Waziri Mwijage: Kwa sasa Tanzania ina zaidi ya viwanda 52, 000

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
Charles-Mwijage.jpg


Kuelekea uchumi wa viwanda nchini, serikali imefanikiwa kufufua na kuanzisha viwanda ambapo kwa sasa vinavyofanya kazi vipo zaidi ya 52,000. Sekta hiyo pia imetajwa kuwa inatarajia kukuza uchumi wa watanzania asilimia 40.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya viwanda Tanzania yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam kuanzia Disemba 7 hadi 1, 2016.

“Kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda, nilipewa maelekezo kufanya mambo matatu, ikiwemo uhakikisha vilivyopo ambavyo vingi vilikuwa vinazalisha chini ya kiwango vinaongeza uzalishaji, pili vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi vinafanya kazi na la mwisho nilipewa agizo la kuhakikisha wekezaji wa ndani na nje ya wanakuja kuwekeza,” amesema na kuongeza.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu serikali hii iingie madarakani, kuna viwanda 52,000 vinafanya kazi na kwamba asilimia 40 ya watanzania uchumi wao utatokana na viwanda.”

Aidha, Mwijage amesema Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia taasisi yake ya Mamlaka na Maendeleo ya Biashara Tanzania, imeandaa maonesho yatakayokutanisha wadau wa sekta ya viwanda kwa lengo la kutangaza pamoja na kujadili fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.

Amesema maonesho hayo pia yatatoa taswira ya juhudi za ujenzi wa viwanda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.


Chanzo: Dewji Blog
 
Viwanda 52000 kwa mwaka mmoja? These people aint serious! Itakuwa wanahesabu mpaka mashine za kukoboa mahindi na za kupiga tofali. Inabidi tufafanuliwe tunamaanisha nini tunapozungumzia viwanda! Tuambiewe viwanda vidovidogo, vya kati na vikubwa ni vingapi! Sio tu viwanda. Hata mashine yangu ya kutotolea vifaranga nayo ni kiwanda!
 
Acha ubishi wewe; Mitanzania bhana! Yaani kila kitu wao ni kupinga tu... no research, no right to speak! Nimefanya utafiti, nimegundua Kaijage yupo sahihi or else, prove otherwise:

Kiwanda cha Kuzalisha Mafuta ya Alizeti

00 Alizeti.png


Kiwanda cha Kuzalisha Jibini a.k.a Cheese


00 Jibini.png

Kiwanda cha Kuzalisha Matofali

00 Matofali.png


Kiwanda cha Kuzalisha Mafuta ya Mawese

00 Mawese.png

Kiwanda cha Kubngua Korosho

00Korosho1.png

00Korosho.png

Kiwanda cha Kuzalisha Nondo
00Nondo.png

Kiwanda cha Kuzalisha Mafuta ya Alizeti
00Tomato.png

Leteni sasa ubishi wenu... hapo nimeweka sekta chache sana lakini assume kuna viwanda 20 kwa kila sekta hapo juu... unapata viwanda vingapi hapo? Sio kila mnapinga bhana.....!!!
 
Nadhani kuna usani na ukakasi katika kauli yake. Alitakiwa atuambie toka awamu hii ya 5 kushika atamu walikuta viwanda vingapi, vingapi vilikuwa kwenye operation na vingapi vilikuwa vimekufa. Mpaka sasa kuna viwanda vingapi vimeanzishwa na awamu hii ya tano na vingapi vilifufuliwa kati ya hivyo. Na vingapi ni vya serekali na vingapi vya binafsi. Sio aweke takwimu za viwanda vilivyokuwepo toka awamu zilizopita aseme ndio yeye kavileta.
 
hivi tuna viwanda vingi hiv 52,000 aisee.... kwel nchi ya viwanda tutaifikiaaa...
embu niache kuota hvyo viwanda vya makaratsi ama ni vp maana viwanda vinaonekana jaman sio chumvi ile utaweka mfukon
 
Huyo kakuta orodha ya majina ya viwanda hewa hapo ofisini kwake, naye akaamini kuwa vipo, lakini kwa idadi hiyo, labda WAZIRI kachanganya na viwanda vya wajasiriamali vya kupiga matofali ya mkono, kutengeneza vibatali
 
Back
Top Bottom