Waziri wa Fedha awasimamisha kazi Maafisa Ugani wa Taasisi 6 huku akiwataka Viongozi wa Taasisi hizo kujitathmini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Philip Mpango ameagiza kusimamishwa kazi kwa maafisa ugani wa taasisi sita ili kupisha uchunguzi huku akiwataka viongozi wa taasisi hizo kujipima kama wanatosha katika nafasi zao.

Waziri Mpango ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Septemba 27, 2019 wakati akipokea ripoti ya tathimini ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka 2018/19 ambayo ilionyesha kuwa kulikuwa na udhaifu wa uzingatiaji wa sheria za manunuzi ya umma katika taasisi hizo.

Vilevile, Waziri Mpango pia ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa taasisi zote ambazo miradi yake haina thamani ya fedha na ile ambayo ripoti inaonyesha ilikuwa na viashiria vya rushwa.

Taasisi zinazopaswa kuwasimamisha maofisa ugani wake ni Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Wakala wa Mbuga za Kilimo, Taasisi ya Utafiti wa Dawa (NIMR), Kituo cha Diplomasia, Halmashauri ya Kaliua na Nsibo huku miradi ambayo haina thamani halisi ya fedha ikiwa ni mradi wa uchimbaji wa mashimo ya kuchakata taka ngumu wa Halmashauri ya Kahama na usambazaji wa mita za maji katika halmashauri hiyo hiyo.

“Maofisa ugani wanaohusika wakae pembeni kupisha uchunguzi, tusipofanya hivyo fedha za Watanzania ambao ni walipakodi tutazitumia vibaya. Wale ambao miradi yao haina thamani halisi ya pesa mamlaka zao nidhamu ziwashughulikie natamani wangekuwa hapa ili Takukuru waondoke nao,” amesema Waziri Mpango.

Waziri Mpango aliwakabidhi ripoti hiyo maofisa wa Takukuru na kukiagiza chombo hicho cha kupambana na rushwa kuwashughulikia wote kwa mujibu wa sheria bila kumuonea mtu aibu ili wahusika wote waonje joto la jiwe.

Aidha ripoti hiyo ilizitaja taasisi 12 ambazo miradi yake ilikuwa na viashiria vya rushwa, wizara ya maji, Shirika la Reli Tanzania (TRC) Shirika la viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya maji safi na maji taka, Singida na Wanging’ombe na manispaa za Kigamboni, Ubungo na Kahama.

Pia, ripoti hiyo ambayo ilikuwa ikisomwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA, Balozi Matern Lumbaga ilizitaja Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kama taasisi zilizokiuka sheria na utaratibu wa manunuzi ya umma.
 
Vyuma vitaendelea kukaza. Ingekua Ni amri yangu, magufuli angekaa madarakani mpaka 2035, au sio mazee.
 
Niko Nsimbo huku, nadhani walikuwa wanaondoa mlolongo wa urasimu ili kurahisisha kama vile zinavyonunuliwa ndege.
 
Tangia kuundwa kwa PPRA na CAG, kila report ikitoka kuna ubadhirifu.

Upuuzi ni kwamba wizi unaweza kuwa umefanyika kwenye taasisi au halmashauri ambazo hazikutajwa mwaka uliopita, hila mbinu ni zile zile.

Hapo ndio unaona extent ya uzembe serikarini, inge make sense kama walau wezi wanakuja na mbinu mpya, binafsi ningewapongeza kwa ubinifu hao wezi.

Hila kwakuwa mbinu ni zile zile serikari nayo lazima ichukue lawama wataalamu wameshindwa kuja na effective control measures za kupambana na hili tatizo.

It’s pathetic to say the least na kuna watu humo ndani wanajigamba ni certified ACCA accountants.
 
Duh.....hii nchi sijui upigaji utaisha lini?

Yaani hadi Manispaa ya ubungo inayoongozwa na Chadema imo!!!
Hahahaaahhaha..........wewe utakuwa mchawi....ikitokea kashfa za upigaji serikalini lazima uiangalie kwa jicho la kupinda.
 
Duh.....hii nchi sijui upigaji utaisha lini?

Yaani hadi Manispaa ya ubungo inayoongozwa na Chadema imo!!!
Hahahaaahhaha..........wewe utakuwa mchawi....ikitokea kashfa za upigaji serikalini lazima uiangalie kwa jicho la kupinda.
 
Back
Top Bottom