MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Mh Nape nadhani wewe uko tofauti kidogo na vituko vinavyoendelea katika taifa hili pamoja na wewe kua mfia chama wa CCM, Wewe ni nembo ya vijana waliolelewa katika familia za kiuongozi wakajifunza,wakelimika na kustaarabika. Tunajua kuna maamuzi ulikua ukiyachukua kwa mashinikizo lakini hivi sasa tunakuona kua umechoka brother! Umechoka baada ya kuona maamuzi yako si kitu kwa watu flani.
Kiukweli wewe ni binamu yangu japo sikuwahi kulisema hili humu, lakini nikuambie kabisa kama una nia na malengo makubwa na taifa hili baadae ukiamua kujiuzulu kwa kutofurahia madhambi flani utajijengea heshima kubwa sana na utakua umelijenga na kulikuza jina lako.
Huwezi kutoka kwenye madia waziri mzima ukatoa msimamo wako na kuelezea hatua ulizoanza kuzichukua anatokea mtu mmoja akakukatisha tamaa, hata ukifanya uchunguzi na kamati yako hiyo unafikiri nani atakuelewa?