Mdakuzi mkuu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 212
- 720
Nape ,Nape kulikoni?Umesimamia upande gani?Ukakasi huu..
Suala la mtu fulani kuvamia kituo cha Clouds lilileta sintofahamu mpaka ukaamua kuwatembelea na kusema mawili matatu, ikiwemo kuchukua hatua baada ya ripoti ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza swala hili,ambayo wewe mwenyewe ulisema ingekamilika na kukabidhiwa ndani ya masaa 24 (juzi jumatatu, March 20,2017).
Lakini katikati kamati ikiwa kwenye uchunguzi,Mh Rais alisema "Makonda chapa kazi, nasema chapa kazi". Ilikuwa katika kukoleza kwamba,Makonda alikuwa na yupo sahihi kwenye tukio la uvamizi Clouds Media.
Sasa wewe Nape, kauli yako ya kwamba mtatoa maamuzi na mtachukua hatua kali imekaaje hii?Maana bado tunasubiri.
Kama imezimwa na kwamba huwezi tena, tengua kauli yako na si kukaa kimya tu. Kama vipi hamia CHADEMA kama mwenzako Msukuma wa Geita.
Asubuhi njema.