Waziri Sitta: Dowans ni genge la ulaji wa vigogo watatu; tusiwalipe!

Samwel sitta anajua mengi,hili la dowans ni moja kati ya mengi,tumpe nafasi na kuendelea kumchokonoa zaidi ili ayatoe yote moyoni,kauli yake juu ya kuilipa downs ni kuhujumu uchumi inabeba ujumbe mzito nyuma yake.
Nadhani utafika muda na tutajua tu tena kwa uwazi zaidi na si kwa tetesi kama ilivyo kwa sasa juu ya nani haswa wanaowaumiza watanzania kwa mambo kama hayo ya dowans.
Tupo vitani,hakuna kunyamaza kimya hadi kieleweke,pamoja tutashinda tu,kwani tumeshaambiwa kuwa wanaofaidika na dowans ni watu wakuu watatu na ni mpango wao wa maandalizi ya urais wa 2015
watashindwa na mpango wao mzima wa kishetani wa kuwalaza watanzania gizani ili wapate pesa za uchaguzi wa 2015,lowasa,chenga na rostam watanzania si mabwege tena
 

Dowans ndiyo ilirithi mkataba wa Richmond na kwa mujibu wa Sitta, njama za kuileta kampuni hiyo zilisukwa na vigogo watatu ambao ni wabunge wa muda mrefu na wamekuwa wanahusishwa na matukio mbalimbali ya ufisadi, na mmojawao ni mwanasheria maarufu aliyebobea katika masuala ya mikataba ya kimataifa. Kwa sababu za kitaaluma, gazeti hili litahifadhi majina yao kwa sasa.


Doh! Huna hata haja ya kuuliza ni nani????

Get your bucket of salted POPCORN 2015 Movie has just started!!!

Topic za mafumbo hazihitajiki jamvini. Wewe kama unamjua sio utuambie ? Hata mm najua nyuma ya Richmund ni vigogo watupu japo siju majina yao.
 
Sitta anasema imefika wakati sasa genge hili linalohujumu uchumi lishughulikiwe na serikali, tatizo ni kuwa serikali yenyewe imewekwa na hili genge, na kama tulivyoshuhudia kwenye uspika, genge hili linao uwezo wa kuiondoa serikali hii litakapoiona ni tishio kwake. Hata hivyo nampongeza Sitta kwa ujasiri wa kusema aliyosema. Namshauri kwenye vikao vyao vya Cabinet uwajibikaji wa pamoja kisiwe kikwazo kwake. Atakapoona maslahi ya taifa yanawekwa kando kwenye vikao vya huko awe tayari kuuacha uwaziri.
 
Ameyataja lakini hayakuandikwa na gazeti kwa sababu zao za kimaadili. Kama huwajui ni Rostam Aziz, Edward Lowasa wa Monduli na Nimrod Mkono, no! Andrew Chenge!!
 
Atakuwa Mzee kitarabushi, mwenye BANK M?

oh! asante. lakini yule nacho mpendea ame invest saana kwenye Ilimu/shule kwa watu wa kwao na nduguze na alianza zamani kabla ya huu ufisudi anao fanya sasa.
sasa sijui uwekeza wa Richie Richie, Rowans kwenye Elimu hususana ya Upili kwa majengo na kusomesha watu. upoje.
 
Kama sisi wanaJF tunaogopa kuwataja wakati tunatumia majina bandia, itakuwaje kwa serikali yetu iliyowekwa mfukoni na watu maarufu. Kama kuna mtu anawafahamu jamani, tufumbueni macho wengine hatujui ni nani hao haswaaa!
 
sitta na wazee wengine hakuna sababu za kuulea uovu kwani taifa halitawakumbuka kwa kulea uovu,kemeeni hadi mpasuke
 
oh! asante. lakini yule nacho mpendea ame invest saana kwenye Ilimu/shule kwa watu wa kwao na nduguze na alianza zamani kabla ya huu ufisudi anao fanya sasa.
sasa sijui uwekeza wa Richie Richie, Rowans kwenye Elimu hususana ya Upili kwa majengo na kusomesha watu. upoje.

Mafisadi wote ndivyo walivyo. Wakishatuibia wanaturudishia kwa njia hizo za misaada isiyo endelevu kwa malengo maalum. Malengo yao yanapotimia hautawaona tena na miradi hii wanayoifadhili hufa haraka kama ilivyoanza.
 
Back
Top Bottom