chase amante
JF-Expert Member
- Feb 24, 2018
- 5,553
- 2,073
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano.
Waziri wa Teknolojia na mawasiliano, jana alitangaza kua anawakaribisha watu kuwekeza kwenye mtandao wa 5G nchini Tanzania, na pia mpango wake wa kubadili mfumo wa 2G kwenda 3G unaotumika kwenye simu za tochi.
Pia, akatangaza na mpango wake wa miaka mitano wa wizara yake kuanzia 2021-2022 hadi 2025-2026 wa kuiendeleza sekta hii ya mawasiliano na teknolojia.
Nakiri, hiyo Yote ni mipango mizuri lakini haitoshi kutufikisha kwenye maana halisi ya mapinduzi ya kidigitali.
Mapinduzi ya kidigitali(digital revolution) nchini tanzania yameanza miaka ya 2005,na yalihusisha ujenzi wa mkongo wa taifa na minara ya simu.
mapinduzi haya, yanahusisha uwepo wa CCTV kamera, drones, maroboti na miji ya kisasa(smart cities).yana faida nyingi km kuongeza makusanya ya kodi na kupunguza rushwa, kupunguza uharifu na mengineyo.
Pia yana athari nyingi sana, ambazo zingine tunazioana kupitia wizi wa kwenye mitandao na simu.pia yanaweza kutumika kuchunguza watu, kuiba taarifa za watu bila ridhaa yao.
Kenya na Rwanda ni nchi zilizoendelea sana kwenye mapinduzi ya kigitali na ni majirani zetu. Lkn sisi bado tupo nyuma sana. Kwanza, mkongo wa taifa haujafika maeneo ya vijijini. Hii inawakosesha fulsa wananchi wa kijijini zikiwemo kupata intaneti.
Na kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kuwepo kwa 3g coverage na ustawi wa jamii. Kuna utafiti ulifanywa senagal (nimekosa link yake), ulionyesha maeneo yenye coverage 3g, wananchi wake waliongeza matumizi kwa 14% na kupunguza umaskini kwa 10%.
Hata smart cities hapa Tanzania Sidhani kama zipo. Waziri aende kujifunza Kenya, kwani huo ndo ujirani mwema.
Sisemi kwamba tukurupukie tu hizi teknolojia, bali tutumie muda kujifunza faida zake , na hasara zake kisha tuamue zipi nzuri na zipi mbaya.