Waziri wa Elimu tunakuomba iangazie jicho Shule ya Msingi Lukooni Chanika, Dar es Salaam

Gatekalii

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
286
500
Shule ya msingi ya lukooni iliyopo wilaya ya Ilala chanika Dsm imeanzisha utaratibu wa kufundisha tuition hapo shuleni kuanzia darasa la tatu mpaka darasa la Saba. Gharama ya tuition kwa kila mwanafunzi ni tsh 300 kwa Siku kwa kila mwanafunzi.

Watoto wanaokosa hela ya tuition wamekuwa wakinyanyapaliwa na hata kufikia hatua ya kutengwa madarasa na watoto wanaotoa pesa ya tuition. Pia kumekuwa na kauli ambazo kwa nanna moja au nyingine ni Kama kauli za vitisho kwa wazazi.

Mfano wa kauli hizo ni Kama ifuatayo:
Nanukuu " Kama hutaki mwanao asome tuition we acha asisome lakini kitakachompata badae usitulaumu" mwisho wa kunukuu.

Utaratibu huu una athari kubwa sana kwaani watoto wamekuwa wakitoka jioni mashuleni. MTOTO ANASHINDA NA NJAA KUTWA NZIMA AKIWA SHULENI. Kuna wakati watoto wanarudi saa kumi na mbili jioni. Hii itapelekea wanetu wapate vidonda vya tumbo kwa kushinda NJAA.

Pili wazazi wengi uwezo wao wa kifedha ni mdogo kiasi Cha kushindwa kumudu hiyo gharama ya shilingi 300 kila Siku. Pia unakua NI mzigo mkubwa zaidi kwa wale wenye mtoto zaidi ya mmoja.

Hivyo Basi tunaomba wahusika akiwepo waziri wa elimu atusaidie juu ya hili.

TUITION ZA LAZIMA MASHULENI NI MZIGO KWA WAZAZI.

Pia kwa mwenye namba ya waziri wa elimu naomba anitumia huko PM ili nimpigie kwaani nahofia anaweza asipate malalamiko yetu haya.
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,656
2,000
Mmmh tunadanganyika na elimu bure za majukwaani!

Wanaopata shida ya ufaulu ni hao hao watoto wetu hohehahe!
Mie siyo mwalimu na wanangu hawasomi St Kayumba lakini nina ndugu jamaa na marafiki walimu, ukiwasikiliza wanachozungumzia kwenye hii elimu bure, utafuta buku jero walau kwa mwezi mtoto aongezewe nguvu.

Elimu, Afya na kilimo nchi hii vinasikitisha sana, namna sekta hizo zisivyopewa kipaumbele cha ukweli.

Nikiangalia matokeo ya juzi, gap la shule za serikali na zile binafsi, itupe mwamko wazazi hawa wanasiasa na vizazi vyao hawasomeshei St Kayumba!

Everyday is Saturday............................ :cool:
 
Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,086
2,000
Nampongeza sana mwalimu mkuu wa hiyo shule kwa hako kautararibu.

Wakati mimi nahangaika kuzipata shule kama hizo wewe unazikataa? Mkuu usidhani matokeo mazuri yanakuja kwa kutegemea masaa ya kawaida ya darasani tuu, inabidi mtoto apate muda wa ziada wa kuboostiwa kama hivo.

Hakuna kitu sitaki kukisikia kama shule za private, napenda sana shule za government lkn zenye walimu wanaojituma kama hiyo shule unayoilalamikia wewe.
Unforgetable
 
vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,572
2,000
Aisee.. wazazi kama wewe ni chenga mno.

1.Kiuhalisia anapokwambia kitakachokuja kumpata mwanao usilaumu (KITAKACHOMPATA MWANAO NI UFAULU MDOGO ZAIDI KULINGANA NA HAO WANAOTUMIA MUDA MWINGI ZAIDI KUSOMA)

2. Watoto kupata vidonda vya tumbo kwa kukaa na njaa, huo kwa mara nyingine unasimama kama uzembe wako mzazi kwenye kutojali future ya mwanao (mpe pesa ya chakula au mpikieni aende na "kontena" shuleni)

3. Jichetue ufahamu na swala la kutaka ubure na ubwete, ila jua dhahiri akifeli mtihani darasa la 7 ujiandae KIBUNDA KIZURI CHA KUMLIPIA PRIVATE SCHOOLS au uamue kumuacha nyumbani uje kutuongezea idadi ya wezi wa kutukaba na kutuvunjia baadae.

4. Ukimpata huyo "piemu" unayemtafuta jitahidi umuulize yeye wanae walisoma shule za aina gani

Hopeless kabisa
 
Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,463
2,000
Siku 5 kwa wiki kila siku tsh 300

5*300=1500/=

Kwa hyo mzazi mwalimu anakusaidia kumsaidia mwanao kwa buku jero kwa wiki

Niwe muwazi mm mwanangu anasoma kayumba lakn napambana kwa hali na mali ili afanikiwe nalipa tuition tsh 30000 kwa mwezi na bado mm mwenyewe nakomaaa nae kila wikend napopata nafas

Kwa Sasa anaingia darasa la tano na matokeo ya std 4 mwanangu kapata wastan wa A kapata daraja B somo moja tu la kiingereza na kapata wastan wa A peke yake darasa la watoto 120

Lengo langu nikukueleza na kukushaur hili suala la elimu bure lisiwapumbaze wazazi tuwasimamie watoto wetu
 
Scoob102

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
269
500
Shule ya msingi ya lukooni iliyopo wilaya ya Ilala chanika Dsm imeanzisha utaratibu wa kufundisha tuition hapo shuleni kuanzia darasa la tatu mpaka darasa la Saba. Gharama ya tuition kwa kila mwanafunzi ni tsh 300 kwa Siku kwa kila mwanafunzi.

Watoto wanaokosa hela ya tuition wamekuwa wakinyanyapaliwa na hata kufikia hatua ya kutengwa madarasa na watoto wanaotoa pesa ya tuition. Pia kumekuwa na kauli ambazo kwa nanna moja au nyingine ni Kama kauli za vitisho kwa wazazi.

Mfano wa kauli hizo ni Kama ifuatayo:
Nanukuu " Kama hutaki mwanao asome tuition we acha asisome lakini kitakachompata badae usitulaumu" mwisho wa kunukuu.

Utaratibu huu una athari kubwa sana kwaani watoto wamekuwa wakitoka jioni mashuleni. MTOTO ANASHINDA NA NJAA KUTWA NZIMA AKIWA SHULENI. Kuna wakati watoto wanarudi saa kumi na mbili jioni. Hii itapelekea wanetu wapate vidonda vya tumbo kwa kushinda NJAA.

Pili wazazi wengi uwezo wao wa kifedha ni mdogo kiasi Cha kushindwa kumudu hiyo gharama ya shilingi 300 kila Siku. Pia unakua NI mzigo mkubwa zaidi kwa wale wenye mtoto zaidi ya mmoja.

Hivyo Basi tunaomba wahusika akiwepo waziri wa elimu atusaidie juu ya hili.

TUITION ZA LAZIMA MASHULENI NI MZIGO KWA WAZAZI.

Pia kwa mwenye namba ya waziri wa elimu naomba anitumia huko PM ili nimpigie kwaani nahofia anaweza asipate malalamiko yetu haya.
Mtoto anasoma bure, unashindwa muandalia mtoto mazingira ili aweze shinda mpk hiyo jion... mpe mtoto hiyo 300 na umuandalie na kaukau za kushindia acha akili za kitoto. Tabia za kulalamika lalamika hivi zilishapitwa na wakati.
 
Scoob102

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
269
500
Siku 5 kwa wiki kila siku tsh 300

5*300=1500/=

Kwa hyo mzazi mwalimu anakusaidia kumsaidia mwanao kwa buku jero kwa wiki

Niwe muwazi mm mwanangu anasoma kayumba lakn napambana kwa hali na mali ili afanikiwe nalipa tuition tsh 30000 kwa mwezi na bado mm mwenyewe nakomaaa nae kila wikend napopata nafas

Kwa Sasa anaingia darasa la tano na matokeo ya std 4 mwanangu kapata wastan wa A kapata daraja B somo moja tu la kiingereza na kapata wastan wa A peke yake darasa la watoto 120

Lengo langu nikukueleza na kukushaur hili suala la elimu bure lisiwapumbaze wazazi tuwasimamie watoto wetu
Kuna watu hata kufikiria kdg tu hawezi... yaan sh 300 kwa siku inamshinda ili mtoto wake apate matokeo mazuri kea huo muda wa ziada!!! Mueleweshen huyo raia atokekea hicho kifungo cha akili
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
13,476
2,000
Mtoa mada unatia aibu,
Sidhan Kama bado unafaa kuitwa mzazi.

Mzazi gan huwez gharamia elim ya mwanao?

Sh. 300 kwa siku ikuharibie future ya mwanao kweli?

Hebu kua serious bhana, Hawa wanasiasa wasikutoe relini.

Jiulize swali dogo TU,
-uyo anaekwambia elim bure WANAE WANASOMA WAPI?

Za kuambiwa changanya na zako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom