Shule ya msingi ya lukooni iliyopo wilaya ya Ilala chanika Dsm imeanzisha utaratibu wa kufundisha tuition hapo shuleni kuanzia darasa la tatu mpaka darasa la Saba. Gharama ya tuition kwa kila mwanafunzi ni tsh 300 kwa Siku kwa kila mwanafunzi.
Watoto wanaokosa hela ya tuition wamekuwa wakinyanyapaliwa na hata kufikia hatua ya kutengwa madarasa na watoto wanaotoa pesa ya tuition. Pia kumekuwa na kauli ambazo kwa nanna moja au nyingine ni Kama kauli za vitisho kwa wazazi.
Mfano wa kauli hizo ni Kama ifuatayo:
Nanukuu " Kama hutaki mwanao asome tuition we acha asisome lakini kitakachompata badae usitulaumu" mwisho wa kunukuu.
Utaratibu huu una athari kubwa sana kwaani watoto wamekuwa wakitoka jioni mashuleni. MTOTO ANASHINDA NA NJAA KUTWA NZIMA AKIWA SHULENI. Kuna wakati watoto wanarudi saa kumi na mbili jioni. Hii itapelekea wanetu wapate vidonda vya tumbo kwa kushinda NJAA.
Pili wazazi wengi uwezo wao wa kifedha ni mdogo kiasi Cha kushindwa kumudu hiyo gharama ya shilingi 300 kila Siku. Pia unakua NI mzigo mkubwa zaidi kwa wale wenye mtoto zaidi ya mmoja.
Hivyo Basi tunaomba wahusika akiwepo waziri wa elimu atusaidie juu ya hili.
TUITION ZA LAZIMA MASHULENI NI MZIGO KWA WAZAZI.
Pia kwa mwenye namba ya waziri wa elimu naomba anitumia huko PM ili nimpigie kwaani nahofia anaweza asipate malalamiko yetu haya.