Waziri Ummy ataka wanafunzi wasisome masomo ya ziada wakati wa likizo

Hivi umemuelewa waziri kweli?

Ulichoongea hapa ni tofauti na maagizo yake

Kwenda tution kwa maamuzi yako na wazazi wako hakuna tatizo, ila tatizo ni pale shule zinapolazimisha wazazi kulipa pesa ili watoto wao waendelee na tution pale pale shuleni kwao kipindi Cha likizo.
Hiyo labda private, kwan hata gvt hua wanalazmsha hili?
 
Kuna sehemu huku mbeya watoto wanasoma january to january yaani hawanaga cha likizo,siku ambayo hawaji shule ni jumapili tu siku zingine ni asubuhi mpaka sa 12
 
Kuna sehemu huku mbeya watoto wanasoma january to january yaani hawanaga cha likizo,siku ambayo hawaji shule ni jumapili tu siku zingine ni asubuhi mpaka sa 12
Huku huku mbeya Kuna shule mpaka jumapili wanaenda na ni January to December na ni shule za serikali
 
kwamba na sisi kama ingekuwa kipindi kile ety tusiende soma kwa kina muddy physics , ngaiza na kina mbuga bila tution advance nisingetoboa ( pre form 5 form six ) kwa private n sawa pigen marufuku lkn sio kayumba ambazo hazina hata waalimu wa masomo flan flan aliyetoa tamko anatokea internationally
Itakuwa hujamuelewa waziri wewe?
 
Ila sumbawaga kule namanyele ndo waliniacha hoi yaani wao hata jumamosi hawataki mtoto shule wanasema anaenda kusaidia shamba likizo ndo usiwaulize
Wako sahihi kwa upande wao, serikali imeweka jumatatu Hadi ijumaa Sasa inakuwaje mtu aseme jumamosi watu waende shuleni?
 
Kuna shida hapa, likizo ni likizo ibaki hivyo kuna maisha mengine ukiacha vitabu na kukariri
Hapo ndipo watanzania tunahitaji kuelimishwa. Ukifika muda wa likizo mtoto afanye kazi za nje ya shule. Nakumbuka tukiwa shule ya msingi nilikuwa nachukia sana shule ikifunga kwasababu kulikuwa na biashara ya familia ambayo tulikuwa tunaifanya wote na kama ni muda wa kulima basi wote tulikuwa tunaenda shambani. Lakini ile biashara ndiyo ilinistili sana baada ya kumaliza chuo na kazi kutoonekana, na mpaka napata kazi nilikuwa nafanya biashara ile ile
 
Miradi ya walimu hiyo.

Wanalazimisha kabisa watoto wakae kambi shule zikifungwa.

Mzazi unachangia elfu hamsini.

Mkuu na walimu wake wanatia mfukoni maisha yanasonga.
 
Wapi RC Anthony Mtaka?

Nakumbuka alimtolea povu Ndalichako kuhusu hii issue.
 
Mimi ambaye nilisoma shule ambayo ilikua na uhaba wa walimu na vitabu siwezi kudharau tution ata siku moja.Tungekua tumetatua baadhi ya changamoto kwenye sekta ya elimu hili agizo lingekua na maana tofauti na hapo ni kujidanganya.

Nakumbuka miaka yangu nilikua naenda kupiga tution kwenye mabanda ya mabanzi pale jangwani chini ya jamaa alikua anajiita Mtata Mtatuzi.Ile tution ilinisaidia sana.
 
Aisee.
Hii naona itakuwa fulsa kwa walimu kuanzisha madarasa ya Tuition huku majumbani. Hata wale Walimu wasio na ajira hii ni fulsa kwao, si watasema wanawasimamia kufanya Home work huku wazazi wao wakiwa bize na kazi zao.
 
Bado hii kitu inayoitwa pre form one na five
Pre form one na pre form five zina tatizo gani?

Kwanza sio lazima ni maamuzi ya mzazi ampeleke mtoto wake au asimpeleke.

Alichokataa waziri ni ile tabia inayoota mizizi siku hizi shule zikifungwa mwezi wa 6 au 12 kuna baadhi ya shule za serikali na private wanawazuia wanafunzi wasipumzike inakuwa ni lazima kwenda shule kwa kigezo cha masomo ya ziada tena wazazi wanashurutishwa kuchangia pesa za hiyo program.

Hiko nafkiri ndo alichokikataza waziri.
 
Tatizo wanakaririshwa mitihani, maswali na majibu. Hawajikiti kuelewa topi husika kwa maana nakumbuka enzi zetu za wahenga, mnasoma topic, anaelewa kiasi cha kujiuliza kuwa katika topic hii swali la kunishinda litatoka angle gani. wanafunzi mnatungiana maswali na kujiridhisha kuwa topic imeeleweka, mnasubiri mitihani. Leo hii ni mwendo wa past papers!
Huu ndo usomaji ambao watoto wetu wangesoma hivi basi wasingetumia nguvu nyingi kufaulu.

Leo mtu anasoma topic alafu hajui kwamba akiulizwa nini ndo atajibu hiko anachosoma.
 
Back
Top Bottom