Waziri Simbachawene awasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri wanaodaiwa kuhonga wapate Hati Safi

Usanii mtupu. Mfano halisi ni mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga,,, ukienda pale leo utamkuta amekaa kwenye kiti chake cha kuzunguka wakati juzi tu hapa tuliambiwa amesimamisha na watu walienda kumchunguza tuhuma na ripoti wameweka mfukoni
wanawazuga wajinga..alaf JPM anasema ukawa haitoongoza milele..
eti kisa daganya totot zao
wajinga ndo wadanganywao sisi tunaolewa mambo tunawacheka2.......mtu kma smbachawene
anapata wapi kibuli cha kuita waandishi na kutangaza ujinga wakati ye mwenyewe mpigaji...mfyuuuuu
 
kamati za bunge zilizoea kujadili taarifaza cag na kujichukulia ujiko lakini walitakiwa kwenda mbali hii simara ya kwanza ofisi ya cag kutuhumiwa kupokea rushwa
lakini waziri asiishie kuwasimamishwa inabidi waende mahakamani
 
hivi wadau kusimamishwa kazi ni tofauti na kufukuzwa kazi?,na kama ni hivyo it meanz wataendelea kupata mshahara ingawa itakuw kwa asilimia flani amabayo nahisi ni nusu mshahara? then mwisho wa adhabu atapewa tene pesa zote alizokuw anakatwa au inakuaje sielewi hapo naombeni ufafanuzi hasa kwa experience ya mtumishi wa kawaida wa umma
 
Hiii nchi ilikuw ishakuw kama chaka la kijiji,anaejiskia kutata nyasi ,kuni, gogo ruksa,majipu yakitumbuliwa walau unapata kanegative ka picha hiii nchi ilikuw wapi na tungekuw wapi kama isingekuw utawala mpya,
 
Nadhani tungefuta watumishi wote tu... tuanze upya!!!

Hizi fukuza fukuza kila siku tutazizoea sasa
Baadhi ya hawa wanaofukuzwa ndio watakaofilisiwa, hivyo huu mchakato ni muhimu sana. Anapofungwa mtu, na mali zake zinafilisiwa, ni vitu vinavyokwenda sambamba.
 
Kwa wafanyakazi wa serikali, ile mikopo mliyoichukua kwa kutegemea kazi,sasa jaribu kufikiria mara mbili. Halafu jaribuni kuongea na familia kuhusu kubana matumizi, kwa kasi hii ya kufukuzana, akiba muhimu. Maana wengi wenu mna vimeo ofisini, siku kikiguswa inaweza kuwa hatari.
 
UFAFANUZI KUHUSU MATUMIZI YA NAPTHA
Nimshukuru mleta mada, kwani ina hasi na chanya.
Niongezee kwa hoja ya AVEROES kwanza kurusha mwanga kidogo kwa uzalishaji wa hii NAPTHA. NAPTHA huzalishwa kwa wingi kutokana na usafishaji mafuta ghafi (crude oil) ambapo, crude oil hutiwa ktk kinu cha moto au joto kali inayopelekea kuzalisha mafuta na gesi tofauti ktk layers tofauti.
Layers hizi hutofautisha mafuta na gesi tofauti yaani PETROL, KEROSENE (mafuta ya taa), DIESEL, mpaka chini kabisa kunapatikana LAMI.
Hali kadhalika gesi aina tofauti kama butane, propane, nakadhalika hupatikana hapa. NI VYEMA pia nikawajuza Watanzania kuwa hii gesi ya kupikia majumbani, iitwayo Liquefid Petroleum Gas au LPG, inayosambazwa katika mitungi kama ORYX, MIHAN, CAM GAS, LAKE GAS nakadhalika hutokana na mchanganyiko wa PROPANE NA BUTANE kupata LPG. Huingizwa nchini kutoka nchi zinazozalisha mafuta na kusambazwa hapa nchini katika mitungi ya gesi ya kilo 3, 6, 15, 38, na hadi mitungi mikuuubwa ya kilo 500, 1000 nakadahlika.
Sasa tofauti za mafuta haya huja kwenye parameters tofauti kama boiling points, flammability rates, viscocity, density nakadhalika nakadhalika.
Refineries tofauti duniani huenda wakazalisha bidhaa Fulani na Fulani zaidi kulingana na mikakati yao , mfano huenda akaset kupata petro zaidi.
Ama nikirudi kwenye NAPTHA, hii imeegemea zaidi katika PETROLI na tofauti zinakuja kwenye parameters kama nilivitaja hapo juu. Nirejee kusema
Kabla sijahama kutoka uchimbaji wa mafuta ghafi (crude oil) na usafishaji wa mafuta yaani petroleum refinery, NIWAKUMBUSHE Watanzania refinery tuliyokuwa nayo ya TIPER ambayo kwa leo ni mali ya kampuni ya ORYX. Refinery hii ilitumika miaka ya nyuma kusafisha mafuta, kwa maana mafuta ghafi yaliingizwa nchini, na uzalishaji au usafishaji wa mafuta kama nilivoeleza awali ulifanyika hapa nchini. Refinery hii ilikufa kifo cha mende, ingawaje ki uchumi ilikuwa na faida.

Katika uchimbaji wa NATURAL GAS, pia hupitia process kama ya hapo juu, ila hapa huingizwa kwenye mtungi mkuuubwa kwanza wa High Pressure Separator, ambapo GAS ASILIA huchujwa, ikielea juu kwa sababu ya uwepese wake (density), na chini yake kubaki CONDENSATE. Hii condensate, hukamuliwa maji (water) na kutolewa na albaki kuingizwa tena katika Low Pressure Separator. Hali kadhalika hupatikana maji na mabaki kuwa aina tofauti za kinachofanana na mafuta ghafi. Zao hili sasa, huwekwa ktk treatment tofauti kupata kitu gani mzalishaji anataka….ambapo, pamoja na mengineyo hupatikana NAPTHA.

Hii NAPTHA sasa hupitia pia michakato tofauti kama vile kuiondolea sulfur na treatments nyinginezo zinazoweza kukupatia PETROL.
Vile vile, kutokana na NAPTHA, tunaweza pata SOLVENTS, sabuni za maji au cleaning fluids, diluents (nimekosa neon la Kiswahili hapa) za rangi, varnish, asphalt, pamoja na bidhaa kama solvents katika makampuni ya mpira (rubber) , viberiti vya gesi, hata mali ghafi katika dry cleaners na kutengeneza mbolea.

Sasa basi, Watanzania tunapotezwa sana katika propaganda kuliko kuelewa vitu, na kuchangamkia FURSA. Kuliko kumshambulia OILCOM, hapa naona fursa nyingi, nyingi, na nyingi ambazo OILCOM aliona baadhi, na sio kwa U-HASI BALI KWA U- CHANYA.
Zipo sheria za OSHA zinazosimamia athari au maelekezo ya viwango vya matumizi ya NAPTHA. Na sheria nyingine nyingi katika hili. Kwa faida yako, pia kasome kidogo kuhusu MSDS
Mwisho nimuulize ndugu yetu huyu mtoa mada, alikuwa wapi toka OILCOM anaanza biashara miaka ya tisini? Vyombo husika vyote vililala? Na je mbona hatujasikia magari ya wateja wa OILCOM yakiharibika miaka yote hiyo? Mbona hii story inakuja baada ya baadhi ya watu kukosa tenda ya kununua CONDESATE? Na baadhi ya makampuni kutumbuliwa majipu ya kodi?

Labda pia nieleze kidogo hapa. TPDC ilitengaza tenda ya kuuza CONDESATE. Wadau mbalimbali waliomba na aliyeshinda akapewa. Bahati mbaya mshindi huyu alipigwa chini baada ya muda kwa sababu siwezi zieleza hapa. Mimi sio mchafua watu bhaaana!!!!

Hivyo ndugu, ninapenda kuamini kuna motivation ya kuagizwa kupewa vijisenti kuchafuana ila tufahamu, Watanzania walio makini hawaangalii propaganda na maneno hewa, ila scientific facts, na uhalisia. Tanzania ya leo inahama kutoka enzi za kuamini udaku, fitna na wauza maneno. Ila tuwapatie WATANZANIA uchambuzi wa hoja na scientific facts.
Ahsanteni na siku njema.
 

Attachments

  • mafutaaa.docx
    16.2 KB · Views: 78
Back
Top Bottom