Waziri Nape kuzindua msimu mpya wa mashindano ya Miss Tanzania 2016

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
OTH_4512.JPG

Mkurugenzi wa lino International Agency LTD, Hashimu Lundenga akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) katika ukumbi wa idara ya habari (MAELEZO), kuhusiana na msimu mpya wa mashindano ya urembo ya miss tanzania 2016. Lundenga amesema msimu huo mpya unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya jumamosi Machi 19,2016 katika hotel ya Ramada iliyopo eneo la kunduchi jijini Dar. Katika uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake mgeni rasmi amepengwa kuwa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Mh. Nape Moses Nnauye. Kati ni mshindi wa Miss tanzania 2014-2015 Lilian Kamazima pamoja na mkuu wa kamati ya itifaki wa kamati ya miss Tanzania Albert Makoye.
OTH_4512.JPG

Lundega akifafanua jambo kwa umakini mbele ya wanahabari(hawapo pichani)
Lundenga amesema katika uzinduzi wa msimu huo mpya, utawakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo wakiwemo wabunifu wa mavazi, mawakala mbalimbali wanaoandaa mashindano ya miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini. Kama vile haitoshi lundenga alibainisha kuwa pia wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ambao miongoni mwao wanatarajia kuwa wadhamini wa shindao hilo kwa mwaka huu.

katika kunogesha uzinduzi huo wa aina yake, Lundenga amesema kuwa burudani kadhaa zitakuwepo akiwemo msanii wa kizazi kipya Linnah Sanga na msanii wa ngoma za asili Wanne Star.

Lundenga alisema alisema baada ya uzinduzi huo kufanyika jijini Dar, utahamia mkoa wa arusha ambako pia kutakuwa na aina nyingine ya uzinduzi, "Uzinduzi huo ukikamilika itafuata ratiba ya semina ya mawakala na kuanza kwa semina ya mawakala na kuanza kwa mashindano ya urembo katika ngazi za vivutio, Wilaya, Mikoa na Kanda", alisema Lundenga.

Amesema kuwa mpaka sasa wadhamini kadhaa wamejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kudhamini shindano hilo katika ngazi ya taifa. Lundenga ameyataja makampuni ambayo yamedhamini uzinduzi huo wa shindano la urembo la Miss Tanzania 2016 kuwa ni Ramada Resort Dar, Naf Beach Hotel Mtwara, Kitwe General Trader, CXC Africa, MMI Tnzania,Mwandago Investment Ltd, Break Point pamoja na GSM Media.
Chanzo: Michuzi
 

Attachments

  • 2.JPG
    2.JPG
    21.4 KB · Views: 90
Back
Top Bottom