Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,606
- 1,956
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amesema endapo Zambia haitaondoa vikwazo visivyo vya kisheria vya kuzuia mahindi, yanayotoka nchini kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) kupita katika nchi yao, nao watawawekea vikwazo hivyo wasipitishe mizigo yao kuelekea Rwanda.
Alisema hayo jana katika mkutano, ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) wa kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa maendeleo ya viwanda. Mkutano huo ulishirikisha mawaziri kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Biashara na Viwanda na wadau mbalimbali wa kilimo. Alisema ipo changamoto kwa mahindi kutoka Tanzania kwenda soko la DRC kupitia Zambia, kwani nchi hiyo imekuwa ikiweka vikwazo visivyo vya kisheria.
Alisema kutokana na hali hiyo, amewasiliana na waziri wa viwanda na biashara wa Zambia na kumwomba watumie njia za kidiplomasia ili kuondoa vizuizi hivyo. Alisema hilo linashangaza, kwa sababu Zambia ikipeleka bidhaa zake Rwanda hupitia Tanzania, ambapo wao hawajawekewa vikwazo hivyo.
“Kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tumeiandikia serikali ya Zambia kuwa wanachokifanya sio sawa, kwani sisi na wao ni sehemu ya SADC (Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika) na tumekubaliana ndani ya SADC kuweka uwanja wa sawa soko la pamoja.
Kwa hiyo wanachokifanya hatua ya kwanza kuifanya ni kupitia majadiliano ya kidiplomasia, lakini wakiendelea kutokutoa kibali na sisi upande wetu tutazuia bidhaa zao zisipite nchini kwenda Zambia,” alisema.