vyuo vya mitaani ambavyo siyo accredited. Lakini wanataka watambuliwe na kusifiwa na wabobezi wa taaluma hiyo ya uandishi kama Prof. Kabudi! Wasiambiwe kitu! Na huu umekuwa ugonjwa wa watanzania wengi, kukataa kujifunza zaidi na kuwaponda wenye kuwazidi kielimu. Haishii hapa tu, hii tabia utaikuta kwa watanzania wengi hasa mafundi ambao hawajaenda darasani kusomea haswa ufundi huo. Utamsikia akiponda mainjinia eti hawajui kufanya hiki eti wana degree! Ni mengi sana. Ndiowale wanaomponda mheshimiwa Kabudi. Ndio maana taaluma nyingi zinachukuliwa na waganda na waKenya - wao wanaamini kusomea taaluma fulani ni bora kuliko kubangaiza na kujisifia ujinga na kuwaponda waliokuzidi.
Umejiwakilisha vizuri Sana

This is you representing what you have written
 
Back
Top Bottom