Waziri Sitta: Dowans ni genge la ulaji wa vigogo watatu; tusiwalipe!

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
42,837
2,000
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ametishwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), iliyoipa ushindi Kampuni ya Dowans dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), lakini akasema haya ni matokeo ya genge la watu wachache wanaofahamika ambao wameamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma.

Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano katika miaka mitano iliyopita na ambaye aliruhusu Bunge kujadili masuala kashaa ya kifisadi, alisema hayo jana katika mazungumzo maalumu na Tanzania Daima kwa simu kutoka Kampala Uganda.

Alisema vigogo hao waliileta Dowans makusudi baada ya kampuni ya awali iliyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development LLC, kushindwa kutimiza malengo.

Dowans ndiyo ilirithi mkataba wa Richmond na kwa mujibu wa Sitta, njama za kuileta kampuni hiyo zilisukwa na vigogo watatu ambao ni wabunge wa muda mrefu na wamekuwa wanahusishwa na matukio mbalimbali ya ufisadi, na mmojawao ni mwanasheria maarufu aliyebobea katika masuala ya mikataba ya kimataifa. Kwa sababu za kitaaluma, gazeti hili litahifadhi majina yao kwa sasa.

Kwa mujibu wa Waziri Sitta, hili ni genge ambalo limeamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma, na bila kujali maslahi ya vizazi vijavyo.

"Nakwambia hakuna jambo ambalo linakera kama kuona genge la watu wachache limeamua kutafuna rasilimali za taifa hili bila huruma. Wameshindwa kufikiria kizazi kijacho kitanufaika vipi.

"Hii inaletea hisia kuwa kundi hili linaendesha hujuma nzito dhidi ya mali za taifa hili… haiwezekani hata kidogo kununua jenereta halafu unasema huu ni uwekezaji… huu si uwekezaji," alisema Sitta.

Alisema hukumu iliyotolewa dhidi ya TANESCO ni mwendelezo wa hujuma kubwa dhidi ya taifa kwa vile inaonekana wazi kwamba kuna kundi la watu maarufu ambalo ndilo chanzo cha suala hilo, na ambalo kwa namna moja au nyingine lilishiriki kuhujumu mwenendo wa kesi ili serikali ishindwe, wao walipwe pesa.

Alisema Dowans ni mali ya wachache hao ambao wameamua kufumba macho ili kufanikisha malengo yao kibiashara, na kwamba umefika wakati serikali iamue kwa nguvu zote kuwashughulikia bila huruma kwa vile ni sawa na wahujumu uchumi.

"Sisi tulioko serikalini lazima tukomeshe hali hii… kwani mchezo huu umekuwa ukijirudiarudia mara kwa mara. Lazima tujipange vizuri ili kuhakikisha nchi haichezewi tena.

"Serikali iko kwa ajili ya watu. Sasa iweje tushindwe kujipanga vizuri, tunataka kuona wananchi wetu wananufaika na rasilimali zilizopo, na hiyo ndiyo sifa (yetu) kwa taifa," alisema Sitta.

Alisema hata hukumu hiyo ni matokeo ya watu fulani ambao walitaka kesi hiyo isikilizwe nje ya nchi kisha wagawane fungu la fedha zitakazopatikana.

"Inashangaza mno kuona kuna watu fulani wamekuwa wakipendekeza kesi hizi zisikilizwe nje ya nchi… lazima tujiulize, wanavuna nini? Hata hii inawezekana wazi ulikuwa mpango wao wa kuhakikisha wanapokamilisha mambo yao wanagawana wanachovuna.

"Wamesababisha mahakama zetu zinyang'anywe uwezo wa kusikiliza kesi hizi... wanawapelekea Wazungu… hii haijakaa sawa hata kidogo," alisititiza.

Kauli ya Sitta ni ushahidi mwingine wa vita ya makundi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ambayo imeibuliwa upya na sakata la Dowans.

Sitta anatoa kauli kali hii siku moja baada ya mwanasheria mkongwe anayeheshimika nchini, Jaji Mark Bomani, kuzungumza na gazeti hili juzi akisema ushindi kampuni ya Dowans dhidi ya TANESCO ni matokeo ya namna taifa lilivyoshindwa kushughulikia vema mikataba mikubwa ya kimataifa katika uwekezaji na nishati.

Alisema: "Sakata la TANESCO na Dowans linasikitisha. Nafikiri liliendeshwa kwa namna ambayo ingewafikisha wahusika pabaya kama ilivyotokea.

"Fundisho ni kwamba unaposhughulikia masuala yanayogusa mikataba ya kimataifa kama haya yanayohusu nishati, madini na mengineyo, umakini mkubwa unatakiwa," alisema Bomani.

Mjadala wa mitambo ya Dowans, uliwahi kuligawa taifa kwa kipindi kirefu mwaka 2008 baada ya Kamati Teule ya Bunge chini ya Uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe baada ya kutoa taarifa ya kuchunguza uhalali wa kampuni ya Richmond na mtakaba kati yake na serikali.

Kutokana na taarifa iliyowasilishwa bungeni Februari mwaka 2008 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alijiuzulu ikiwa ni ishara ya kuwajibika kama kiongozi mkuu wa ofisi yake iliyodaiwa kushiriki katika kuiwezesha Richmond kushinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.

Hali ilipokuwa tete, aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, aliishauri serikali kuinunua mitambo hiyo, lakini baadhi ya wanasiasa walilisukuma Bunge kukataa kununua mitambo hiyo kwa maelezo kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 inakataza serikali au taasisi zake kununua mitumba.

Wengine walikwenda mbali zaidi wakisema ununuzi wa mitambo hiyo utaifaidisha Dowans ambaye ni dada yake Richmond.

Katika uamuzi wa ICC uliotolewa na jopo la majaji watatu chini ya uenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, TANESCO imeamriwa kuilipa Dowans fidia ya zaidi ya sh bilioni 36 na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 tangu Juni 15 mwaka huu, hadi fidia hiyo itakapolipwa.

Kadhalika, jopo hilo liliamuru malipo ya sh bilioni 60 na riba ya asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.

Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi wa ICC na utawala ni sh bilioni moja zinazotakiwa kulipwa na pande zote.


Chanzo: Tanzania Daima
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,104
2,000
Nani anasema makundi ndani ya CCM yamekwisha? bado yanafukuta. Ingawa SS ameficha majina tunawajua wahusika wakuu wa sakata hili ni.........Lowassa, Rostam na...................
Nafikiri SS ataweza akatusaidia sana kuhusu sakata hili maana kwa kiasi kikubwa ndilo lililochangia kuukosa uspika na anaujua undani wake.
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,104
2,000
"Nakwambia hakuna jambo ambalo linakera kama kuona genge la watu wachache limeamua kutafuna rasilimali za taifa hili bila huruma. Wameshindwa kufikiria kizazi kijacho kitanufaika vipi.

"Hii inaletea hisia kuwa kundi hili linaendesha hujuma nzito dhidi ya mali za taifa hili… haiwezekani hata kidogo kununua jenereta halafu unasema huu ni uwekezaji… huu si uwekezaji," alisema Sitta.

"Inashangaza mno kuona kuna watu fulani wamekuwa wakipendekeza kesi hizi zisikilizwe nje ya nchi… lazima tujiulize, wanavuna nini? Hata hii inawezekana wazi ulikuwa mpango wao wa kuhakikisha wanapokamilisha mambo yao wanagawana wanachovuna.
"Wamesababisha mahakama zetu zinyang'anywe uwezo wa kusikiliza kesi hizi... wanawapelekea Wazungu… hii haijakaa sawa hata kidogo," alisititiza.
 

King kingo

JF-Expert Member
Sep 6, 2010
401
195
Duh huyu mheshimiwa sita nae si alikuwa na uwezo wa kuwamaliza hawa alivyokuwa spika???? mbona aliizima richmondi kiaina bungeni? na sasa analalamika
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
KWA HAWA MAFISADI WA DOWANS NA WAFADHILI WAO 'MWENDO WA KUWANYATIA MMOJA BAADA YA MWINGINE, FAMILIA ZAO PAMOJA NA MALI ZAO NDIO JIBU KWETU VIJANA TANGU SASA:

Wenye magendo na nia ya dhati kuendelea kuhujumu uchumi na KUTAFUNA RASILMALI YA TAIFA BILA HURUMA, nadhani siku si nyingi sana Wa-Tanzania tutalazimika kidogo kuweka AMANI yetu kabatini na UTAWALA WA KIJANJA WA SHERIA na kuzipitia baadaye kidogo ili vijana kwanza tukamalizane kiaina na nyie. Hapo adabu itakwepo.

Ndio, nadhani njia pekee tuliobaki nayo ni hii hapa. Hakika, itabidi na familia zenu popote pale walipo nao kama hawaoni kwamba mnafanya KUFURU vitendo vyenu vinatuelekeza kuchukua hatua za makusudi kabisa ili sasa tuanze tu na nyinyi pamoja na familia zenu popote pale mlipo - KWA MWENDO WA KUWANYATIENI BILA YA KELELE ZOZOTE ZA MWIZI MWIZI - halafu matamu yake yatakua fundisho tosha kwa wengine wengi wa aina yenu.

Nyinyi si ni wajanja, na wanasheria wote mnao, taasisi zote muhimu tayari mmezinunua ndani na nje ya nchi sio??????????? Sawa basi!!! Huu ujinga tutaufumbia macho hadi lini. Ole wake mtu atumie sehemu ya KODI YANGU kuwalipeni ninyi MASHETANI WAKUBWA!!!!!!!!!!

Nao wanafamilia zenu wamekataa katakata kuwashaurini kutufanyia taifa letu huu UBAKAJI WA KUTISHA WA AINA HII, OK!!!!!!!!!! Hivi kwanza wanachi mnaowakilishwa na watu kama hawa mnajisikieje????
 

mtemiwao

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
384
0
Kwa mtanzania yoyote halisi anayelipa kodi(anayewalisha vigogo)atakubaliana nami ni wakati wa kuchukua hatua,tushikamane dhidi yao
 

tunalazimika

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,099
1,195
too much talking watz, hapa ni watu hao kufahamika bila kusema majina tunayahifadh kwa upumbafu fulan fulan _yawekwe waz halafu tuwafanyie mbaya mafara hawa
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,584
2,000
Gazeti la Mwananchi la leo linamripoti Waziri wa Afrika ya Mashariki Samweli Sitta akiendeleza ahadi zake za kupambana na ufisadi kwa kusema ...."Serikali isiilipe Dowans".......................Na ya kuwa pesa hizi ni mikakati ya kusaka fedha za kampeni za uchaguzi wa 2015................

Habari hii imejirudia tena kwenye magazeti ya Nipashe lenye kichwa cha habari.................."Sitta kuilipa Dowans ni kuhujumu uchumi"

Vile vile gazeti la the Citizen linayo hiyo habari.............


Sitta: Kuilipa Downs ni kuhujumu uchumi


Wednesday, 08 December 2010 08:13
SEMA HIZO NI NJAMA ZA GENGE LINALOTAFUTA FEDHA ZA UCHAGUZI MKUU 2015
Na Mwandishi Wetu
sittaspika.jpg

WAZIRI mpya wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, amesema hatua yoyote ya kulipa fidia ya Sh 185 bilioni kwa kampuni ya Dowans, ni kuhujumu uchumi wa nchi.

Sitta, ambaye aliongoza Bunge la Tisa lililotikisa nchi kwa kuibua kashfa za ufisadi, pia amesema kuna kila dalili za genge linalohujumu nchi kuandaa mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

Sitta alikuwa akitoa maoni yake baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuhishi wa Kibiashara (ICC) iliyolitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kuilipa Dowans Sh185 bilioni kutokana na kuvunja mkataba bila ya kufuata taratibu.

Tanesco ilivunja mkataba huo wa kuzalisha umeme mwaka 2008, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya kuisha, ikieleza kuwa mkataba huo ulikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma. Tanesco imesema itazungumzia suala hilo baada ya hukumu hiyo kusajiliwa nchini.

Hukumu hiyo imeamsha mjadala mkubwa uliokuwa umepoa kuhusu kampuni ya Dowans ambayo ilirithi mkataba uliobainika kuwa wa kifisadi wa Richmond Development LLC ambayo ilitakiwa izalishe umeme wa dharura wakati kulipotokea tatizo kubwa la umeme mwaka 2006.
Jana Sitta alizidi kuukoleza mjadala huo aliposema: "Kuna kila dalili ya genge la watu wenye fedha chafu kujaribu kuandaa mpango wa kuihujumu nchi."
"Hakuna uhalali wowote wa kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha, si haki hata kidogo.
"Kuilipa Dowans Sh185 bilioni ni kuhujumu uchumi wa nchi, na kuna kila dalili ni genge lilelile ambalo sasa linatafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015."
Sitta, ambaye aliweka bayana dhamira yake ya kuendelea kupambana na ufisadi mara baada ya kuapishwa kuwa waziri, aliendelea kusema: "Ni genge ambalo halina huruma na nchi na umasikini wa Watanzania... na kama likiachwa lijiimarishe, Watanzania wasubiri matatizo makubwa zaidi huko mbele.
"Genge hili limekuwa likiwafanya Watanzania kuwa ni wajinga wasioweza kufikiri. Ni kwa sababu limeshika nchi, linafikiri siku zote litafanya mambo ya hovyo na kuangaliwa... sijui linawatafuta nini Watanzania wazalendo?"
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye wakati akiwa spika Bunge lilijadili kwa kina kashfa ya Richmond iliyokuwa na matokeo ya kihistoria baada ya Edward Lowassa kulazimika kuachia uwaziri mkuu na kufuatiwa na mawaziri wengine wawili, alisema kinachofanyika sasa ni genge hilo kujiandalia mazingira ya kujikusanyia mabilioni ya fedha chafu za uchaguzi wa 2015.
Pamoja na Tanesco kuvunja mkataba na Dowans mwaka 2008, shirika hilo la umma liliibuka na mapendekezo ya kununua genereta za kampuni hiyo zinazoendeshwa kwa gesi, mapendekezo ambayo Bunge la Sitta liliyakataa kwa maelezo kuwa yanakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Msimamo huo wa Bunge ulimfanya mkurugenzi wa zamani wa Tanesco, Dk Idris Rashid kukubali kwa shingo upande akilaumu wanasiasa kwa kukwamisha masuala ya kitaalamu na kunawa mikono kwamba asilaumiwe kwa matatizo ya baadaye ya umeme.
Wakati nchi ikiwa imeingia kwenye tatizo jingine kubwa la umeme linalokaribiana na la mwaka 2006, ICC ilitoa hukumu ambayo imeamsha mjadala huo na Sitta alisema jana kuwa Tanesco isilaumiwe kwa uamuzi huo akielekeza lawama zake kwa genge hilo ambalo hakutaja walio ndani.
"Nitashiriki kikamilifu kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa na hakuna mianya yoyote ambayo genge hili inaweza kuitumia kuhujumu nchi," alisema Sitta, ambaye ni mmoja wa wanasiasa wazoefu walio kwenye baraza jipya la mawaziri.

"Hili nataka uninukuu vizuri, kwamba sasa ni dhahiri kuna mkono wa ambao kila dalili unaonyesha ni genge linalotaka kufanya hujuma. Linachotaka kufanya ni mchezo mchafu ambao sisi serikalini tutajitahidi kuuzuia."
Alifafanua kwamba watu hawapaswi kuitwisha mzigo Tanesco kwani uamuzi uliangal;ia kwa kina maslahi ya taifa kuliko baadhi wanavyojaribu kupotosha.

Sitta alisema huu ni wakati wa kuhakikisha genge hilo halifanyi hujuma zake kwa nchi.
Sitta pia alidai kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini wamekuwa wakikwepa kufungua kesi zao kwenye mahakama za ndani kwa hofu ya kuumbuka.
Dowans ilifungua kesi hiyo kwenye mahakama hiyo ya ICC ambayo makao yake makuu yako Paris, Ufaransa.
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,522
2,000
Nakubaliana kabisa na Sitta. Waache mafisadi wavune walichopanda, siyo kutumia migongo yetu.
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Afadhali mafisadi wa DOWANS pamoja na familia zao wanaotuhujumu wakaongee sasa hivi hkuhusu hujuma zao kwa taifa letu au wasije wakaongea kabisa hapo baadaye!!!

Nafasi ya toba ni sasa au haitokwepo kabisa hapo baadaye kwao, sasa basi tena!!!
 

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,523
2,000
Ni suala la kisheria na implications za kutolipa wanasheria wanaweza kutueleza zaidi!
 

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
2,000
hapo ndo sitta unakuwa mwanaume wa shoka, hata nyerere aliwahi kumwambia mkapa usilipe madeni ya wazungu na mpaka leo hawalipwa, nashangaa hao mediator waliokaa london kuwataka watanzania wanaoishi chini ya dola moja kwa siku kutaka tuwalipe majambazi wetu 185bilioni!!!!!!!!
 

chobu

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
309
225
jamani ukweli ni kwamba RICHMOND bado inatutafuna!!!!!!!!fungueni macho watanzania!!!!!!!!!!!!!!!tumechoka hatutaki tena kunyonywa!!!!!!!!!!!:nono::nono::nono::nono::nono::nono:
 

Questt

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
3,010
1,195
Huyu muungwana anapaswa kuungwa mkono.......Its true, katika hii nchi kuna watu wana fedha zaidi ya Budget ya Serikali. Swali, Wamezitoa wapi??? kwa njia zipi??? why wao??? na Kwa nini wawe wachache????
 

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
250
Hapa nimefurahishwa sana na kauli hii, kwani imedhihirisha kuwa waananchi ni wengi lakini Watanzania ni wachache kama SS, JKN, na humu tunaye MMKJ,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom