Waziri wa fedha: Matumizi ya Serikali kuongezeka katika bajeti ijayo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Matumizi ya Serikali yanakadiriwa kuongezeka kutoka Sh33.105 trilioni ya mwaka wa fedha 2019/2020 hadi Sh34.360 trilioni kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 bungeni leo Jumanne Novemba 5, 2019.

Amesema matumizi ya kawaida yanakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 4.7 hadi Sh21.66 trilioni sawa na asilimia 13.7 ya Pato la Taifa na matumizi ya maendeleo yanakadiriwa kuwa Sh12.699 trilioni sawa na asilimia 8.0 ya Pato la Taifa.

Dk Mpango amesema katika mwaka 2020/21 jumla ya misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo inatarajiwa kufikia Sh1.269 trilioni ambapo misaada ya kibajeti (General Budget Support- GBS) inatarajiwa kuwa Sh154.2 bilioni.

Amesema misaada ya mifuko ya pamoja ya kisekta (Basket Funds) Sh172.9 bilioni na misaada ya miradi (Project Funds) Sh941.5 bilioni.

Aidha, amesema nakisi ya bajeti inayojumuisha misaada inakadiriwa kuwa Sh3.943 trilioni sawa na asilimia 2.5 ya Pato la Taifa kwa mwaka 2020/21 ambapo Sh2.355 trilioni zitagharamiwa na mikopo ya nje na Sh1.588 trilioni zitagharamiwa na mikopo ya ndani sawa na asilimia 1 ya Pato la Taifa.
 
Serkali inaongeza matumizi hadi tilion 35.

Je!! Serikali inakusanya tilioni ngapi kwa mwaka huu wa fedha?
Au ndio wameamua kutunyonga kabisa!!
 
Only good on paper for public relations purposes!!! In the last budget, how much did they disburse for development projects?
Ukiwa na kipato cha chini,ni vyema ukawa na matumizi yanayoendana na kipatochako ,na hatakama unaongeza matumizi kwasababu ya maendeleo hata kwa kukopa,basi hakikisha hukopi zaidi ya robo ya wastan wa kipato chako harali.

Haiwezikani kipato chako ni laki 2 kwa mwezi unaenda kukopa laki na nusu,na unatakiwa mwisho wa mwezi uiludishe ikiwa na riba.unategemea familia yako utaindeshaje?

Ni wehu kama tunakusanya tilioni 22 kwa mwaka halafu tuna propose budget ya tilion 35.

Watanzania tupo milion50 -55 .watu wazima wa kufanya kazi wapo chini ya milion30 ,na wenye ajira hawazidi milion 15,unafikili nani atakaelipa hapa.

SIKU MKILETEWA MIKATABA MIBOVU KWENYE RASILIMALI ZEZU,WENYE UZALENDO WAKIJALIBU KUSEMA WANAITWA MABEBELU WANAKOKIWA BUNDUKI.
hovyo kabisa.
 
Tangu jiwe lishike hatamu,hakuna bajeti iliwahi kufanya kazi,faru ndugai na watoto wake wa ndiooooo!!!! Wanaigiza tu

Jiwe ndio kila kitu linaamua bajeti likiwa jukwaani.
 
Back
Top Bottom