Lancashire
JF-Expert Member
- Sep 20, 2014
- 14,057
- 10,364
Viongozi mnaleta utani kwenye mambo ya msingi. Kuchumi wa viwanda mlidhani lelemama.
Watanzania au huyu jamaa?Watanzania TUNAONGEA sana
Vpo na vya kusaga mahindi, kukamua mafuta ya alizetikweli mkuu,vidumu vya gongo vya chama cha mapinduziiiiiii!!!!! vidumuuuu!!
Ni kweli , maana hata wale waranda mbao kule keko na wakereza miguu nao wanamiliki viwanda .View attachment 424435
Kuelekea uchumi wa viwanda nchini, serikali imefanikiwa kufufua na kuanzisha viwanda ambapo kwa sasa vinavyofanya kazi vipo zaidi ya 52,000. Sekta hiyo pia imetajwa kuwa inatarajia kukuza uchumi wa watanzania asilimia 40.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya viwanda Tanzania yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam kuanzia Disemba 7 hadi 1, 2016.
“Kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda, nilipewa maelekezo kufanya mambo matatu, ikiwemo uhakikisha vilivyopo ambavyo vingi vilikuwa vinazalisha chini ya kiwango vinaongeza uzalishaji, pili vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi vinafanya kazi na la mwisho nilipewa agizo la kuhakikisha wekezaji wa ndani na nje ya wanakuja kuwekeza,” amesema na kuongeza.
“Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu serikali hii iingie madarakani, kuna viwanda 52,000 vinafanya kazi na kwamba asilimia 40 ya watanzania uchumi wao utatokana na viwanda.”
Aidha, Mwijage amesema Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia taasisi yake ya Mamlaka na Maendeleo ya Biashara Tanzania, imeandaa maonesho yatakayokutanisha wadau wa sekta ya viwanda kwa lengo la kutangaza pamoja na kujadili fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.
Amesema maonesho hayo pia yatatoa taswira ya juhudi za ujenzi wa viwanda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Chanzo: Dewji Blog
Dah kwa viwanda elfu 52 nadhani hata ujerumani nchi iliyoendelea zaidi ulaya kiviwanda haitufikii,
Uwongo mwingine bwana wala huhitaji PhD kung'amua
Kiwanda cha kuchoma mahindi
Hata kutengeneza gongo ni viwanda cha vinywaji.sasa kama tunazungumzia viwanda 52000 vya kutengeneza chibuku basi sawa.tuna uchumi wa viwanda.Kiwanda ni nini?
Na sifa za kinachoitwa kiwanda ni zipi?
Nimenda chungulia website ya NBS hiyo orodha ya viwanda ina aina hii ya viwanda leather production,Fruits processing,Tailoring,Cements blocks,Furnituring manufacturing,Door,windows,frames,gates and grills yahani zilekazi za wajasiriamali wadogo ndio imefika hiyo idadi."Dhana ya viwanda ni pana sana na tafsiri yake ni kubwa mno" wengi wasio elewa watalubali hivyo.Pia tukumbuke tupo least developed country hivyo viwanda 52000 si mchezo waliosoma history ya Britain kabla awajafanya mapinduzi ya viwanda mwaka 1750 wanaweza kutuambia walikuwa na viwanda vya aina gani.Come on man, vinafika bhana... usiyatazame hayo mapicha kama yalivyo but OBSERVE the logic behind those photos!
Nimengia humo na orodha ya hivyo viwanda vingi ni vile vya wajasiriamali wadogo vya i aina hii leather production,Fruits processing,Tailoring,Cements blocks,Furnituring manufacturing,Door,windows,frames,gates and grills yahani zilekazi za wajasiriamali wadogo wameweja ndio imefika hiyo idadi mi nafaikiri neno zuri ni viwanda vidogo cottage industries.Orodha ya viwanda kwa Tanzania Bara - Desemba 2015
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa orodha ya viwanda kwa Tanzania Bara.
Tanzania Bara ina viwanda 50,776 kwa takwimu za Desemba 2015.
Orodha hii inaonyesha Jina la kiwanda, mkoa , wilaya na kata kilipo na shughuli kuu ya kiuchumi kufuata "Mwongozo wa Kimataifa wa Kuainisha Shughuli za Kiuchumi Toleo la Nne (International Standard Industrial Classification - Rev 4)".
Orodha ya viwanda kwa Tanzania Bara - Desemba 2015
Povuuu..Unaniuliza mimi?! Kamuulize aliekwambia kuwa jiko la kuchomea nyama nalo ni kiwanda.
Ahsante... nitaacha!Acha ujinga wa kitoto hivyo navyo viwanda? au hujui maana ya viwanda? hivi kuwa ccm kunaharibu ufahamu?
Safi sana... sasa rudi kwenye post yangu kisha connect dots na hayo uliyoyaona!Nimenda chungulia website ya NBS hiyo orodha ya viwanda ina aina hii ya viwanda leather production,Fruits processing,Tailoring,Cements blocks,Furnituring manufacturing,Door,windows,frames,gates and grills yahani zilekazi za wajasiriamali wadogo wameweka mpaka namba zao na walipo mpaka mafundi nguo wamo.ndio imefika hiyo idadi.
Msomi yupi huyo? Mwijage? Kumbe naye msomi? Anyways, kusema ukweli, kwa Tanzania ni vigumu sana kufahamu mtu aliye msomi.Hivi msomi mzimaa unakuta hajui definition ya kiwanda
Kwa kweli shame on him hata Japan haina viwanda idadi hiyo
Hvyo vimefika 52,000?.Acha ubishi wewe; Mitanzania bhana! Yaani kila kitu wao ni kupinga tu... no research, no right to speak! Nimefanya utafiti, nimegundua Kaijage yupo sahihi or else, prove otherwise:
Kiwanda cha Kuzalisha Mafuta ya Alizeti
View attachment 424474
Kiwanda cha Kuzalisha Jibini a.k.a Cheese
View attachment 424477
Kiwanda cha Kuzalisha Matofali
View attachment 424478
Kiwanda cha Kuzalisha Mafuta ya Mawese
View attachment 424479
Kiwanda cha Kubngua Korosho
View attachment 424480
View attachment 424483
Kiwanda cha Kuzalisha NondoView attachment 424485
Kiwanda cha Kuzalisha Mafuta ya Alizeti
View attachment 424487
Leteni sasa ubishi wenu... hapo nimeweka sekta chache sana lakini assume kuna viwanda 20 kwa kila sekta hapo juu... unapata viwanda vingapi hapo? Sio kila mnapinga bhana.....!!!