Waziri Ummy Mwalimu: Hatufuti Polyclinic, tunaweka vigezo vya kusajiliwa na NHIF

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124


HATUFUTI POLYCLINIC, TUNAWEKA VIGEZO VYA KUSAJILIWA NA NHIF - WAZIRI UMMY MWALIMU

Serikali imesema haikusudii kufuta Kliniki za Kibingwa (Polyclinics) zilizopo nchini bali inapitia vigezo vya kuwa na Polyclinics ambazo hivi karibuni zimeibuka kliniki nyingi ambazo zimekuwa ni vichochoro vya udanganyifu dhidi ya Mfuko wa Taifa wa NHIF.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu leo alipokutana na Watoa Huduma za Afya wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa Mkoa wa Dar Es Salaam.

"Hatufuti wala hatukusudii kufuta Polyclinics, lakini tunafanya mapitio ya vigezo vya Polyclinics kwasababu ndio kichochoro kingine cha udanganyifu dhidi ya NHIF na ndio maana kuna wingi wa Kliniki za Kibingwa zinazoanzishwa amabzo hazina vigezo kwa sababu ya kufanya udanganyifu” amesema Waziri Ummy Mwalimu.
WhatsApp Image 2022-07-08 at 3.06.43 PM (6).jpeg
 
NHIF ni wapumbavu kiasi gani wao ni kulialia tu hadi serikali iingilie hicho kinachoitwa udanganyifu?
 
Back
Top Bottom