Waziri Sitta: Dowans ni genge la ulaji wa vigogo watatu; tusiwalipe!

Si atake hayo majina sasa anasema vigogo watatu halafu hawataji majina maana yake nini au ndio unakuwa unamhisi mtu fulani bila kuwa na evidence
 
too much talking watz, hapa ni watu hao kufahamika bila kusema majina tunayahifadh kwa upumbafu fulan fulan _yawekwe waz halafu tuwafanyie mbaya mafara hawa

WAMETAJWA SANA, NIMEWACHOKA! Andrew Chenge, Rostam Aziz [huy c mtanzania, msomali haramia], na Edward Lowasa!
Mtu mwenye documents za serikali wekeni. TUIFANYE JF KAMA WIKILEAKS YA WATANZANIA. Hapo tutafanikiwa kuijenga nchi ye2.
 
Sasa hivi kuna watu humu JF wataanza kumshambulia Sitta! Vita ya ufisadi ni ngumu sana jamani!!!!
 
1. Shilingi Ngapi serekali iliipa Richmond kwa ajili ya kununulia mitambo? Je pesa zile zilikuwa mkopo au? na kama haukuwa mkopo kwa nini mitambo imilikiwe na Richmond?

2. Megawat kiasi gani Richmond walizalisha kulingana na mkataba? kama hawakuzalisha umeme wakati tunahitaji faini kiasi gani walitulipa kama adhabu yao ya kulitia taifa hasara kiuchumi na kusumbua wananchi kukaa kwenye giza?

3. Shilingi ngapi Richmond walilipwa kama gharama za administration kila siku wakati walikuwa hawazalishi umeme? kwa ujumla wake?

4. Shilingi ngapi walipaswa kulipa kama kodi? (VAT) ambazo zilipelekea mitambo kukamatwa na leo tunatakiwa kuwalipa wao?

5. Pesa yote ikiwekwa kwa pamoja je inaweza kununua mitambo ya kuzalisha umeme kwa gesi wa megawati ngapi? je tunaweza kuchimba mabwawa mangapi huko Rufiji kwa ajili ya kuzalisha umeme? je inatosha kununua mtambo wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe wenye kuzalisha megawati ngapi?

Je wanajamvini hamdhani kuwa kesi yenyewe ya Richmond kuishitaki serekali ilikuwa ya ujanjaujanja tuu, ie, mitambo haiuziki popote duniani kwa kuwa tayari ina kashfa na wakubwa wenye mitambo ile ambao ni watanzania wenzetu wakaamua kuchonga dili na wizara ya Ngeleja na ile ya sheria kwa kuvunja vipengele makusudi kisha kuanzisha kesi halafu wanasheria wetu wanaelekezwa namna ya kuhakikisha serekali inashindwa ili pesa ilipwe kwa kisingizio cha sheria?
 
Na sitoshangaa kama hii ishu ya dowans kuwa ni mkakati wa kusaka fedha za kampeni za uchaguzi 2015
 
Si atake hayo majina sasa anasema vigogo watatu halafu hawataji majina maana yake nini au ndio unakuwa unamhisi mtu fulani bila kuwa na evidence

Sita ametaja majina ila Gazeti limeficha na kwa kuanza kudadavua mmoja aliyekuwa akipokea malipo ya Richmond ambayo baadaye ilikuwa Dowans ni;
1. Rostam Aziz
2. Andrew Chenge
3. Edward Lowasa
Hao tuchukue hatua sasa.
 
BIGUP MWANANGU!!!!!!!!:kiss::kiss::kiss:; UMEFIKIRIA KITU CHA MAANA SANA. KWA UTARATIBU HUU TUTAWEZA KUPAMBANA NA MAFISADI. LOWASA NA WENZAKE NI WAJANJA SANA; WAMEANZA KUTAFUTA PESA ZA KAMPENI HIVI SASA KWA KULIPWA NA TANESCO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!HATUTAKI TUMECHOSHWA NA MAFISADI HAWA!!!!!!!!!!!!!!WANA JF TUWAPE USHIRIKIANO WATU KAMA HAWA!!!!!!!!!
 
hii haijakaa sawa hata kidogo - Nasisitiza


TUUNGANE PAMOJA KUPIGANA HII VITA TAKATIFU, NAMNUKUU SUGU," KWENYE VITA YA HAKI USHINDI NI LAZIMA" NA TUIUNGE MKONO BLOG MPYA anticorruption in tanzania. SHIME WAPENDA MABADILIKO WOTE TUPIGANE HII VITA TAKATIFU, HATUNA HAJA YA KUWAPA MUDA WAKALE KRISMASI NA MWAKA MPYA KAMA JK ALIWAPA MWAKA ULE. MAANA SISI SHIDA HAZITUPI HATA HIYO NAFASI YA KUPUMUWA ANGALAU KWA KRISMASI NA MWAKA MPYA. WERE IS MY GUN?
 
Duh kwa hili ndo utajua jinsi jamaa wanavyoiba kama nchi si yao, au kwenda mbinguni siku hizi kunatakiwa pay nn maana pesa zote hizo.
 
Standards and Speed forever and always, no matter what!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! defect plse Mr Six, you are in the wrong train.
 
Sitta alipokuwa Spika alikubali kufunika baadhi ya mambo kwenye suala la RICHMOND ili kuinusuru serikali ya JK isianguke kabisa. Madhara yake ndio haya. Haya mambo yasingekuwepo sasa kama suala la Richmond lingemalizika kikamilifu.
 
Six hajawahi kuizima Richmonduli.... alitekeleza wajibu wake 100% Mtoto wa Mkulima na Mwere ndiyo waliozima maana waliagizwa kutekeleza mapendekezo ya bunge na wakagoma.
sasa tumejua Richmond ni ya nani kumbe ni EL, RA na NM aka mzee wa kikofia ok
 
Huyo ndio Samwel John Sitta. Nimefirhai sana hii mbinu ya kupigana kutokea ndani, italeta impact zaidi kuliko asingekuwa waziri. Alikubali nafasi ya kinafiki aliyopewa ili awashe moto humo humo...GOOD!...Mwisho wake mlipuko....ufisadi unateketea. Lowasa na Rostam watajuta kuhujumu mzee asirudi kwenye uspika...mwanamapinduzi ni mwanamapinduzi tu, hata umpeleke wapi...moto wake utawaka tu.

Safi sana mzee wa speed & standard.......viwango hivyo wachemshe navyo baraza la mawaziri. Hata hivyo najua watakutoa uwaziri mda sio mrefu lakini si kitu, moto unauhamishia bungeni...spika wa Lowasa na Rostam atajuuta kuwakilisha ufisadi.

Aluta Continua.....
 
Sitta afyatuka
• Adai Dowans ni genge la ulaji wa vigogo watatu


WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ametishwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), iliyoipa ushindi Kampuni ya Dowans dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), lakini akasema haya ni matokeo ya genge la watu wachache wanaofahamika ambao wameamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma. Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano katika miaka mitano iliyopita na ambaye aliruhusu Bunge kujadili masuala kashaa ya kifisadi, alisema hayo jana katika mazungumzo maalumu na Tanzania Daima kwa simu kutoka Kampala Uganda.
Alisema vigogo hao waliileta Dowans makusudi baada ya kampuni ya awali iliyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development LLC, kushindwa kutimiza malengo.
Dowans ndiyo ilirithi mkataba wa Richmond na kwa mujibu wa Sitta, njama za kuileta kampuni hiyo zilisukwa na vigogo watatu ambao ni wabunge wa muda mrefu na wamekuwa wanahusishwa na matukio mbalimbali ya ufisadi, na mmojawao ni mwanasheria maarufu aliyebobea katika masuala ya mikataba ya kimataifa. Kwa sababu za kitaaluma, gazeti hili litahifadhi majina yao kwa sasa.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta, hili ni genge ambalo limeamua kutafuna rasilimali za taifa bila huruma, na bila kujali maslahi ya vizazi vijavyo.
"Nakwambia hakuna jambo ambalo linakera kama kuona genge la watu wachache limeamua kutafuna rasilimali za taifa hili bila huruma. Wameshindwa kufikiria kizazi kijacho kitanufaika vipi.
"Hii inaletea hisia kuwa kundi hili linaendesha hujuma nzito dhidi ya mali za taifa hili… haiwezekani hata kidogo kununua jenereta halafu unasema huu ni uwekezaji… huu si uwekezaji," alisema Sitta.
Alisema hukumu iliyotolewa dhidi ya TANESCO ni mwendelezo wa hujuma kubwa dhidi ya taifa kwa vile inaonekana wazi kwamba kuna kundi la watu maarufu ambalo ndilo chanzo cha suala hilo, na ambalo kwa namna moja au nyingine lilishiriki kuhujumu mwenendo wa kesi ili serikali ishindwe, wao walipwe pesa.
Alisema Dowans ni mali ya wachache hao ambao wameamua kufumba macho ili kufanikisha malengo yao kibiashara, na kwamba umefika wakati serikali iamue kwa nguvu zote kuwashughulikia bila huruma kwa vile ni sawa na wahujumu uchumi.
"Sisi tulioko serikalini lazima tukomeshe hali hii… kwani mchezo huu umekuwa ukijirudiarudia mara kwa mara. Lazima tujipange vizuri ili kuhakikisha nchi haichezewi tena.
"Serikali iko kwa ajili ya watu. Sasa iweje tushindwe kujipanga vizuri, tunataka kuona wananchi wetu wananufaika na rasilimali zilizopo, na hiyo ndiyo sifa (yetu) kwa taifa," alisema Sitta.
Alisema hata hukumu hiyo ni matokeo ya watu fulani ambao walitaka kesi hiyo isikilizwe nje ya nchi kisha wagawane fungu la fedha zitakazopatikana.
"Inashangaza mno kuona kuna watu fulani wamekuwa wakipendekeza kesi hizi zisikilizwe nje ya nchi… lazima tujiulize, wanavuna nini? Hata hii inawezekana wazi ulikuwa mpango wao wa kuhakikisha wanapokamilisha mambo yao wanagawana wanachovuna.
"Wamesababisha mahakama zetu zinyang'anywe uwezo wa kusikiliza kesi hizi... wanawapelekea Wazungu… hii haijakaa sawa hata kidogo," alisititiza.
Kauli ya Sitta ni ushahidi mwingine wa vita ya makundi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ambayo imeibuliwa upya na sakata la Dowans.
Sitta anatoa kauli kali hii siku moja baada ya mwanasheria mkongwe anayeheshimika nchini, Jaji Mark Bomani, kuzungumza na gazeti hili juzi akisema ushindi kampuni ya Dowans dhidi ya TANESCO ni matokeo ya namna taifa lilivyoshindwa kushughulikia vema mikataba mikubwa ya kimataifa katika uwekezaji na nishati.
Alisema: "Sakata la TANESCO na Dowans linasikitisha. Nafikiri liliendeshwa kwa namna ambayo ingewafikisha wahusika pabaya kama ilivyotokea.
"Fundisho ni kwamba unaposhughulikia masuala yanayogusa mikataba ya kimataifa kama haya yanayohusu nishati, madini na mengineyo, umakini mkubwa unatakiwa," alisema Bomani.
Mjadala wa mitambo ya Dowans, uliwahi kuligawa taifa kwa kipindi kirefu mwaka 2008 baada ya Kamati Teule ya Bunge chini ya Uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe baada ya kutoa taarifa ya kuchunguza uhalali wa kampuni ya Richmond na mtakaba kati yake na serikali.
Kutokana na taarifa iliyowasilishwa bungeni Februari mwaka 2008 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alijiuzulu ikiwa ni ishara ya kuwajibika kama kiongozi mkuu wa ofisi yake iliyodaiwa kushiriki katika kuiwezesha Richmond kushinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.
Hali ilipokuwa tete, aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, aliishauri serikali kuinunua mitambo hiyo, lakini baadhi ya wanasiasa walilisukuma Bunge kukataa kununua mitambo hiyo kwa maelezo kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 inakataza serikali au taasisi zake kununua mitumba.
Wengine walikwenda mbali zaidi wakisema ununuzi wa mitambo hiyo utaifaidisha Dowans ambaye ni dada yake Richmond.
Katika uamuzi wa ICC uliotolewa na jopo la majaji watatu chini ya uenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, TANESCO imeamriwa kuilipa Dowans fidia ya zaidi ya sh bilioni 36 na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 tangu Juni 15 mwaka huu, hadi fidia hiyo itakapolipwa.
Kadhalika, jopo hilo liliamuru malipo ya sh bilioni 60 na riba ya asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.
Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi wa ICC na utawala ni sh bilioni moja zinazotakiwa kulipwa na pande zote.


Source..Tanzania daima




Yaani hapa ndo nchi inapodidimizwa... kweli hii nchi itaendelea kuwa maskini daima
 
KWA HAWA MAFISADI WA DOWANS NA WAFADHILI WAO 'MWENDO WA KUWANYATIA MMOJA BAADA YA MWINGINE, FAMILIA ZAO PAMOJA NA MALI ZAO NDIO JIBU KWETU VIJANA TANGU SASA:

Wenye magendo na nia ya dhati kuendelea kuhujumu uchumi na KUTAFUNA RASILMALI YA TAIFA BILA HURUMA, nadhani siku si nyingi sana Wa-Tanzania tutalazimika kidogo kuweka AMANI yetu kabatini na UTAWALA WA KIJANJA WA SHERIA na kuzipitia baadaye kidogo ili vijana kwanza tukamalizane kiaina na nyie. Hapo adabu itakwepo.

Ndio, nadhani njia pekee tuliobaki nayo ni hii hapa. Hakika, itabidi na familia zenu popote pale walipo nao kama hawaoni kwamba mnafanya KUFURU vitendo vyenu vinatuelekeza kuchukua hatua za makusudi kabisa ili sasa tuanze tu na nyinyi pamoja na familia zenu popote pale mlipo - KWA MWENDO WA KUWANYATIENI BILA YA KELELE ZOZOTE ZA MWIZI MWIZI - halafu matamu yake yatakua fundisho tosha kwa wengine wengi wa aina yenu.

Nyinyi si ni wajanja, na wanasheria wote mnao, taasisi zote muhimu tayari mmezinunua ndani na nje ya nchi sio??????????? Sawa basi!!! Huu ujinga tutaufumbia macho hadi lini. Ole wake mtu atumie sehemu ya KODI YANGU kuwalipeni ninyi MASHETANI WAKUBWA!!!!!!!!!!

Nao wanafamilia zenu wamekataa katakata kuwashaurini kutufanyia taifa letu huu UBAKAJI WA KUTISHA WA AINA HII, OK!!!!!!!!!! Hivi kwanza wanachi mnaowakilishwa na watu kama hawa mnajisikieje????

Mimi nimeisha pata Manati, wewe subiri dawa yao iko jikoni. Nitaanza na Makongoro Mahanga. mwingine ajitolee kumshughulikia Hosea waTAKAKURU. Chenge, Rostam na Lowasa tutapambana nao kwa namna nyingine! Hawa jamaa hawana huruma hata kidogo!
 
Vallambia hajalipwa mpaka sasa. Zaidi ya miaka 25 nafikiri. Kwa hiyo inawezekana.
Jasusi ni kweli Valambia hajalipwa, take my words, atalipwa!.
Mikataba iko governed na law of contract, yaani makubaliano ya hiari na kwenye makubaliano hayo lazima kuna kipengele cha iwapo mmoja atashindwa kutekeleza mkataba, nini kilitakiwa kufanyika sambamba na mmoja akiamua kuuvunja mkataba nini kifanyike.

Hizi ni points za kisheria na sio politics. Sitta anataka kuleta tena politics kwenye issue za kisheria. Kwa vile yeye ni mwanasheria, nilitegemea aseme hatulipi kwa hoja za kisheria na sio za kisiasa.

Mimi ni miongoni mwa niliomuunga mkono Zitto pale mwanzo kuwa ama tuzinunue ama tuzitaifishe hizo jenereta za Dowans bila kuchanganya na politics. Sitta na timu yake wakapoliticize kuonekana kuzinunua ni ufisadi, mara PPRA mara ohh.., pure politics!

Ule ulikuwa ni ufa hatukuuziba, sasa tutajenga ukuta.
Nimesisitiza mara nyingi, Tanzania kwa upande wa serikali, hatuna kabisa wanasheria makini, tumejaza watu waliosoma tuu sheria na kupewa vyeti vya LL.B na LL.M lakini hakuna kitu!

Kwa vile hukumu hiyo ya ICC lazima iwe registed mahakama zetu ili iwe applicable kwa Tanzania, serikali yetu na Tanesco bado wanayo nafasi ya kuwatumia wanasheria wa ukweli, wakaiponda ponda hiyo hukumu ya ICC na kuwapatia Watanzania haki yao dhidi ya hiki kiini macho cha Dowans, sio tuu, tusilipe hata senti tano, bali pia tuitafishe hiyo mitambo kwa ku quatify loss Tanzania kama nchi, tuliyoipata kwa Richmond waliposhindwa kutimiza wajibu wao, ambao Dowans ndio wameubeba!.
 
Gazeti la Mwananchi la leo linamripoti Waziri wa Afrika ya Mashariki Samweli Sitta akiendeleza ahadi zake za kupambana na ufisadi kwa kusema ...."Serikali isiilipe Dowans".......................Na ya kuwa pesa hizi ni mikakati ya kusaka fedha za kampeni za uchaguzi wa 2015................

Habari hii imejirudia tena kwenye magazeti ya Nipashe lenye kichwa cha habari.................."Sitta kuilipa Dowans ni kuhujumu uchumi"

Vile vile gazeti la the Citizen linayo hiyo habari.............

Sitta yuko sahihi kabisa.Kama serikali italipa fedha hizo,hatutakuwa na njia ila kuamini kabisa kwamba serikali nayo ipo katika mipango hiyo ya kifisadi.Hili liko wazi kwamba hiyo yote ni mipango iliyopangwa ili kuendeleza wimbi la kuwaibia wananchi maskini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom