Nape Nnauye: Nilikatazwa Kwenda kuchunguza Uvamizi Clouds, niliambiwa nitafukuzwa kazi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema wakati anaenda kufanya uchunguzi wa uvamizi uliofanywa Clouds na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alizuiwa kwa kuambiwa kuwa atafukuzwa kazi kama ataenda kuchunguza tukio hilo.

“Asubuhi yake nilizuiwa kwenda kuchunguza, nikaambiwa ukienda utakuwa hauna kazi. Nikasema ni bora nisiwe na kazi lakini nilinde heshima.”

Ameongeza, “Kwa sababu katika mazingira wewe ndiyo waziri, watu wanavamia kituo, halafu wewe unatakiwa usiende. Unachagua kati ya heshima na kazi. Heshima utaenda nayo, kazi ipo siku itaondoka tu, kwa hiyo nikachagua heshima ambayo nadhani naendelea nayo leo”.

"Kwamba mwajiri anasema ukienda kazi huna, nikasema sawa, halafu mimi naendelea kusema tunachunguza, mwajiri anasema bhana wewe uliyevamia endelea na kazi vizuri hakuna shida"

Baada ya tukio hilo, Waziri Nape amebainisha kuwa waliunda Tume ambayo siku ya kusoma ripoti walianza kushauriana wasome au wasisome, ambapo aliwaaambia wajumbe wa tume kuwa kama wataisoma yeye hatakuwa tena na hiyo kazi.

"Wakasema Mhe. Waziri tukisoma utafukuzwa kazi, nikasema ndiyo na nimetoka kuthibitishiwa pia sasa hivi maana kabla ya pale nilipitia mahali, nikasema jamani ile taarifa ipo tayari na wananisubiria tufanyeje? Wakasema sasa uamue, uisome afu uondoke au uinyamazie uendelee na kazi. Nikatafakari, nikachagua heshima maana haviwezi kukaa pamoja"

Amekiri kuwa hata kitendo cha yeye kuondolewa wizarani hakikumshangaza kwa kuwa alijua litatokea, wakati anapokea taarifa aliwaambia wajumbe wa tume kuwa kuna gharama za kulipa baadae na yeye yupo tayari.
 
Nape mbona unataka ushujaa usio na msingi. Ulienda kuomba msamaha wa nini ikulu? Kama ulikuwa na misimamo si ungekaa zako Lindi ulime kama Ally Hapi then ndio uje utusimulie?

Nape fanya kazi uliyotumwa, hizo hadithi zako hazibadili chochote. Tasnia unayosimamia ina matatizo mengi na mengine ulishiriki kutengeneza ikiwemo sheria ya kukataza bunge live.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema wakati anaenda kufanya uchunguzi wa uvamizi uliofanywa Clouds na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alizuiwa kwa kuambiwa kuwa atafukuzwa kazi kama ataenda kuchunguza tukio hilo.

“Asubuhi yake nilizuiwa kwenda kuchunguza, nikaambiwa ukienda utakuwa hauna kazi. Nikasema ni bora nisiwe na kazi lakini nilinde heshima.”

Ameongeza, “Kwa sababu katika mazingira wewe ndiyo waziri, watu wanavamia kituo, halafu wewe unatakiwa usiende. Unachagua kati ya heshima na kazi. Heshima utaenda nayo, kazi ipo siku itaondoka tu, kwa hiyo nikachagua heshima ambayo nadhani naendelea nayo leo”.

"Kwamba mwajiri anasema ukienda kazi huna, nikasema sawa, halafu mimi naendelea kusema tunachunguza, mwajiri anasema bhana wewe uliyevamia endelea na kazi vizuri hakuna shida"

Baada ya tukio hilo, Waziri Nape amebainisha kuwa waliunda Tume ambayo siku ya kusoma ripoti walianza kushauriana wasome au wasisome, ambapo aliwaaambia wajumbe wa tume kuwa kama wataisoma yeye hatakuwa tena na hiyo kazi.

"Wakasema Mhe. Waziri tukisoma utafukuzwa kazi, nikasema ndiyo na nimetoka kuthibitishiwa pia sasa hivi maana kabla ya pale nilipitia mahali, nikasema jamani ile taarifa ipo tayari na wananisubiria tufanyeje? Wakasema sasa uamue, uisome afu uondoke au uinyamazie uendelee na kazi. Nikatafakari, nikachagua heshima maana haviwezi kukaa pamoja"

Amekiri kuwa hata kitendo cha yeye kuondolewa wizarani hakikumshangaza kwa kuwa alijua litatokea, wakati anapokea taarifa aliwaambia wajumbe wa tume kuwa kuna gharama za kulipa baadae na yeye yupo tayari.
JamiiForums1622786688.jpg
 
Back
Top Bottom