Waziri SMZ Atoa Mpya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri SMZ Atoa Mpya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Oct 11, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  SLIM SAID SALIM,

  KWA mara nyingine tena, kama ilivyotokea wakati wa kuelekea chaguzi zilizopita za mfumo wa vyama vingi vya siasa Zanzibar, zinasikika kelele, kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, za kuwataka wanafunzi wasijihusishe na mambo ya uchaguzi.

  Hiki ni kichekesho ambacho hakina tofauti na zile hadithi za Esopo, mazimwi na za Abu Nuwasi, kwa vile ni tafsiri potofu ya hali halisi.
  Huku ndiko tunakoita kuisaliti katiba ya nchi ambayo inasema wazi kuwa mtu anayefikisha umri wa miaka 18, mwenye akili timamu, anastahili kupiga kura na hakuna kipengele katika katiba kinachomzuwia mwanafunzi aliyetimiza umri huo kuwa mpiga kura.
  Sasa mtu hubaki anajiuliza wapi Waziri wa Elimu na Kazi za Amali, Haroun Ali Suleiman, anapata haki na ujabari wa kuwataka wanafunzi wa Visiwani waachane na masuala ya uchaguzi?

  Niliamini Waziri angekuwa mstari wa mbele kuwashajiisha wanafunzi katika shule za serikali na binafsi waliotimiza miaka 18 kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili wapige kura katika uchaguzi ujao na sio kuwataka wakae mbali na uchaguzi.

  Waziri aelewe kuwa neno mwanafunzi ni pana sana kwa vile linajumuisha watu wote wanaojifunza jambo, kitu au fani fulani. Wapo wanafunzi wenye miaka 60 na zaidi na je hawa nao waziri anawataka wakae mbali na uchaguzi wa mwaka 2010?

  Inasikitisha kuona kila ukifika wakati wa uchaguzi utaona wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo wa Zanzibar, hasa wenye asili ya Pemba, wanasumbuliwa na hata kufukuzwa shule kwa kosa la kudai haki ya kupiga kura. Huu ni uonevu mkubwa na dhuruma na inafaa kulaaniwa.
  Katika uchaguzi wa mwaka 1995, zaidi ya wanafunzi 300 wa kidato cha tano na sita walifukuzwa kitendo kilichofanya washindwe kufanya mitihani.
  Hata mahakama iliposema wanafunzi hao walikuwa na haki ya kudai kuandikishwa kuwa wapiga kura Tume ya Uchaguzi iliwanyima haki yao. Ni uhuni na sio jambo jengine.

  Baadhi ya hawa wanafunzi baada ya kuhangaika sana na kutofanikiwa kurudishwa shule, wakati Waziri Haroun akiwa mkurugenzi katika Wizara ya Elimu, walikwenda nchi za Ulaya kama wakimbizi na wengine walisaidiwa na wahisani wa ndani na taasisi za kimataifa kuendelea na masomo nje ya nchi.

  Wengi wao sasa wamebakia huko na wanasoma katika vyuo vikuu na kufanya kazi za kitaalamu kama za madaktari, walimu na wahandisi.
  Vijana wengine ambao hawakubahatika kuendelea na masomo waliharibikiwa na maisha na hatimaye kuwa madereva wa magari yanayotembeza watalii na daladala na wengine wakigeuka wauza nazi na mbaazi.

  Kwa kweli vijana wale walidhurumiwa na historia hata siku moja haitasawasamehe waliochochea na walioshiriki kuwafukuza shule. Waziri Haroun anaelewa vizuri jambo hili na ingekuwa vyema kama angelitoa maelezo.

  Katika mkumbo ule Wizara ya Elimu, ambayo siku zote imekuwa ikisemekana kuongozwa zaidi na utashi wa kisiasa na sio elimu, ilifukuza zaidi ya walimu 400, wengi wao siku hizi wanafundisha shule binafsi za Unguja na Pemba na wengine Tanga, Dar es Salaam na Mombasa.
  Athari za SMZ kufukuza kundi kubwa la walimu wakati ule zinaonekana mpaka leo katika shule za serikali Visiwani hapa.

  Sijui kwa nini Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekuwa ikipenda kuwatenga wanafunzi na uchaguzi wakati wanafunzi , kama wana jamii, wanayo haki ya kushiriki katika kuchagua viongozi wa nchi na kutumia kiwango cha elimu kinachotolewa katika shule zetu za serikali kama kigezo cha kuendelea kuiweka madarakani serikali iliopo au kutafuta viongozi wengine.

  Lakini baya zaidi na linalozusha masuala mengi ni huu wito wa kuwataka wanafunzi wasijiandikishe kupiga kura unaonekana kutiliwa nguvu zaidi kisiwani Pemba.

  Bado sijamsikia na nina shauku kubwa kumsikia Waziri Haroun akitoa kauli kama hiyo ya kuwataka wanafunzi wasijihusishe na uchaguzi akiwa katika jimbo lake la Makunduchi au maeneo mengine ya Unguja.
  Unabaki kujiuliza kwa nini onyo hili liwe zuri kwa wanafuzi wa Pemba pekee yao? Au ni hofu tu ya kuwa Pemba ni ngome ya Chama cha (CUF) na kwa hivyo na wanafunzi wa Pemba nao pia wataipigia kura CUF?

  Ni vizuri kwa Wizara ya Elimu na Kazi za Amali ya Zanzibar ikaachana na kauli hizi za kuwabagua, kuwanyanyasa na kuwadhulumu wanafunzi na badala yake iwahimize wanafunzi kuwa mstari wa mbele kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi inaoqaona wanafaa kuwatumikia.

  Hizi ni zama za watu kuruhusiwa bila ya vikwazo kutumia haki zao na sio za kuwapa amri za kiimla, miongozo isiokuwa na maana au vitisho. Nimeambiwa hata katika shule zetu siku hizi somo la imla halitiliwi maanani.

  Nasi tubadilike katika maisha na kuachana na kuongoza watu kiimla. Tunasema Watanzania ni watu huru basi tuwaachie watumie uhuru wao kama ilivyoainishwa ndani ya katiba bila ya kuwawekea vikwazo vya aina yoyote ile.

  Ni matumaini yangu wanafunzi wa Zanzibar hawatakubali kuona haki zao zinapotea au kudanganyika na kauli za kutaka wakae mbali na shughuli za uchaguzi.

  Ni muhimu kuhakikisha hawashiriki katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha yao au kuvuruga amani. Vile vile wanapaswa kuwa na hadhari ya kutokuwa mashabiki wa kisiasa na kuathiri masomo yao. Wakati umefika kwa SMZ kuelewa wanafunzi wa Visiwani ni sehemu ya umma wa Tanzania na wanayo haki sawa na raia wengine. Tubadilike na tuache kuwakaba koo wanafunzi.

  Kinachoelezwa eti kitendo cha wanafunzi cha kujitokeza kutaka kuandikishwa kuwa wapiga kura ni kujiingiza katika utashi wa kisiasa ambao hauna manufaa kwao na kwamba hali hii inaweza kuathiri masomo yao.

  source:
  Tanzania Daima.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tokea Haroun Ali Suleiman awe waziri wa elimu zanzibar, mm sijaona lolote la maana alilofanya au jipya alilokuja nalo, zaidi ya kufianya wizara ya elimu na taasisi zake kuwa hifadhi ya Wamakunduchi wenzake, baas.
  Nashangaa, kuboronga na kushuka kwa kasi ya kutisha kwa kiwango cha kufaulu wanafunzi zanzibar kimekuwa kikubwa katika wakati wake kuliko wakati wote, bado waziri Haroun hataki kushindwa au kukiri kuwa wizara imemshinda. Mara ya mwisho wizara ya elimu zanzibar kufanya kazi kama wizara yenye dhamana ya mambo ya kitaaluma, ni wakati wa Maalim Seif Shariff Hamad, alipo kuwa waziri wake na alipokuwa waziri kiongozi, hakuna tena zile zama sasa unakwenda Taasisi ya kiswahili na lugha za kigeni, unakuta magwiji wa lugha zote wapo pale, ni katika enzi hizo watu kama Dr. Abdallah Kanduru, Dr. Idrissah(nimesikia yupo kwa Bill Gates sasaivi) walipatikana kwa tasnia tofauti,kuanzia sanaa mpaka sayansi, vipo wapi vichwa kama vya akina Mwalimu Njeketu...hakuna ...saivi siasa tu, wizara imejaa majungu, fitina, ubaguzi wa kieneo..mara katibu hapatani na waziri tutafika wapi?
  Haroun, badala ya ku-focus kwenye mambo ya maana ya wizara...anashughulika na habari za wanafunzi na siasa. Huku ndo kushindwa kazi au vp sijuwi...
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wakati wenzetu wanahimiza wanafunzi wawe na muamko wa kisiasa kwa kupiga kura, sisi tunawa condescend in this horrible way!
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio serikali iliyowekwa na baadhi ya WaTanganyika inavyotakiwa ifanye la si hivyo hawana kazi.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Junius,\
  Mkuu ningependa kusoma nukuu ya maelezo ya waziri mwenyewe kwani yawezekana hakuwa na maana iloandikwa hapa..
  Kwa mana kwamba yawezekana wanafunzi wengi sasa hivi wanatumiwa na vyama kupiga kampeni za kisiasa badala ya kuwa masomoni malalamiko ambalo yeye kama waziri kayapokea toka kwa walimu. Huu ni mfano tu hivyo ni vizuri tuipate hotuba nzima ya waziri huyu kuliko kudandia katikati pasipo kuelewa haswa sababu ilotokana na maneno hayo.
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu waziri historia yake ya elimu ikoje na ya kisiasa pia ikoje?
   
Loading...