Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Ameyasema leo alipokuwa anaongea na wanahabari kwenye maadhimisho ya siku ya redio duniani.
''Kumekuwa na mjadala mkubwa wa madawa ya kulevya, wito wangu kwa wanahabari,.. Tuliunganishe Taifa letu, tuungane katika kupiga vita madawa ya kulevya, lakini tuungane kwa kuliunganisha taifa letu kuwa kitu kimoja, tupambane dhidi ya madawa ya kulevya, hili ndilo kubwa sana.
Lakini wakati huo maisha mengine lazima yaendelee. Iko shida kila kitu sasa hivi hata ukikohoa kinahusishwa na madawa ya kulevya.
Tuna vita ya madawa ya kulevya, vyombo vyetu vyote lazima viungane kwa pamoja, Tasnia zote ninazoziongoza lazima zipige vita hii kwasababu kushinda ni lazima na Rais ameshatuelekeza kupambana na madawa ya kulevya kwa kutenda haki na kusimamia haki.
Tusimuonee mtu lakini lazima tuungane wote pamoja, watanzania wote kwa pamoja.
WITO KWA WANAHABARI; Sisi tuna uwezo wa kuliunganisha Taifa letu likapambana na vita hii ya madawa ya kulevya kwasababu athari zake ni kubwa.
Naomba kutumia siku hii ya Redio duniani kutoa wito na ombi maalum kwenu na kwa wote ambao wako chini ya wizara yangu tuungane kwa pamoja tumuunge mkono Rais na wote wanaopambana na vita hii ya madawa ya kulevya.