Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,200
- 27,248
Waziri Ummy hili la Bima ya Afya Umeniangusha sana, hapa nilipo nina masikitiko makubwa sana ya maelezo unayoyatoa na kinachoendelea.
Ni wazi kabisa tumeanza kukwama kwenye hili ya bima ya afya.
Waziri umesema watu ambao sio watumishi ndio pia wamechangia mfuko kuelemewa na kuufanya udhoofike. Kimsingi kabisa kila mtu anapaswa kuwa na bima ya afya, wengi wamejiunga na NHIF sababu gharama za kujiunga na kulipia kwa mwaka ni ndogo kulinganisha na bima zingine. Vipato vya watanzania vinajulikana.
Afya ndio uti wa mgongo wa taifa lolote, ambae hana elimu Iia ana afya njema ataweza kuzalisha, Ila ambae hana vyote atawezaje kuzalisha? Taifa litakua la aina gani?
Tabia ya wengi huwa hawapendi kwenda hospitali hata kama ana bima, ukimuona mtanzania anaenda sana hospitali basi kweli huyo mtu ana shida kubwa. Hivyo hakuna ambae anafanya makusudi kwenda mara kwa mara hospital.
Sasa hivi pamoja na yote hayo bado Kuna mamia ya watu ambao kila siku huku mitandaoni wanaomba msaada wa matibabu. Na wewe waziri umekua mmoja wa watu wanaochangia na kusaidia hawa watu huku mitandaoni. Vipi bima ikienda kupunguza na kuweka masharti magumu zaidi, Hali itakuaje?
Ni hadi lini tutaendelea kuchangishana mitandaoni kuwasaidia walioshindwa gharama za matibabu??
Waziri ninakuomba tuwekeze zaidi kwenye afya, tubane mwingine. Kama kifaa flani cha mil 10 kinanunuliwa kwa mil. 50, basi tubane kuanzia hapo. Bado naamini pesa ipo ni kuweka tu mipango vizuri.
#kazi inaendelea#