Waziri wa Madini, Angellah Kairuki aelezea vipaumbele vyake

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki aelezea vipaumbele vyake

JINOME

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Posts
958
Reaction score
1,427
FB_IMG_1507713454323.jpg

Waziri wa Madini, Mhe. Bi. Angellah Kairuki ameeleza vipaumbele vyake katika, Wizara kuwa
ni pamoja na

01. Udhibiti wa Utoroshaji wa Madini nchini,
02. Maslahi kwa Wafanyakazi
03. Watumishi kufanya kazi kwa Uadilifu na Weledi wa hali ya juu.

Mhe. Bi. Angellah Kairuki, ameyasema hayo mapema jana Jumanne Oktoba 10,2017, Jijini Dar-Es-Salaam, alipozungumza na Watumishi wa Wizara ya Madini, pamoja na Taasisi zake, waliopo Dar-Es-Salaam, na Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kufahamiana na kupanga mikakati ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa Uchumi wa nchi. Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na

01. Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),
02. Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
03. Chuo cha Madini Dodoma (MRI) pamoja na
04. Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (TEITI).

Amesema kuwa Sekta ya Madini inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwataka wataalam wa madini kubuni mbinu za ukusanyaji wa maduhuli pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye uchimbaji madini.

Katika hatua nyingine aliwataka wataalam hao kubuni mikakati ya kuzuia utoroshaji wa madini nchini ili nchi ipate mapato stahiki. Amewataka watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwa wabunifu ili sekta hiyo iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo, amewakumbusha watumishi kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara, ikiwemo kufanya kazi kwa tija, ili hatimaye Sekta ya Madini iweze kuchangia katika uchumi wa nchi kwa kuwa mchango wa sekta husika bado ni kidogo.
 
Kampuni ya Barrick walipokuwa wanataka kumfukuza kazi Meneja Mkuu wa Mgodi fulani unaomilikiwa na Barrick walikuwa wanamuhamishia Bulyanhulu,yaani hapo hachomoki. Namuhurumia huyu mama kama kweli atapamudu hapo basi ni jembe maana madini ndo sehemu ya kuchomolea mawaziri
 
Huyu mama mwaka jana alisema bungeni , baada ya kumaliza uhakiki serikali itaajiri watumishi kama kawaida wakiwemo walimu wa masomo ya arts, mwisho wa siku mwaka umekatika hakuna utekelezaji, halafu leo tena mtu anakuja na ngonjera mpya.

Huu ujinga wa kuweka wine mpya kwenye vikombe vilivyochoka , sijui tutaacha lini.
 
Maslahi kwa wafanyakazi[emoji7] [emoji7] [emoji7]
 
Kila la Kheri , tumtatikie ufanisi katika wizara yake mpya ili madini yakalinufaishe taifa .pia nina Imani na uwezo wake hivyo dhamira yake imuongoze kuweka legacy mpya katika madini ili wizara hii ikatoe mchango mkubwa katika uchumi wa taifa letu
 
Back
Top Bottom