Waziri wa Afya, Dr. Gwajima fuatilia yanayoendelea MOI mapema kabla mambo hayajaharibika

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Unyanyasaji wa Wafanyakazi umerudi tena Muhimbili. Mfanyakazi ukiongea kitu ambacho kinaonekana ‘kutishia’ cheo cha boss unaondolewa kwa sababu za kutunga.

Waziri tunajua una taarifa nyingi unapewa na wasaidizi wako, ila tunaomba ufike mwenyewe MOI uokoe jahazi.

Wagonjwa wanaongezeka, watu wanahamishwa na kufanya waliobaki kufanya kazi muda mrefu na kuchoka sana. Matokeo ufanisi unapungua.

Idara ya Radiology MOI kuna hujuma, tunaomba Waziri fuatilia sababu za kuwahamisha kwa Matusi na dharura Wafanyakazi wafuatao kwa wakati mmoja:

1. BAKARI MSONGAMWANJA - LINDI
2. DOTHA MBASHA - SIMIYU
3. JOSEPH KULINGA - TABORA
4. JUMA SLIM - SUMBAWANGA
5. NGINA MITTI - SINGIDA

Fuatilia walikuwa wanadai nini kwa muda gani. Ukikwama tutakusaidia, si yote yanafaa kwenda public tutazua taharuki.

Mkurugenzi na Mkuu wa Idara wanajua kila kitu. Kuwahamishia mbali haitazuia haki kutendeka na sheria kuchukua mkondo wake.

Asante.
 
Field Marshal anatengeneza ndoa yake vizuri. Ngoja amalizane napo, atakuja tu
 
Nyang’au utamjua tu
Watu wananyanyaswa we unasema mtoa taarifa ana gubu? Nyang’au lenye roho mbaya wewe
Nyang'au ni yupi kati yangu na wewe, Ok ngoja nikueleweshe maana mstari mmoja umekushinda kuelewa,,nilimjibu mtoa taarifa hii ndg Dubu,,au hujui anaitwa Dubu hapa jf?

Nikamwambia kwa hali aliyofikia,,ni muhimu achane mkeka kwa maana ya kuliweka wazi zaidi ya hapo maana imeonekana wazi ni mtu wa anayeguswa directly na jambo hilo na probably ni moja wa wafanyakazi wa MOI, usikimbilie kumtukana mtu pasipo kuelewa kwa kina alichokisema,,ungeuliza namanisha nini first.
 
Back
Top Bottom