Waziri wa fedha na mipango ataja hatua zilizofikiwa kujenga Tanzania ya viwanda

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
924
1,096
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ATAJA HATUA ZILIZOFIKIWA KUJENGA TANZANIA YA VIWANDA.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mipango ametaja hatua zinazoendelea kutekelezwa na serikali ili kufikia malengo ya uchumi wa Viwanda.
Maeneo hayo ni kupambana na rushwa, kuimarisha miundombinu ya umeme na barabara. Dk Mpango amesema pamoja na juhudi hizo, lengo la kufikia uchumi wa Viwanda siyo la serikali pekee.

Dk Mpango aliyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa Warsha ya 22 ya tafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Repoa. "Serikali inatengeneza mazingira ya uwekezaji,inatoa fursa kwa kila mtanzania anayehitaji kuwekeza lakini ni muhimu kushirikiana pamoja. Kubadili fikra za watanzania ili wajitokeze zaidi katika fursa hii, "alisema.

Warsha hiyo inayofanyika kila mwaka, ina lengo la kujadili changamoto, mbinu, uzoefu na jinsi ya kuimarisha taasisi katika malengo ya uchumi wa viwanda.
 
Fursa gani hiyo anayoizungumzia Waziri? Kuuza pipi kwenye flyover ikikamilika?

Mimi huwa siwaelewi hawa viongozi wetu. Wanafanya mambo ya kunishangaza kila uchao. Wana maamuzi yenye kuwatoa watu 300 kwenye ajira yakiwaingiza watu wawili kwenye ajira huku wanahubiri fursa.

Hivi, kwa mwenendo huu wa biashara na ajira, hivyo viwanda vinavyozungumziwa vitakuwa vya kuzalisha nini, mteja nani na ananunua kwa purchasing power ipi ikiwa unga tu ni gumzo?
 
hoja za kipumbav sana hz,unapanga mikakati bila resource,kama vile wataalam,mitaj na v2 kama hvyo haf unajiita prof! au mtazid kuwakamua wafanyakaz? nch isiyokuwa na dira ya kuandaa rasilimali watu na na kipofu kumwongoza anaeona! mf maguful anawajal wanafunz bila kujal walimu ndio wanaowaandao hao wanafunzi,huu n upumbav ulokithiri ktk nch inayojinad kuwa nch ya uchum wa kati ikitegemea kod kwa wafanyakaz!
 
Samahani watanzania wenzangu kama huyu waziri amesomea uchumi na anaujua uchumi anao zungumzia basi elimu haina umhimu kwa watanzania naona anacho zungumza hakieleweki hata kidogo japo wafuasi wake watasema ameeleweka
 
Hahaha hizo fursa zikowapi na kwa resourse zipi?

Tunamsubiria bungeni atueleze vizuri mwa nini serikali imepeleka 34% tu ya bajeti wakati pesa zimeelekezwa kwenye ujenzi wa Chato International Airport.
 
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ATAJA HATUA ZILIZOFIKIWA KUJENGA TANZANIA YA VIWANDA.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mipango ametaja hatua zinazoendelea kutekelezwa na serikali ili kufikia malengo ya uchumi wa Viwanda.
Maeneo hayo ni kupambana na rushwa, kuimarisha miundombinu ya umeme na barabara. Dk Mpango amesema pamoja na juhudi hizo, lengo la kufikia uchumi wa Viwanda siyo la serikali pekee.

Dk Mpango aliyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa Warsha ya 22 ya tafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Repoa. "Serikali inatengeneza mazingira ya uwekezaji,inatoa fursa kwa kila mtanzania anayehitaji kuwekeza lakini ni muhimu kushirikiana pamoja. Kubadili fikra za watanzania ili wajitokeze zaidi katika fursa hii, "alisema.

Warsha hiyo inayofanyika kila mwaka, ina lengo la kujadili changamoto, mbinu, uzoefu na jinsi ya kuimarisha taasisi katika malengo ya uchumi wa viwanda.

Angeeleza vimeanzishwa viwanda vingapi na vimefungwa vingapi? Vile vile ajira ngapi zimepatikana na zimepotea ngapi katika kipindi chake hapo ningemuelwa kabisa kabisa!!!!
 
Fursa gani hiyo anayoizungumzia Waziri? Kuuza pipi kwenye flyover ikikamilika?

Mimi huwa siwaelewi hawa viongozi wetu. Wanafanya mambo ya kunishangaza kila uchao. Wana maamuzi yenye kuwatoa watu 300 kwenye ajira yakiwaingiza watu wawili kwenye ajira huku wanahubiri fursa.

Hivi, kwa mwenendo huu wa biashara na ajira, hivyo viwanda vinavyozungumziwa vitakuwa vya kuzalisha nini, mteja nani na ananunua kwa purchasing power ipi ikiwa unga tu ni gumzo?
unatakiwa uumize kichwa chako ni jinsi gn utatoka, fursa ziko nyingi. sio usubiri serikali ikupe ajira, kina billgate na wengine waliumiza vichwa vyao ndo wakatoka, hawakukaa wakisuri ajira serikalini.

kazi ya serikali ni kukufungulia njia ili kazi au kipaji chako kisonge mbele na sio kukuajiri.
 
My friend, hakuna...narudia tena HAKUNA nchi yeyote hapa duniani ambayo wananchi wake woooote wanajiandaa kuwa Bill Gates. Hata mimi hapa nazungumzia SERIKALI KUFUNGUA NJIA badala ya kuhubiri siasa za MJIAJIRI MJIAJIRI.

Nikikuuliza wewe binafsi (mwenye akili) kwa nini hauko kama Bill Gates majibu yako yatakuwa kituko. Hapa nilikuwa namuelimisha mwenzio kuwa ni jukumu la SERIKALI kujenga hicho kiwanda anachokisemea kindotondoto ndipo iwe fursa kwa wakulima kulima zaidi. Ikiwa wakulima wamelima vitunguu, basi ni jukumu la serikali kufanya jasho lao lipande thamani kwa kuhakikisha uwepo wa kiwanda cha kusindika mazao, iwe direct au kwa kuwatumia wawekezaji wenye mitaji mikubwa.

Kuhusu ajira serikalini nalo sipendi mijadala yake lakini serikali zote duniani zinahangaika na ajira za wananchi wao. Isionekane kama Watanzania ni wa ajabu saaaaaana kuuliza ajira kwa serikali yao. Juzi tu hapa, profesa mzima na vyeti vyake ameshukuru kama kapewa hela, kisa tu kapewa kazi. Je, kati ya huyu profesa na mkulima aliyeishia darasa la saba huko Kolomije, nani ana nafasi ya kuziona fursa?

Wakati mnatuletea mifano ya wananchi kuwa Bill Gates, muweke na mifano ya marais wetu kuwa Gerald Ford na sio kuishi kwa kutegemea siasa.
 
Kwa viongozi tulionao Tanzania moja ya fursa wanayoiona ni kuhakikisha idadi ya watanzania wenye uwezo wa kufikiri inakuwa kubwa kadri inavyowezekana ili waweze kuila vizuri national cake.
 
Habari kama hii UKAWA hawataki kuisikia
Wewe umeona kuna habari hapo au taarifa? Kumbe hao ukawa sijui, mnawasingizia mengi. Yaani kwa akili yako MANENO: tunaboresha barabara, tunaboresha umeme, jukumu la viwanda siyo la serikali peke yake; Hii ndo mipango ya kujenga viwanda imekamilika hapo!!? Aibu yako, Hata wewe!!!
 
Back
Top Bottom