Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso , Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Awesowote wanaoshiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Maji kwa Miji 28, akisisitiza kuwa hakutakuwa na nafasi ya kuongezewa muda kwa wakandarasi watakaoshindwa kukamilisha kazi kwa wakati
Ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao na wakandarasi pamoja na washauri wa mradi huo, ambao katika baadhi ya maeneo umefikia hatua ya asilimia 60 ya utekelezaji. Hata hivyo, alionesha kutoridhishwa na kasi ndogo katika baadhi ya maeneo yaliyosalia nyuma
"Nimechoka kusikia hoja za kuomba muda wa nyongeza. Mara hii hatutajadili suala hilo. Tumekubaliana kazi imalizike kwa wakati na lazima hilo litekelezwe," alisema kwa msisitizo Waziri Aweso
Ametaja baadhi ya miji inayotakiwa kuwa imemaliza kazi kufikia Septemba hadi Oktoba 2025 kuwa ni Handeni, Korogwe, Muheza, Pangani, Kilwa Masoko, Manyoni na Geita, huku miji ya Ifakara, Njombe, Makambako, Sikonge, Kasulu na Mpanda ikipaswa kukamilika kufikia Desemba 2025
Aidha, Waziri Aweso alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza juhudi za kuimarisha huduma ya maji nchini, pamoja na kuishukuru Serikali ya India kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kufanikisha mradi huu. Pia alitoa pongezi kwa jamii na mamlaka za serikali za mitaa kwa uvumilivu wao wakati mradi ukiendelea kutekelezwa
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, alisisitiza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya pande zote zinazohusika ni muhimu ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi huu haukwami katika hatua yoyote
Mradi huu unalenga kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa Watanzania zaidi ya milioni 6.9, kwa kuongeza upatikanaji wa maji kwa wastani wa asilimia 5 maeneo ya mijini na asilimia 3 vijijini
Thamani ya mradi ni zaidi ya shilingi trilioni 1.58, ambapo miji 24 inatekelezwa kwa msaada wa kifedha kutoka Serikali ya India (Sh. trilioni 1.167), na miji mingine minne inatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani zenye thamani ya Sh. bilioni 413
Chanzo: ITV