Waziri Nundu awacharukia wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Nundu awacharukia wabunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 13, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Ni waliokosoa Muswada wa Ununuzi

  [​IMG]
  Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu  Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, amewajia juu wabunge waliopinga hatua ya serikali ya kutaka kupitishwa kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma, kuruhusu ununuzi wa vifaa vilivyotumika, akisema wametumwa.
  Muswada huo wa Sheria ya Ununuzi ya mwaka 2011 ambayo inafuta Sheria ya mwaka 2004, uliowasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Fedha,

  Mustafa Mkulo, unapendekeza serikali iruhusiwe kununua vifaa maalum vilivyotumika ambavyo ni vya gharama kubwa na ambavyo ni vigumu kupatikana kwa urahisi vikiwa vipya na upatikanaji wake kuchukua muda mrefu.
  Muswada unavitaja vifaa hivyo kuwa ni ndege, meli, mabehewa na injini zake.

  Wabunge wengi waliochangia muswada huo kuanzia juzi hadi jana mchana, walipinga kununuliwa kwa vifaa hivyo vilivyotumika kwa maelezo kuwa vinaweza kuleta majanga.

  Akichangia muswada huo muda mfupi kabla ya kusitisha shughuli za Bunge jana mchana, Waziri Nundu aliutetea uamuzi huo wa serikali, akisema kuwa kununua vifaa vilivyotumika kama ndege, meli, mabehewa na injini ni utaratibu wa kawaida na kwamba unafanyika katika nchi zote duniani.

  Nundu ambaye alijitambulisha kuwa ni mtaalamu wa kimataifa katika sekta ya anga, alisema mashirika ya ndege duniani yakiwemo makubwa, yamekuwa yakinunua au kukodi ndege zilizotumika.
  Baadhi ya mashirika ambayo aliyataja kuwa yamekuwa yakifanya hivyo ni British Airways, Ryaair, Air France, Virgina Atlantic, Lufhthansa na Kenya Airways.

  Katika kuthibitisha kuwa anazo taarifa za kutosha ili kutetea hoja yake, Nundu alitaja tarehe ambayo kila shirika lilikuwa linanunua ndege mpya pamoja na tarehe ya kuiuza kwa shirika lingine.

  “Baadhi yenu mnatumwa. Kwa nini tunaposema ndege zinakuja ndipo mnasema zitaleta ajali,” alisema Nundu kwa jazba bila kutaja mtu au watu waliowatuma wabunge kupinga mpango huo wa serikali.
  Hata hivyo, wakati akiendelea kutoa maneno makali, muda wake wa kuchangia ulimalizika na Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene,

  kumsimamisha. Kabla ya kuwashambulia wabunge walikosoa, Nundu alisema sio kweli kwamba ndege zilizotumika hazisababishi ajali kwa sababu ndege zote zinatunzwa katika mfumo mmoja wa kimataifa kuhakikisha kuwa ni salama.
  Alisema kuna muda wa kuzifanyia ukaguzi na kutoa mfano kuwa kila inapotua hukaguliwa. Pia alisema ndege hazina umri wa mwisho wa kutumika.

  Aliwahakikishia wananchi kwamba hakuna ndege chakavu itakayoingia nchini bali zilizotimiza taratibu.
  Wabunge waliochangia na kupinga kununuliwa kwa vifaa vilivyotumika zikiwemo ndege ni Dk. William Mgimwa (Kalenga-CCM), alisema kununua mali chakavu kama ndege, meli, behewa au kichwa cha treni kunaweza kuhatarisha maisha ya watu.

  “Vile vile, unaweza kuingia katika hasara ya matengenezo. Ufanisi wake ni mdogo kuliko chombo kipya,” alisema.
  Christowaja Mtinda (Viti Maalum-Chadema), alisema hakubaliani na muswada huo kwa kuwa kuruhusu kununua vifaa vilivyotumika ni kuleta makaburi.

  Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini-Chadema), alisema kupanga kununua vifaa vilivyotumika ni fikra za kimaskini na kuishauri serikali kwamba ni bora kukopa kuliko kuvinunua.

  Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF), alisema kuruhusu ununuzi wa vifaa vilivyotumika kunaweza kuligharimu taifa kwa kuwa kuna ukosefu mkubwa wa maadili katika kusimamia sheria ya manunuzi.
  Alisema miaka ya nyuma maadili yalipokuwa yanasimamiwa, Waziri na Mkurugenzi wa lililokuwa Shirika la Ndege nchini (ATC) walinunua ndege

  mbovu, lakini uamuzi huo uliwagharimu kwa kuwa walifutwa kazi.
  Wabunge waliotetea ununuzi wa ndege, meli, mabehewa na injini zilizotumika ni Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM); Diana Chilolo (Viti

  Maalum-CCM); Asumpta Mshamu (Nkenge-CCM); Henry Shekifu (Lushoto-CCM) na Dk. Benedith Mahenge (Makete-CCM).
  Na katika hatua nyingine, baadhi ya wabunge wamesema kuwahusisha madiwani kupitia tenda za manunuzi kutadhibiti vitendo vya ufisadi katika halmashauri.

  Wabunge hao wametoa kauli hizo wakati wakichangia Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 inayofuta sheria ya 2004, uliowasilishwa juzi na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo.

  Muswada huo unapendekeza kuwa kamati za fedha za halmashauri zipitie mikataba ya manunuzi kabla ya kusainiwa. Kabla ya hapo, michakato ya manunuzi ilikuwa ikifanywa na watendaji na wenyeviti wa halmashauri ndio waliokuwa wakisaini mikataba hiyo bila madiwani kuhusishwa na matokeo yake mikataba mingi ilikuwa ikiziingiza halmashauri katika hasara.

  Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi, alisema pamoja na madiwani kushirikishwa katika kupitisha mikataba ya manunuzi, mikataba hiyo inapaswa kuandikwa kwa Kiingereza na Kiswahili ili iweze kueleweka kwao vizuri.

  Mbunge wa Makete (CCM), DK. Benedith Mahege, alisema ni vizuri madiwani kushirikishwa, lakini pia kiwekwe kitengo cha manunuzi kila wilaya ili iwe rahisi kuzifuatilia halmashauri katika manunuzi.
  Seleman Said Jafo wa Kisarawe (CCM), alisema kuruhusu madiwani kushirikishwa katika mikataba ya manunuzi kutasaidia kudhibiti ubadhirifu na
  udanganyifu wa watendaji ambao waliitumia vibaya fursa hiyo.

  Subira Khamis Mgalu wa Viti Maalum (CCM), alisema madiwani kutoshirikishwa katika mikataba ya tenda kumezisababishia halmashauri hasara na kutoa mfano kwa Halmashauri ya Kinondoni ambayo ilisaini mkataba na mwekezaji mmoja kwa kumpangisha katika eneo ambalo yeye

  anachukua asilimia 75 ya mapato na halmashauri kuambulia asilimia 25 tu. Alisema mkataba huo wa miaka mingi ulisainiwa na makamu mwenyekiti bila madiwani kuhusishwa.
  Menrad Kigola wa Mufindi Kusini (CCM), alisema uamuzi wa kuwashirikisha madiwani katika uamuzi wa tenda ni mzuri kwa sababu huko nyuma

  madiwani walipokuwa wakiulizwa walikuwa wakisema hawajui.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri, akichangia muswada huo, alisema utaratibu katika kanuni uliwapa madaraka watendaji kuamua masuala ya manunuzi bila kuwahusisha madiwani na kuipongeza serikali kuandaa

  sheria hiyo ambayo itathibiti madudu yaliyokuwa yakifanyika katika halmashauri.
  “Muswada utazuia watendaji kupitisha tenda badala yake kamati za fedha za halmashauri zitaidhinisha. Utasaidia kudhibiti ufisadi katika manunuzi na uchakachuaji,” alisema Mwanri na kuongeza: “Tumejiandaa kuhakikisha hakuna kuchezewa chezewa.”

  Aidha, Mwanri alisema wanasheria wa halmashauri watatumika kupitia mikataba na kuhakikisha haichezewi kwa kuwa asilimia 70 ya fedha za halmashauri zinapotea kupitia katika manunuzi.
  Akisisitiza suala la uadilifu na uaminifu,alisema: “Kama nchi hii haitakuwa na watu wa kuifia, hatuendi popote.”
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. OPTIMISTIC

  OPTIMISTIC Senior Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mimi nimepata mashaka na na uwezo wa wabunge kujenga hoja. Tatizo sio kusababisha ajali that is minor tatizo ni kama mitambo chakavu ilinunuliwa tukiwa na sheria inayozuia itakuwaje baada ya kuruhusu
   
 3. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni point muhimu, cha musingi ni kuwa kukishashamiri vitendo vya kukosa uadilifu yaani ufisadi wa kupindukia, dawa yake ni kuwa na regulations zenye kudhibiti siyo kulegeza. Kwa kuruhusu ununuzi wa vitu vilivyotumika katika mazingira ya hapa kwetu, wataleta hata visivyotumika kabisa au vilivyoopolewa toka madampo ya ulaya, marekani na mashariki ya mbali. Tukumbuke jinsi ATCL walivyokodi ndege AIRBUS chakavu toka Caribean / Venezuela ilivyokaribia kuktutoa roho watanzania!! Nashangaa huo ushauri wa Waziri Nundu haukuzingatia hali halisi ya Tanzania, au huyu kakaa sana nje ya nchi kwa muda mrefu yuko dis-connected na hali halisi???? Wanasiasa wetu bwana, wee acha tu!!!!
   
Loading...