Waziri wa kilimo angalia hili

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,765
10,639
Wakuu, mnazungumziaje tabia iliyokomaa ya kuuza matunda mabichi? Yaani taifa letu limekuwa la ajabu kwa kuhalalisha mambo ya kijinga kweli kweli. Mfano embe changa, pilipili changa, matikiti machanga na sasa machungwa machanga. Kwa nini serikali imeridhia biashara hii haramu ya vyakula vichanga? Embe zinaliwa kwa chumvi na pilipili kitu kinachokera sana
 
Pole sana mkuu, lakini hapa nawaza tu kwamba.... Kama mlaji hana hitaji na tunda bichi/changa, kwanini anunuwe..??
Na je, hayo maembe mabichi yanayoliwa na wateja tena kwa chumvi, hauoni kama pengine hilo ndilo hitaji lao..??
Kwenye tikiti kidogo ni ngumu kwa mteja kununuwa likiwa bichi ama changa, kwasababu wateja wengi walisha shtuka kwamba anapo nunuwa tikiti lazima ahakikishe muuzaji amelikata (kisambusa) na mteja ajiridhishe kwamba ananunuwa bidhaa aliyo kusudia.
Kwenye pilipili, hapa naona unafanya masihara mkuu... Yaani kweli hauna uwezo wa kutambua tofauti ya pilipili komavu/ama iliyo iva...!!??
 
Vipi kuhusu vipodozi vyenye zebaki? Huoni kuwa ni mahitaji ya mlaji? Kwa nini serikali iingilie kati wakati tayari ilishatoa elimu kwa watumiaji wake?
 
Naona unarukaruka kama maharage yanayo anza kuiva.
Mkuu, nikama haujuwi nini lalamiko ama hoja yako hapa.
Chakula na Vipodozi ni mambo mbili tofauti aiseee
 
Huyu itakuwa kuna dodo lake mtaani alikuwa analikuza ili likomae liive alitafune, Sasa wahuni wameliwahi kwa chumvi na pilipili amebaki kuweweseka. Akitulia ataleta mada inayoeleweka.
 
Naona unarukaruka kama maharage yanayo anza kuiva.
Mkuu, nikama haujuwi nini lalamiko ama hoja yako hapa.
Chakula na Vipodozi ni mambo mbili tofauti aiseee
Wewe ndio unaropoka kama usiyefikiri, hapa ninaongelea afya ya mlaji ilindwe. Usipoweza kufikiri utaelewa mfano? NAZUNGUMZIA AFYA YA MLAJI. Usipoelewa hili utabaki kutapatapa, kuna TFDA inayoshughulikia haya mambo,
 
Wakuu, mnazungumziaje tabia iliyokomaa ya kuuza matunda mabichi? Yaani taifa letu limekuwa la ajabu kwa kuhalalisha mambo ya kijinga kweli kweli. Mfano embe changa, pilipili changa, matikiti machanga na sasa machungwa machanga. Kwa nini serikali imeridhia biashara hii haramu ya vyakula vichanga? Embe zinaliwa kwa chumvi na pilipili kitu kinachokera sana
Sijajua kama kweli zinakuwa changa, nachojua wanachuma kabla hazijaiva ila zikiwa zimekomaa. na ni jambo la kawaida kabisa, fikiri ukivuna embe iliyoiva mbeya unaleta dar litafika kweli? wanalogic kwanini wanafanya hivyo hasa ukizingatia miundombinu ya usafirishaji wa vitu fresh uliopo. ilikuwa vyema kuimarisha iundo mbinu ili mambo yawe powaa zaidi.
 
Hoja nzuti, lakini ukienda sokoni ukweli sio huo. Sio kukomaa, tatizo ni uchanga, nadhani ni kutafuta pesa kwa haraka. Bidhaa iliyokomaa ikikaa muda huiva, mfano maparachichi. Hayo mengine ni machanga kabisa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom