Waziri Tizeba: Hakuna bei nzuri ya kahawa Uganda

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa biashara ya Kahawa katika ukumbi wa Happiness Hoteli uliopo katika eneo la Mtukula Wilayani Misenyi, Leo 11 Julai 2018. (Picha zote Na Mathias Canal-WK)

Wadau wa biashara ya Kahawa wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe. dkt Charles Tizeba katika ukumbi wa Happiness Hoteli uliopo katika eneo la Mtukula Wilayani Misenyi, Leo 11 Julai 2018.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akisalimiana na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume muda mchache kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa nchi hizo mbili, mkutano uliohudhuriwa pia na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Leo 11 julai 2018.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisalimiana na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume muda mchache kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa nchi hizo mbili, mkutano uliohudhuriwa pia Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage, Leo 11 Julai 2018.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa mkutano na Waziri wa biashara na ushirika nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume (Kushoto), Mwingine ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage (Katikati).
Na Mathias Canal-WK,
Mtukula-Kagera

Imebainika kuwa bei ya uuzaji wa
Kahawa nchini Uganda haina tofauti kubwa na bei ambayo ingepatikana nchini
Tanzania endapo wakulima wangeuza Kahawa zao kwenye soko la awali jambo ambalo
linawatoa wasiwasi wakulima wa Kahawa nchini waliokuwa wakidanganywa kuwa bei
ya Uganda ni kubwa na yenye tija kwa wakulima kuliko hapa nchini.
Kilogramu moja ya Kahawa ya
maganda nchini Uganda inanunuliwa kwa shilingi 2000 ya Uganda sawa na Shilingi
1400 za Kitanzania (exchange rate 1.7) ilihali hapa nchini Tanzania bei ya
Kahawa kwa kilo moja ya maganda ni Shilingi 1460 ya bei elekezi hivyo kuwa na
tofauti ya Shilingi 60.
Hata hivyo, wakulima wa Tanzania
watapata zaidi kwa kuuza mnadani moja kwa moja na kuachana na bei ya shambani
kwa kutumia ushirika wao ambapo bei ya chini inayopatikana ni wastani wa
Shilingi 1950 kabla ya gharama za uendeshaji. Kwa kuuza mnadani mkulima anapata
bei kutokana na Ubora wa Kahawa yake na ikiwa kwenye madaraja na hivyo kutoa
motisha kwa wakulima kuzalisha Kahawa bora kuliko kuuza ikiwa ghafi.
Hayo yamebainishwa leo 11 Julai
2018 na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza na wadau wa
biashara ya Kahawa katika ukumbi wa Happiness Hoteli uliopo katika eneo la
Mtukula Wilayani Misenyi.
Dkt Tizeba amezungumza hayo
ikiwa ni muda mchache tangu alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa
Biashara na Ushirika nchini Uganda Mhe Fredrick Ngobi Gume katika mkutano
uliohudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles
Mwijage.
Mkutano huo ni muendelezo wa
utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli aliyoyatoa wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu
Jijini Dar es salaam tarehe 2 Julai 2018 na kuitaka Wizara ya Kilimo kufuatilia
kwanini wakulima wa zao la Kahawa wanacheleweshewa malipo yao sambamba na kujua
kwanini wakulima wanauza Kahawa yao nchini Uganda.
“Ndugu zangu kuna jambo
hamlifahamu wale wanaosema Uganda bei ya Kahawa ni nzuri kuliko Tanzania
wanawadanganya hakuna bei nzuri Kule kinachofanya watu kupeleka Kahawa Uganda
ni kutokana na mikopo wanayokopeshana isiyo rasmi (Butura) hivyo makubaliano ya
kurejesha mkopo yanakuwa na masharti magumu yanayowataka wakulima wa Kahawa
nchini kulipa madeni kwa kupeleka Kahawa sio fedha” Alisisitiza Dkt Tizeba
wakati akizungumza na wadau wa Kahawa eneo la Mtukula Wilayani Misenyi
Waziri wa biashara na ushirika
nchini Uganda Mhe Fredric Ngobi Gume amemuhakikishia mwenyeji wake kuwa
biashara ya Kahawa nchini humo ina changamoto sawa katika nchi zote mbili kwa kuwa
swala la mikopo isiyo rasmi inayowanyonya wakulima (Butura) nchini Uganda ipo
kwa kiwango cha juu kiasi kwamba ameomba kuja kuja nchini kwa miadi maalumu kwa
minajili ya kujifunza kuhusu namna bora kuendesha ushirika na kuanzisha mfumo
wa stakabadhi ghalani.
Aidha, Gume alisema kuwa
serikali ya Uganda inayoongozwa na Rais wa nchi hiyo Mhe Yoweri Kaguta Museveni
itaendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt
John Pombe Magufuli hivyo panapohitajika ushirikishwaji katika biashara
hususani kwenye sekta ya Kilimo watakuwa na msimamo wa pamoja.
Katika hatua nyingine pande zote
mbili kutoka Tanzania na Uganda wameeleza changamoto mbalimbali zinazoikabili
mipaka ya nchi hizo ikiwemo biashara ya magendo inayofanyika huku wakiahidi
kutokomeza kadhia hiyo.
MWISHO.
 
Sawa ila WASIPANGIWE wapi wakauze jasho lao... nyie bakini na ukweli wenu mnaoujua majukwaani
 
HUU MCHEZO HAUTAJI HASIRA, MWABIE HAWARUSU WAGANDA
 
Katika soko huria haina haja ya kuwa na sheria za monopoly, wekeni mazingira free na fair ili watu wenyewe wauze wanakotaka ambako kunawavutia kwa sababu zao wenyewe.

Kuleta hizi habari za kubumba bumba bado ni utaperi na ubabaishaji. Sioni ni kwanini wakulima kwa kutumia akili yao timilifu wakubaliane na huu utoto wa namna hii.

Kwani hawa watanzania wanapouza kwa waganda huwa wanalipwa kwa pesa ya kiganda ma ya kitanzania?
 
Sawa ila WASIPANGIWE wapi wakauze jasho lao... nyie bakini na ukweli wenu mnaoujua majukwaani
Sure. Wawaache wakulima wauze popote wanapoona pana unafuu. Kwanini wanalazimisha kudhibiti kila kitu ?
 
Back
Top Bottom