Waziri Ndalichako ataka ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga ukamilike kabla ya Juni 2022

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia Profesa Joyce Ndalichako ameitaka SUMA JKT Kanda ya Magharibi kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Chuo Kipya cha Ualimu Kabanga ifikapo Juni 2021.

Profesa Ndalichako ametoa agizo hilo mjini Kasulu baada ya ukaguzi kazi ya ujenzi wa chuo hicho na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji mradi huo.

"Ujenzi wa Chuo cha Kàbanga ulianza Machi 19, 2019 na ulipaswa kukamilika Juni 2020, pamoja na mkandarasi kuongezewa muda wa miezi nane bado kazi haijakamilika, hili halikubaliki,"alisema Waziri Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 10.6 bado unasuasua, na hata katika eneo la ujenzi hakuna wafanyakazi wala vifaa huku SUMA JKT wakiwa tayari wameshalipwa bilioni sita.

"Nimetembelea na kukagua kila jengo hapa, majengo mengine hayana wafanyakazi na yaliyo na wafanyakazi ni wachache na wala hakuna vifaa vya kufanyia kazi hapa. Mradi huu umekuwa ukisuasua tangu umeanza" amesema Waziri Ndalichako.

Amesisitiza kukamilika kwa ujenzi huo ili kuokoa wanachuo wanaoendelea kutumia majengo ya chuo cha zamani ambayo ni hatarishi na kwamba ubovu wa majengo ya Chuo cha zamani ndio umepelekea Serikali kuja na uamuzi huo wa kujenga upya Chuo hicho.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Huruma Mageni amemwambia Waziri kuwa chuo hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanachuo 800 kwa mara moja ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi utawezesha kudahili wanachuo 400.

Mageni ametaja majengo yatakayojengwa katika awamu ya kwanza ni pamoja na maktaba, bweni moja la wanachuo wa kike na moja wa kiume, ukumbi wa mihadhara pamoja na mikutano, bwalo la chakula na jiko.

Majengo mengine ni jengo moja lenye madarasa kumi, jengo la utawala, zahanati na nyumba nne za wakufunzi.

Naye msimamizi wa ujenzi kutoka SUMA JKT Luteni Kanali Onesmo Njau amesema wanashukuru wamepata fedha nyingine kutoka Wizara ya Elimu na kuwa wanakwenda kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri na watakamilisha kazi hiyo kulingana na maelekezo.

Wakati huo huo katika kuonesha msisitizo wa uhitaji wa Chuo hicho kukamilika, Ndalichako ameambatana na wakandarasi hao kuwaonesha hali halisi ya uchakavu ya majengo yanayotumika sasa.

IMG-20210304-WA0000.jpg
IMG-20210304-WA0002.jpg
IMG-20210304-WA0003.jpg
IMG-20210304-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom