Waziri TAMISEMI ni dhaifu hana kasi ya Magufuli

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,905
4,054
Tangu awamu hii ingie tumeona mawaziri mbalimbali wakitembelea maeneo yao ya kazi kuona utendaji.

Sasa kama kuna wizara nyeti ni Tamisemi ambayo ndio inamfikia mwananchi,mtumishi, wa chini kabisa.

FACT

Naelezea kwa mfano halisi wa Wilaya Ilala. mwezi November wamewatoa kwenye payroll walimu zaidi ya mia sitini, tatizo wakisema hawana HISTORY SHEET. kwa asieelewa history sheet no Maelezo binafsi ya utumishi pamoja na vitu vingine ambavo mtumishi yoyote hujaza anapoomba kazi.

Sasa baadhi ya wafanyakazi walipeleka hizo history sheet kwa maafisa utumishi wa Ilala na kuziscan kwenda utumishi makuu. Hapo ndio zimetupwa tangu tarehe 1november hazijafanyiwa kazi na wameambiwa hata desemba hawatapa isipokuwa labda January. hii sio haki kabisa, niliipata hii habari nilisikitika sana mtu kuishi mjini bila kupewa mshahara miezi 2 kisa history sheet tu.

Huu ni uzembe kwa maafisa utumishi ilala,pia pale utumishi kivukoni ambapo fomu huenda kabla ya kupelekwa hazina.

Tunamuomba waziri husika aende manispaa ilala aulizie haya nilioyaandika ni kweli tupu.

Chanzo: Walimu wa Ilala

cc Rais Magufuli
cc Waziri TAMISEMI
cc Katibu mkuu TAMISEMI
 
watu wanafanya kazi kwa mazoea magufuli ataweza kwan ; hahangaikii mifumo anakomaa na watu
 
TAMISEMI hovyo kabisa watumishi wapya kwa sasa hawapewi pesa za kujikimu wao wamejifungia maofisini
 
Naunga mkono hoja yule Simbachanani sijui ni hovyo kabisa
Ila Magu nae mnafiki kwenye kampeni alisema waziri mwenye dhamana wa nishati
akiingia tu ikulu tarehe 25 atamuwajibisha, sasa kampa hiyo TAMISEMI
 
Wabongo bwana Mtu kateuliwa juzi tu leo makelele mengi alafu malalamiko yenyewe ni ya ndani ya Halmashauri ambayo sio rahisi waziri kujua bila kupewa malalamiko kwa hata akitembelea hapo ilala Ofisini hawezi kujua hilo tatizo kama hakuwakuta walalamikaji wakamueleza. Mbona waziri huyo anaonekana kwenye maeneo mbalimbali mara nyingi tu na juzi alikuwa na waziri mkuu kwenye ukaguzi wa mradi wa DART.

TAMISEMI ni wizara kubwa sana hivyo waziri wake ni sawa tu Waziri Mkuu maana TAMISEMI inafanya majukumu Wizara nyingi sana kwa wakati mmoja kwa hiyo usipomuona kwenye Halmashauri yako basi ujue yupo maeneo mengine
 
unafiki at its peak
 
TAMISEMI inafanya kazi kama jeshi la sungu sungu,sheria zinawa favor wakubwa tu!Zinatumika sheria za pori ambapo mwenye nguvu anaweza tu kumla asiye na nguvu!
 
acha kutetea ujinga kama waziri anakosa intelijensia ya kujua mambo madogo
 
TAMISEMI inafanya kazi kama jeshi la sungu sungu,sheria zinawa favor wakubwa tu!Zinatumika sheria za pori ambapo mwenye nguvu anaweza tu kumla asiye na nguvu!

nakuunga mkono mkono mkuu hii serikali ya kibwege sana
 
Back
Top Bottom