barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amewasimamisha kazi wakurugenzi wa Halmashari nne nchini kwa tuhumiwa za kutoa rushwa kwa maofisa wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kubatilisha hati chafu zilizopata halmashauri zao.
Wakurugenzi hao ni wa Halmashauri ya Manispaa ya Misenyi Kagera Elizabeth Kitundu, Halmashauri ya Nanyumbu Mtwara Mohamed Kesenge, wa Halmashauri ya Kilolo Iringa Luckson Pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume.
Wakati huo huo Simbachawene amemvua madaraka mkurugezi wa mji wa Tunduma Halima Mpita na kuagiza mamlaka zimsimamishe kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za Halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.
=================
WAZIRI nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne ambao ni Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara, Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita, baada ya kubainika wakurugenzi hao wametenda kosa la kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ili wapewe hati safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi.
Pia, Waziri Simbachawene amemsimamisha kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma Mkoani Mbeya Bi Halima Ajali ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka.
Hata hivyo Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari mda huu Jijini Dar es Salaam, Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake.
Waziri Simbachawene ameyataja makosa yao kila mmoja wao ambapo amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu ametenda ametanda kosa baada ya kumwagiza mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa ya (CAG) kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo.
Ambapo Maafisa hao wa CAG waliopokea pesa hizo ni Stevin Buawa, John Elias pamoja na Kilembi Mkole.
Waziri Simbachawene amesema Katika Halmashauri ya Nanyumbu ambapo amedai tarehe 26 Juni 2015 mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa wamlimkabidhi fedha ya Milioni 3 na laki tano afisa wa CAG ambapo afisa huyo alipokea pesa hizo kwaniaba ya wenzake kwa lengo la kutoa hati safi.
Sanjari na huyo pia Waziri Simbachawene amesema hata katika Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita ambapo amedai mwezi Novemba mwaka jana, Mkurugenzi wa Halmahsauri hiyo Abdalla Mfaume na mweka hazina wake walimpatia fedha maafisa wakaguzi wa CAG ambao walipokea rushwa ya milioni 16 ili wafiche ufisadi walioubaini.
Hata hivyo Simachawene amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ukiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi.
Aidha, Waziri Simbachawene amesema katika wilaya hiyo ambapo mkaguzi wa mkoa wa Geita alipewa Rushwa kutoka kwa viongozi wa wilaya hiyo ili kuficha ufisadi wa milioni 90 ambazo zilitengwa kwa ajili ya kununulia dawa.
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amesema Kwa mamlaka aliyekuwa nayo amewasimamisha kazi pia mkurugenzi wa Mji wa Tunduma Bi Halima Ajali baada ya kubainika kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.
Amesema Mkurugenzi huyo alikuwa anawatumia watoto wake kwenye shughuli za Halmashauri huku akiwalipa pesa pamoja na kuikosesha mapato Halmashauri hiyo yaliyotokana na Ushuru wa Magari kwenye Mpaka wa Tunduma.
Vilevile waziri Simbachawene amemteua Erick Mpunda kukaimu nafasi ya mkurugenzi huyo ambapo Mapunda kabla ya kuteuliwa kwake hapo alikuwa Mkuu wa Rasilimali watu wmkoani Mbeya.
Waziri Simbachawene amemuagiza Katibu kongozi kuwasimamisha watendaji wote ambao walihusika na rushwa hizo kwenye ofisi ya CAG kwa madai kuwa wapo kwenye Mamlaka yake.