PreGE2025 Waziri wa Maji Jumaa Aweso akagua Ujenzi wa Ofisi za RUWASA na kugawa Magari 19 kwa Ofisi za Makao Makuu na Wilaya

PreGE2025 Waziri wa Maji Jumaa Aweso akagua Ujenzi wa Ofisi za RUWASA na kugawa Magari 19 kwa Ofisi za Makao Makuu na Wilaya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093

1749801277110.png

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na kukabidhi magari 19 kwa ajili ya ofisi za makao makuu na wilaya mbalimbali nchini.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Waziri Aweso alisema RUWASA ilianzishwa kutokana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini, jambo lililopelekea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuona umuhimu wa kuanzishwa kwa wakala huo.

“Leo hii suala la ujenzi wa miradi ya maji vijijini siyo tatizo tena. Namshukuru sana Rais Samia kwa kuwa ujenzi wa taasisi hii unaenda sambamba na mazingira bora ya kazi kwa watumishi,” alisema Waziri Aweso.

Ameeleza kuwa Rais Samia alitoa kiasi cha Shilingi bilioni 24 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya RUWASA, na kupongeza juhudi hizo akisema: “Hakika Rais wetu ni mjenzi. Yote aliyotufanyia tutamlipa kwa kufanya kazi kwa bidii, kwani amefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini.”

Ameongeza kuwa watahakikisha wanamfuatilia mkandarasi kwa karibu ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, na fedha zitatolewa kwa wakati ili kuondoa changamoto au malalamiko yoyote.

“Ujenzi bora wa miradi ya maji unaendana na usimamizi makini na ufuatiliaji wa karibu. Nitahakikisha RUWASA wanapata ushirikiano wote wanaouhitaji ili kukamilisha yote waliyokusudia,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA, Bi. Ruth Koya, alimshukuru Waziri Aweso kwa kuonesha uangalizi wa kipekee kwa taasisi hiyo, akisema magari 19 yaliyotolewa yataongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya RUWASA.

“Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi kumtua mama ndoo kichwani na anaendelea kutekeleza hilo kwa vitendo. Waziri wa Maji naye anatekeleza wajibu wake kwa dhati. Magari haya yatasaidia kufanikisha lengo la Ilani ya CCM ya kuhakikisha huduma ya maji vijijini inafikia asilimia 85 ifikapo mwaka 2025,” alisema.

Katika kikao hicho, Mkuu wa Kitengo cha Ushauri Elekezi wa mradi huo, Bw. Peter Salyeem, aliwasilisha taarifa ya maendeleo ya ujenzi, akieleza kuwa mchakato ulianza Machi


Chanzo: WIZARA YA MAJI TZ
 
Back
Top Bottom