Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa anahujumu miradi ya maji, nchi, na Serikali ya Awamu ya Tano

Dispensa

New Member
Oct 31, 2019
3
2
Husika na maada tajwa hapo juu.

Mim ni mdau mkubwa wa maji nmekuwa nikishirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo kuchimba visima vidogo na vikubwa maeneo yenye uhitaji mkubwa hasa kwenye kambi za wakimbizi.

Pili niipongeze wizara ya maji kufanikisha uundwaji wa RUWASA hii itasaidia kupunguza urasimu mkubwa uliokuwa ukisababishwa na halimashauri nyingi hapa chini kufanikisha miradi ya maendeleo hasa madiwani, pamoja na pongezi hizo pia ningependa kuelimishwa.

Ninaruhusu michango yenye kujenga sio kejeli na matusi.

Tunatambua kuwa kila mwaka serikali imekuwa ikitenga bajeti ili kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo. Mwaka 2018/19 wizara ya maji ilitengewa fedha ili kutekeleza miradi ya maji katika maeneo mbali mbali hapa nchini. Miradi au zabuni za miradi hii ilianza kutangazwa mwezi april 2019, chakusikitisha ni kwamba tunaingia mwezi Novemba, karibia nusu ya mwaka wa fedha 2019/20 miradi hii bado haijaanza kufanyika, pia tukumbuke kuwa 2019/20 wizara pia ilitengewa fungu tena la kutekeleza miradi mingine, tunajua fedha hizi za bajeti huwa hazitoki zote lakini mbona hata hzo kidogo zinazotoka hatuoni matunda yake kama kwenye barabara, umeme, majengo na miundombinu mingine?

Nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa Ziara za Waziri wa Maji kuna kauli ambazo amekuwa akizitoa mara nyingi sana, naomba kunukuu mojawapo ambayo ndiyo inanifanya niandike uzi huu. "Wakandarasi wa maji ni wahuni, wababaishaji, wanaomba miradi kwa gharama za juu hivyo wamekuwa wakiitia hasara serikali"

Naomba kuelimishwa au kuuliza maswali machache yafuatayo.

1. Ni nani anafanya feasibility study, inventory, project cost estimates kati ya mkandaraasi na client(Wizara ya Maji)
2. Sheria za manunuzi zinasemaje kuhusu mchakato wa kutafuta mzabuni anayefaa kutekeleza mradi?
3. Kwenye evaluation ya miradi ya hakuna kipengere kinachoangalia gharama za mradi, je ikitokea bidders wote wameomba kwa gharama za juu huwa mnafanyeje au wakandarasi huwa wanawalazimisha kuwapa miradi kwa gharama wanazotaka wao?
4. Wizara imejipanga kutekeleza miradi kwa Watalaamu wa ndani, je watalaamu hawa ni tofauti na wale waliokuwa wakifanya kazi hizo hapo awali?
5. Umejaribu kufanya ulinganifu wa gharama za material mnazouziwa serikali na wanazouziwa watu wa kawaida?

Makame Mbarawa amefanya kazi Wizara ya ujenzi na uchukuzi tulitegemea uzoefu uliopata pale uuhamishie Wizara ya Maji, Eng. Mfugale anasifika kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi ya barabara hakuanza kwa kuwatukana wakandarasi, alianza kwa ku review gharama zile pale alippona zina dosari mwisho wa siku amefikia mafanikio haya tunayoyaona leo.

Nina uhakia mafanikio ya TANROAD, TARURA, REA yanatokana na hatua nzuri za kusanifu miradi na usimamizi mzuri wa utekelezaji wake. Wizara inataka kusanifu miradi, ijenge, ijikague yenyewe na kukusanya mapato pia, siamini kama hili litawezekana, miradi mingi itatekelezwa chini ya kiwango kwa sababu mtekelezaji ndo mkaguzi, sitegemei ajikosoe badala yake atafunika kombe mwanaharamu apite.

Nashauri kazi ya RUWASA na Idara za Maji iwe Kusanifu, Kusimamia utekelezaji pamoja na kukusanya mapato kama zinavyofanya taasisi zingine ili ziweze kujiendesha.

Kwa nini nasema Waziri anahujumu

1. Kwa nini unachelewesha miradi kuanza, nini kinatafutwa hapa, kuvuka mwaka wa fedha bila kutekelezwa bajeti iliyotarajiwa huku wanachi wakiendelea kuteseka kila siku? Lengo lako unataka serikali ionekane imeshindwa kupeleka maji vijijini ilihali fedha imetengwa na kutolewa huku ukijifanya mzalendo kwa kuwatukana wakandarasi ambao wamekuwa wazalendo kwa kuvumilia madeni ya wizara yako leo hii unawaita wababaishaji na wahujumu uchumi. Walipeni madeni ili na wao waendelee na Maisha mengine
2. Kuna miradi ambayo wamesitisha mikataba na wakandasi, na sasa anafanya kwa Wataalamu wa ndani kama Muwasa, Mwauwasa, Kashiwasa n.k cha kushangaza miradi hii inafanyika kwa gharama zile zile zilizokuwa zikituma na makandarasi, je faida inayopatika hapa hapa inaenda wapi?
3. Naamini sasa ana bajeti ya miaka miwili mkononi 2018/19 pamoja 2019/20 ni lini tutegemee kuona mafungu haya mawili yakimtua mama ndoo kichwani?
4. Umetafakari athari za kiuchumi zinazoweza kujitokeza baada ya kuamua kufanya biashara hii kujenga miradi hii maji. Serikali haiwezi kufanya biashara ikakusanya na kodi pia huo ni uongo.

Leo nimeanza na Mbarawa, kesho nitaweletea S.J*fo +M******* Builders

1. Ni nani anafanya feasibility study(upembuzi yakinifu), inventory project cost estimates(makisio ya gharama za miradi)
 
Maji Maji Maji Maji,Maji Maji Maji. Hapa hapa ndo tunapitia awamu hii.
 
Usiseme Mbawara ahahujumu serikali sema Mbawara anawalaza njaa nyie wachimba visima. Mara ngapi tumeona visima vinachimbwa kwa gharama ila havitoi maji?
 
Usiseme Mbawara ahahujumu serikali sema Mbawara anawalaza njaa nyie wachimba visima. Mara ngapi tumeona visima vinachimbwa kwa gharama ila havitoi maji?
Sijasemea visima, pia labda nikuambie kwanza visima serikali haiwezi kuchimba visima, kwenye visima hatujaguswa tunapeta tu
 
Sijasemea visima, pia labda nikuambie kwanza visima serikali haiwezi kuchimba visima, kwenye visima hatujaguswa tunapeta tu
Kwa hiyo waziri hajakalia pesa za bajeti ya kuchimba visima? Au hizo pesa za kuchimba visima inatoka wizara tofauti?
 
Rudi kwa huyo aliyekutuma uje umchafue Mzee Mbarawa ili Yeye achaguliwe na uwe unaotea Kitambi chako Kwake kwa Kudoea Chakula chake kuwa huyo Waziri hatotoka hapo katika hiyo ' docket ' kwa huu ' Upuuzi ' uliouanika hapa. Tena kwa Kukusaidia tu ni kwamba Waziri Mbarawa yuko hapo sana tu na hata ' Bwana Mkubwa ' anamkubali na ana imani nae Kubwa mno japo kuna muda ' Upole ' wake wa Kizanzibari nadhani unaochagizwa na ' Ucha Mungu ' wake ndiyo huwa unamgharimu Kiutendaji.
 
Pamoja na kumlaumu Prof. Mbarawa lazima uelewe hivi sasa kuna vitu havitumiki kama nyenzo za michakato ya maamuzi. Vitu kama Bajeti, Annual Procurement Plan na, Public Procurement Act vimetupwa kuleee. Yasemekana vinaleta ukakasi!? Kilichobaki ni kufuta maelekezo ya wazee. Huyo Mnzazibari wa watu utamlaumu buree, hana hata moja ajualo.
Yeye hataki ugomvi na mtu, anafanya kama mnavyotaka nyie. Mkitaka siasa atawapa siasa, mkitaka utaalamu atawapatia. Wanzabari wanamsemo bora yesheee, kugombana na mtu ni kutaka. Yawezekana amekukwaza, lakini ujumbe utamfikia.
 
Atakuwa anatumiwa na mabeberu tu huyu bila shaka, atumbuliwe tu atupishe tumechelewa sana.. By MATAGA..
 
Mwamuzi ni mtu mmoja sasa yeye ndio anaamua wapi hela iende na kwa mradi gani
Pamoja na kumlaumu Prof. Mbarawa lazima uelewe hivi sasa kuna vitu havitumiki kama nyenzo za michakato ya maamuzi. Vitu kama Bajeti, Annual Procurement Plan na, Public Procurement Act vimetupwa kuleee. Yasemekana vinaleta ukakasi!? Kilichobaki ni kufuta maelekezo ya wazee. Huyo Mnzazibari wa watu utamlaumu buree, hana hata moja ajualo.
Yeye hataki ugomvi na mtu, anafanya kama mnavyotaka nyie. Mkitaka siasa atawapa siasa, mkitaka utaalamu atawapatia. Wanzabari wanamsemo bora yesheee, kugombana na mtu ni kutaka. Yawezekana amekukwaza, lakini ujumbe utamfikia.
 
Japo maji ni tatizo,lakini mleta mada unaonekana ni muathirika wa miradi iliopigwa chini
Lazima utakua katika wale wa 65 waliofyekwa kwa kula hela za maji
 
Back
Top Bottom